Aya 54 – 56: Mtu Ni Mbishi Sana
Maana
Na hakika tumewaeleza watu katika hii Qur’an kila aina ya mifano. Lakini mtu amezidi kila kitu kwa ubishi.
Makusudio ya mtu hapa sio kila mtu bali ni watu wengi zaidi, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu kwenye Aya kadhaa: “Watu wengi hawana akili” “watu wengi hawajui” watu wengi hawaamini” n.k. Qur’an ni kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kinachowaongoza kwa dalili zake na mawaidha yake na kuhimiza kushikamana na hukumu zake na mafundisho yake.
Mwenyezi Mungu amefafanua mawaidha na dalilil hizi kwa mifumo mbalimbali na akazipigia mifano mbalimbali; ikiwemo ile ya watu wawili waliotajwa katika Aya ya 32 ya Sura hii na kufananisha maisha na maji katika Aya ya 54. lakini watu hawatii akilini na wanabishana katika mambo yaliyo wazi, wakijaribu kubatishilisha haki kwa mambo ya uongo na ya kupambamba.
Na hapana kilichowazuia watu kuamini ulipowajia uongofu na kuomba maghufira kwa Mola wao; isipokuwa yawafikie ya wale wa zamani au iwajie adhabu waziwazi.
Makusudio ya uongofu ni Qur’an na ubanifu wake ulio wazi. kuomba maghufira ni kutubia na yaliyowafikia wa zamani ni maangamivu; kama yaliyowafikia kaumu ya Nuh, Lut, A’d na Thamud.
Maana ni kuwa washirikina hawajaribu kuamni au kufikiria kuamni mpaka wapatikane na moja wapo ya mambo mawili: Kwanza ni kushukiwa na adhabu ya kuwafyeka; kama ilivyowashukia waliokuwa kabla yao; ndipo wataamni; ambapo imani, wakati huo, haifai kitu; kama Firauni ambaye aliamini alipoona maangamizi na kufa maji kunafika. Jambo la pili ni kuiona adhabu ana kwa ana.
Kwa maneno mengine ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alipobainisha, katika aya zilizotangulia, kuwa Yeye ameleta dalii zilizo waziwazi na watu wengi wakakataa isipokuwa ubishi, sasa anasema kuwa dalili hizi hazifai kitu kwa watu wasioamini isipokuwa wakati wa kukata roho au wanapotishika na adhabu wanapoiona kwa macho yao au wanapoamini kuwa itawafikia tu.
Na hatuwatumi Mitume ila wawe wabashiri na waonyaji.
Huu ndio umuhimu wa Mtume kumpa habari njema ya neema yule mwenye kutii na kumuonya na adhabu yule mwenye kuasi. Maana haya yamekaririka mara nyingi. Tazama Juz. 6 (4:165).
Na waliokufuru wanabishana kwa batili, ili waivunje haki kwayo na wanazifanya ishara zangu na yale waliyoonywa, kuwa ni mzaha.
Ameziweka wazi ishara na akazithibitisha kwa ubainifu na dalili, lakini waliokufuru wakabishana na wakajaribu kuzibatilisha kwa uongo na mizaha. Makusudio ya kuzifanyia mizaha ishara za Mwenyezi Mungu hapa sio mizaha ya kusema tu; bali ni kuwa kila mweye kuijua hukumu, miogoni mwa hukumu za Mwenyezi Mungu, na asiitumie, basi yeye ni katika walioifanya Qur’an na dini ya Mwenyezi Mungu kuwa ni mchezo.
Imam Ali (a.s.) anasema: “Mwenye kuisoma Qur’an, kisha akafa akaingia motoni – kwa kutoitumia Qur’an – basi huyo ni katika waliozifanyia mzaha ishara za Mwenyezi Mungu.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِيَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ ۚ إِنَّا جَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَنْ يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۖ وَإِنْ تَدْعُهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ فَلَنْ يَهْتَدُوا إِذًا أَبَدًا {57}
وَرَبُّكَ الْغَفُورُ ذُو الرَّحْمَةِ ۖ لَوْ يُؤَاخِذُهُمْ بِمَا كَسَبُوا لَعَجَّلَ لَهُمُ الْعَذَابَ ۚ بَلْ لَهُمْ مَوْعِدٌ لَنْ يَجِدُوا مِنْ دُونِهِ مَوْئِلًا {58}
وَتِلْكَ الْقُرَىٰ أَهْلَكْنَاهُمْ لَمَّا ظَلَمُوا وَجَعَلْنَا لِمَهْلِكِهِمْ مَوْعِدًا {59}