Aya 60 – 64: Musa Na Makutano Ya Bahari Mbili
Lugha
Kijana wake, anaweza kuwa mwenzake au mtumishi wae. Makutano ya bahari mbili ni mahali zinapokutana bahari mbili na kuwa moja. Inasemekana hapo palikuwa ni makutano ya bahari nyeupe na bahari nyekundu. Kama ningekuwa mtalamu wa jografia, ningelichanganya kauli zote kisha nikachagua iliyo sahihi zaidi.
Maana
Na pale Musa alipomwambia kijana wake: Sitacha kuendelea mpaka nifike makutano ya bahari mbili au nitaendelea kwa muda mrefu. Basi wawili hao walipofika makutano ya bahari mbili, walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake kuponyokea baharini.
Wametofautiana kuhusu Musa, mhusika mkuu wa kisa hiki; kuwa je, ni Musa bin Imran au ni mwenginewe. Amenukuu Razi kutoka kwa Mayahudi kwamba ni Musa bin Misha bin Yusuf bin Ya’qub. Huyo ni wa mbele kuliko Musa bin Imran. Wafasiri wengi wamesema kuwa ni yule mashuhuri, Musa bin Imran. Hiyo ndiyo kauli iliyo dhahiri.
Kuhusu kijana wake, kauli iliyo maarufu ni Yoshua bin Nun, mtoto wa dada yake Musa bin Imran, mwanaafunzi wake wa karibu na khalifa wake kwa wana wa Israil. Ama yule aliyeambiwa na Musa kuwa nikufuate, kauli maarufu ni Khidhr. Lakini Mwenyezi Mungu amelinyamazia jina la kijana na la aliyemfuata. Kwa hiyo sisi tutajumlisha kwa kusema huyu ni kijana wake na yule ni swahibu wake.
Imesemekana kuwa Khidhr sio jina lake hasa bali ni msimbo. Jina lake hasa ni Fabiliya bin Malkan. Wametofautiana kuhusu kuwa je, yeye alikuwa Mtume au walii? Pia imesemekana kuwa yeye ni katika waliope- wa umri mrefu na kwamba yuko hai hadi siku ya ufufuo.
Ama sisi tunalazimika kunyamaza kuhusu utume wake na uhai wake, kwa vile hakuna dalili ya kukata shaka kutoka katika Qur’an wala Hadithi inayohusiana na mojawapo ya hayo mawili. Wala hayo hayahusiki na itikadi yetu au maisha yetu. Wengine wamesema kuwa ni Malaika. Hiyo ni kauli ya mbali sana.
Kuna riwaya inayosema kuwa mtu mmoja alimuuliza Musa: “Ni nani mwenye elimu zaidi?” Musa akasema ni mimi.
Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akataka kumfundisha kuwa juu ya kila mjuzi kuna mjuzi zidi. Kwa hiyo akampa wahyi kwamba katika makutano ya bahari mbili kuna mtu anajua ambayo huyajui. Musa akasema nitaku- tana naye vipi? Mungu akasema, chukua samaki asiyekuwa na uhai na utakapomkosa samaki huyo, basi hapo ndio kuna huyo mjuzi.
Basi Musa akamchukua samaki na akongozana na kijana wake. Akaenda mpaka Musa akachoka, akapumzika na akapata lepe la usingizi. Wakati akiwa amelala yule samaki akapata uhai na akaingia baharini. Hii ni katika miujiza ya Mwenyezi Mungu kwa Musa.
Ikiwa riwaya hii imetegema hali halisi au imetolewa kwenye maelezo ya Aya, lakini inatoa mwanga wa Aya za kisa hiki.
Walipokwishapita alimwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha machana. Kwa hakika tumepata machovu sana kwa hii safari yetu.
Baada ya Musa na kijana wake kupumzika kidogo kwenye makutano ya bahari mbili, walianza upya safari yao. Mpaka wakachoka na kuhisi njaa. Musa akataka chakula kutoka kwa kijana wake. Yule kijana alishuhudia miujiza ya samaki kupata uhai na kuingia baharini, lakini akasahau kumwambia Musa. Musa alipomtaka chakula ndio akakumbuka na akasema:
Waona! Pale tulipopumzika penye jabali basi mimi nilimsahau samaki, na hapana aliyenisahaulisha nisimkumbuke ila shetani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu.
Musa aliposikia maneno hayo akaona dalili za kupata yale aliyoyataka na akasema: Hayo ndiyo tuliyokuwa tunayataka. Basi wakarudi kwa kufuata nyayo zao. Yaani Musa na kijana wake wakarudi nyuma pale alipoingia baharini kwa kufuata ile njia yao ya kwanza.
فَوَجَدَا عَبْدًا مِنْ عِبَادِنَا آتَيْنَاهُ رَحْمَةً مِنْ عِنْدِنَا وَعَلَّمْنَاهُ مِنْ لَدُنَّا عِلْمًا {65}
قَالَ لَهُ مُوسَىٰ هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰ أَنْ تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا {66}
قَالَ إِنَّكَ لَنْ تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا {67}
وَكَيْفَ تَصْبِرُ عَلَىٰ مَا لَمْ تُحِطْ بِهِ خُبْرًا {68}
قَالَ سَتَجِدُنِي إِنْ شَاءَ اللَّهُ صَابِرًا وَلَا أَعْصِي لَكَ أَمْرًا {69}
قَالَ فَإِنِ اتَّبَعْتَنِي فَلَا تَسْأَلْنِي عَنْ شَيْءٍ حَتَّىٰ أُحْدِثَ لَكَ مِنْهُ ذِكْرًا {70}