read

Aya 65 – 70: Musa Anakutana Na Swahibu Yake

Maana

Basi wakamkuta mja miongoni mwa waja wetu tuliyempa rehema kutoka kwetu na tukamfunza elimu kutoka kwetu. Musa akamwambia: Je, nikufuate ili unifunze katika ule uongofu uliofun- zwa?

Makusudio ya ‘elimu kutoka kwetu’ ni baadhi ya elimu. Na makusudio ya elimu ni elimu ya ghaibu; yaani tulimpa kitu katika elimu ya ghaibu, akiishiria hilo kwa kuitoboa safina, na kumuua kijana. Masufi wanategemea Aya hii kusahihisha madhehebu yao wanaposema elimu ya kupewa; yaani kuwa na elimu bila ya kusoma.

Maana ni kuwa Musa na kijana wake waliporudi mpaka mahali walipop- umzika mwanzo, walimkuta mtu mingoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu, aliyepewa rehema na Mwenyezi Mungu na akamneemesha elimu ya kutosha yenye kunufaisha, Musa akamwamkia, naye akamrudishia salam. Musa akamuambia wewe ndiye niliyekuwa nakutaka je, utaniruhusu niandamane nawe na unifundishe uongofu uliofunzwa ninufaike nao?

Wanodai kuwa mtu huyo alikuwa Mtume, wanatoa dalii kwa kauli hii ya Mwenyezi Mungu: ‘tuliyempa rehema kutoka kwetu’ kwa sababu rehema ni utume.

Lakini wamesahau kuwa rehema inaenea kwenye mambo mengine zaidi ya utume; na kupatikana inayoenea zaidi haifahamishi kupatikana mahsusi. Ukisema nimekula tunda, haifahamishi kuwa lazima uwe umekula zabibu, inawezekana ni aina nyingine ya tunda.

Akasema: Hakika wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami. Na utawezaje kuvumilia yale usiyokuwa na habari nayo?

YulemtumwemaalimwambiaMusakuwalauutafuatananamiutaonamaajabu yatakayokufanya ushindwe kunyamaza, kwa sababu, kwa dhahiri yake yataonekana kuwa ni mambo mabaya na undani wake utakuwa huujui, nawe utakuwa huwezi kuyanyamazia mambo yanayonekana kuwa ni mabaya.

Akasema Musa inshallah utaniona ni mvumilivu wala sitoasi amri yako.

Musa alijitoa kwa kusema inshaalah, kuhofia asije akashindwa kujizuia; kama ilivyotokea.

Akasema: Basi ukinifuata, usiniulize kitu mpaka nianze kukutajia.

Yule mtu mwema alimpa sharti Musa kuwa asimuulize kitu kwa yale atakayoyafanya, kwa hali yoyote itakayokuwa. Musa alikubali lile sharti, kwa sababu aliondoka naye; kama unavyoonyesha ufafanuzi ufuatao:

فَانْطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا رَكِبَا فِي السَّفِينَةِ خَرَقَهَا ۖ قَالَ أَخَرَقْتَهَا لِتُغْرِقَ أَهْلَهَا لَقَدْ جِئْتَ شَيْئًا إِمْرًا {71}

Basi wawili hao wakaondoka, mpaka walipopanda jahazi akailtoboa. Akasema: Unalitoboa ili uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya.

قَالَ أَلَمْ أَقُلْ إِنَّكَ لَنْ تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا {72}

Akasema: Sikukuambia kuwa wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami?

قَالَ لَا تُؤَاخِذْنِي بِمَا نَسِيتُ وَلَا تُرْهِقْنِي مِنْ أَمْرِي عُسْرًا {73}

Akasema: Usinichukulie kwa niliyosahau, wala usinipe uzito kwa jambo langu.

فَانْطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا لَقِيَا غُلَامًا فَقَتَلَهُ قَالَ أَقَتَلْتَ نَفْسًا زَكِيَّةً بِغَيْرِ نَفْسٍ لَقَدْ جِئْتَ شَيْئًا نُكْرًا {74}

Basi wawili hao wakaondoka, mpaka wakamkuta kijana; akamuua. Akasema: Umemuua mtu asiye na kosa na hakuua! Hakikia umefanya jambo baya kabisa!