Aya 57 – 59: Aliyekumbushwa Ishara Za Mola Wake Akazikataa
Maana
Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa ishara za Mola wake na akazipuuza na akasahau yaliyotangulizwa na mikono yake?
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameziweka wazi dalili za kuweko kwake na wajibu wa kumtii Yeye kwa mifumo mbali mbali; kisha akapiga mifano mingi ya hayo. Akamwamrisha mtu kufanya kheri na kutubia dhambi zake zilizopita, akamkataza shari na akamuhadharisha kukhalifu amri na makatazo na kuendelea na dhambi. Lakini mtu ameyapuuza yote hayo na akaitia nafsi yake kwenye maangamivu.
Hakika tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu na tumeweka kwenye masikio yao uziwi.
Umetangula mfano wake pamoja na tafsiri katika Juz. 7 (6:25) na Juz. hii ya 15 (17: 46).
Na ukiwaita kwenye uongofu hawataongoka kabisa.
Wataongoka vipi na hali kwenye nyoyo zao kuna vifuniko na kwenye masikio yao kuna uziwi. Kila asiyenufaika na mawaidha mazuri, basi huyo ni sawa na kipofu wa moyo na macho na ni kiziwi.
Na Mola wako ni mwenye maghufira na mwenye rehema, lau angeliwachukulia kwa walioyachuma, bila shaka angeliwafanyia haraka kuwaadhibu.
UmetangulamfanowakepamojanatafsirikatikaJuz.14(16:61).
Lakini wana miadi ambayo hawatapata kimbilio la kuepukana nayo.
Mausudio ya miadi hapa ni wakati wa kufika mbele ya Mwenyezi Mungu. Ni miadi isiyovunjwa wala kukimbiwa.
Imam Ali (a.s.) anasema kumwambia Mola wake: “Wewe ni wa milele huna muda na wewe ni mwishilio usioepukwa na wewe ni ahadi isiyokimbiwa. Uko mikononi mwako utosi wa kila mnyama na kwako ni marejeo ya kila nafsi.”
Na miji hiyo tuliwaangamiza walipodhulumu na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.
Makusudio ya miji hapa ni ya kina A’d,Thamud na wengineo katika umma zilizopita. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu alijaalia wakati maalum wa kuaangamia madhalimu, ukifika hawatachelewa hata saa moja wala hawatatangulizwa.
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَاهُ لَا أَبْرَحُ حَتَّىٰ أَبْلُغَ مَجْمَعَ الْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِيَ حُقُبًا {60}
فَلَمَّا بَلَغَا مَجْمَعَ بَيْنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ سَرَبًا {61}
فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَاهُ آتِنَا غَدَاءَنَا لَقَدْ لَقِينَا مِنْ سَفَرِنَا هَٰذَا نَصَبًا {62}
قَالَ أَرَأَيْتَ إِذْ أَوَيْنَا إِلَى الصَّخْرَةِ فَإِنِّي نَسِيتُ الْحُوتَ وَمَا أَنْسَانِيهُ إِلَّا الشَّيْطَانُ أَنْ أَذْكُرَهُ ۚ وَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ عَجَبًا {63}
قَالَ ذَٰلِكَ مَا كُنَّا نَبْغِ ۚ فَارْتَدَّا عَلَىٰ آثَارِهِمَا قَصَصًا {64}