read

Aya 50 – 53: Walisujudi Isipokuwa Iblisi

Maana

Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsujudia isipokuwa Iblis;

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1(2:11), Juz. 8 (7:11) na Juzuu hii ya 15 (17: 61).

Alikuwa miongoni mwa majini akatoka kwenye amri ya Mola wake.

Yaani alitoka kwenye twaa ya mola wake. Mara nyingi tumesema kuwa sisi tunaamini kuweko majini, kwa sababu wahyi unathibitisha hilo na akili haipingi hilo; na kwamba ufafanuzi wake tunamwachia Mjuzi wa ghaibu.

Je, mnamfanya yeye na dhuria zake kuwa mawalii badala yangu?

Qur’an huwa inajifasiri yenyewe na sehemu moja inaitolea ushahidi sehemu nyingine. Katika Aya nyingi imeleta ibara ya kuwa wale wanaoichanganya haki na batili kuwa ni askari wa Iblisi na mawalii wake.

Kwa hiyo hapa inafaa kufasiri kuwa dhuria za Iblisi ni askari wake na wazaidizi wake na kwamba kizazi cha Ibilisi, askari wake na mawalii wake, ni wale wanaoichanganya batili na uongo na kuzulia haki. Sio mbali kwamba ibara ya kuwa hao ni dhuria za Ibilisi, ni kufanana vitendo vyao na vyake.

La kushangaza ni kauli ya asemaye kuwa Ibilisi ana tupu ya kiume katika paja lake la kuume na tupu ya kike katika paja lake la kushoto. Kwa hiyo aniingiza ya kiume kwenye hiyo ya kike na anapata kizazi na dhuria

Hali wao ni adui zenu?

Kila anayekupambapamba na kukudanganya na mambo ya batili au kukusifia mambo usiyokuwa nayo, basi huyo ni adui yako, ujue hilo au usijue.

Ama yule anayezua vigano juu ya Ibilisi na wengineo, basi huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na pia wa ubinadamu.

Ni uovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu.

Madhalimu ni wale wanaobadilsha twaa ya Mwenyezi Mungu kuwa twaa ya shetani; miongoni mwao ni wale wanaowachagua wafisadi kwenye vyeo na kuwafidhilisha kuliko watu wema.

Si kuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi wala kuumbwa kwa nafsi zao. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni mkono.

Ambao hawakushuhudishwa ni ibilisi na dhuria zake. Makusudio ya mkono hapa ni usaidizi. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akilitaka jambo ni kuliambia kuwa kisha likawa, hamshauri wala hamtaki msaada yeyote, kwa sababu yeye hawahitajii walimwengu.

Na wakati alipoumba vitu hakumuhudhurisha yeyote katika wao, hata kama ni mwenye takua zaidi ya wote; sikwambii tena akiwa ni mpotezaji; kama vile Ibiisi na askari wake. Madamu mambo yako hivyo, imekuwaje kuasiwa muumbaji na kutiiwa yule ambaye hawezi kujisaidia hata yeye mwenyewe au kujikinga na madhara?

Na siku atakaposema waiteni hao mliodai kuwa ni washirika wangu. Basi watawaita nao hawatawaitikia. Nasi tutaweka baina yao maangamizi.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu kesho atawaambia wale waliokuwa wakimfanyia washirika katika twaa yake: wako wapi wale ambao mliwatii na mkadai kuwa wao watawapa manufaa siku hii ya lo ngumu? Hebu waiteni tuone kama watawaitikia. Hapana! Wenyewe wana shughuli inayowashughulisha; wako katika adhabu ya moto. Kauli yake Mwenyezi Mungu kuwa watawaita na wasiwasikie ni fumbo la kukata kwao tamaa kwa matarajio waliyokuwa wakiyatarajia.

Na wahalifu wataona moto na watadhani kuwa wao watauingia wala hawatapata pa kuepukia.

Makusudio ya kudhani hapa ni kujua na kuwa na yakini. Pia kuepukia ni kuepuka na moto. Kukimbia kesho ni sawa na kujaribu kuyakimbia mauti leo hapa duniani.

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَٰذَا الْقُرْآنِ لِلنَّاسِ مِنْ كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَكَانَ الْإِنْسَانُ أَكْثَرَ شَيْءٍ جَدَلًا {54}

Na hakika tumewaeleza watu katika hii Qur’an kila aina ya mifano. Lakini mtu amezidi kila kitu kwa ubishi.

وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَنْ يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَىٰ وَيَسْتَغْفِرُوا رَبَّهُمْ إِلَّا أَنْ تَأْتِيَهُمْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ قُبُلًا {55}

Na hapana kilichowazuia watu kuamini ulipowajia uongofu na kuomba maghu- fira kwa Mola wao; isipokuwa yawafikie ya wale wa zamani au iwajie adhabu waziwazi.

وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنْذِرِينَ ۚ وَيُجَادِلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ ۖ وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَمَا أُنْذِرُوا هُزُوًا {56}

Na hatuwatumi Mitume ila wawe wabashiri na waonyaji. Na waliokufuru wanabishana kwa batili, ili waivunje haki kwayo, na wanazifanya ishara zangu na yale waliyoonywa, kuwa ni mzaha.