Aya 83 – 92: Dhul-Qarnain
Na wanakuuliza kuhusu Dhul-qarnain. Waambie nitawasimulia baad- hi ya habari zake.
Wametofautiana kuhusu Dhul-qarnaini huyu kuwa ni nani? Ikasemekana kuwa alikuwa miongoni mwa Malaika, lakini hili ni jambo la kushangaza. Ikasemekana alikuwa Mtume.
Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s.) kwamba yeye alikuwa ni mja mwema. Hakuna shaka ya wema wake, kwani vitendo vyake na kauli zake, alizozisajili Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika kitabu chake, zinatoa ushahidi wa ubora wake na wema wake.
Pia imesemekana kuwa ni Alexandre wa Macedonia (The great Alexandre), mwanafunzi wa Aristotle. Lakini hili nalo ni la kushangaza zaidi, kwa sababu Alexandre alikuwa ni mwabudu masanamu na Dhul-qar-nain alikuwa akimwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Amenukuu Razi na Abu Hayyani Al-Andalusi (Mhispania), kutoka kwa Abu Rayhan Al-Biruni, kuwa Dhul-qarnaini alikuwa ni mwarabu wa Yemen kutoka kabila la Himayr na jina ake ni Abu Bakr.
Vilevile wametofautiana, kuwa kwa nini aliitwa Dhul-qarnain (mwenye pembe mbii)? Ikasemekana ni kwa kuwa yeye aikuwa ni mtukufu wa wazazi wawili.
Ikasemekana kuwa ni kwa vile alikuwa na misokoto miwili ya nywele. Pia ikasemekana ni kwa vile yeye alimiliki mashariki na magharibi na mengineyo katika kauli za kutofautiana.
Ni ajabu kwa wafasiri kujishughulisha na kuwashughulisha watu kwa jambo lisilokuwa na faida yoyote ya kidunia wala akhera. Tangu lini Qur’an ikajishughulisha na majina na sababu zake? Kama hilo lingekuwa na faida basi Qur’an isingelinyamazia.
Ni kwa ajili hii ndio sisi tukatosheka na dhahiri ya Qur’an na tunasema: watu walimuuliza Mtume mtukufu (s.a.w.) kuhusu mtu aliyeitwa Dhul-qarnain, Mwenyezi Mungu akamwamrisha awaambie waulizaji kuwa nitawaambia baadhi ya habari zake.
Hakika sisi tulimmakinisha katika ardhi na tumpa sababu ya kila kitu
Makusudioyakummakinishahapaninguvunautawala.Nasababuni nyenzo zinazomfikisha mtu kwenye yale anayoyataka; kama vile elimu, uwezo, afya, mali, watu na zana. Zaidi ya hayo ni tawfiki ya Mungu na msaada wake. Nyenzo zote hizi alikuwa nazo Dhul-qarnain. Kwa hiyo akawa ni mwenye nguvu. Hii ndiyo maana ya kummakinisha katika ardhi. Aya inafahamisha waziwazi kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) analeta vitu kwa sababu zake.
Basi akafuata sababu
Mwenyezi Mungu alimwandalia njia naye akazitumia katika kheri na matendo mema. Miongoni mwazo ni kwenda kwake magharibi ambako amekuashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika kauli yake:
Hata alipofika machweo ya jua aliona linatua kwenye chemchem yenye matope meusi
Makusudio ya machweo ya jua ni miji ya magharibi. Ni wazi kuwa jua haliwezi kuingia kwenye chemchem. Kwa hio makusudio ni chemchem yenye matope meusi ya bahari ambayo yanaonekana na watu kama Jua linatua ndani yake. Bahari hii ni miongoni mwa bahari za miji ya magharibi, lakini ni bahari gani hiyo? Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi wa hilo. Sheikh Maraghi anasema ni bahari ya Atlantic.
Na hapo akawakuta watu, tukasema: Ewe Dhul-qarnain! Ama uwaad- hibu au watwae kwa wema.
Makusudio ya hapo ni hapo kwenye chemchem. Dhahiri ya Aya, ikiwa peke yake, inafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwachia Dhul-qarnain afanye atakavyo kwa watu wa mji huo, akitaka atawaadhibu na akitaka awafanyie hisani.
Na ilivyo hasa ni kuwa jambo hilo haliafikiani na uadilifu wake Mwenyezi Mungu Mtukufu. lakini tukiiunganisha Aya hii na Aya nyingine zinazoamrisha kuwaua makafiri na washirikina, ikiwa watang’ang’ania kufru na shirk, tutapata kuwa watu aliowakuta Dhul-qar-nain huko magharibi walikuwa ni makafiri na kwamba yeye aliwelezea imani wakaikataa. Unaweza kuuliza, kuwa je, inafaa kuwafanyia wema makafiri?
Jibu: Inafaa ikiwa hawakutupiga vita kwenye dini yetu wala hawakututoa majumbani mwetu. Mwenyezi Mungu anasema:
لَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ {8}
Akasema (Dhul-qarnain): Ama aliyedhulumu, basi tutamwadhibu adhabu na kisha atarudishwa kwa Mola wake amuadhibu adhabu isiyojulikana. Na ama mwenye kuamnini na akatenda mema tutamli- pa malipo mazuri na tutamwambia lililo jepesi katika amri yetu.
Hii ndio desturi ya hukumu Dhul-qarnain na utawala wake. Kwa ufupi ni kuwa, upanga ni kwa mwenye kuasi na wema ni kwa mtiifu. Hakika mali, elimu, na utawala ni neema kubwa anayowapa mtihani Mwenyezi Mungu kwayo waja wake.
Basi neema hiyo huwazidisha washari ukafiri na kupitua mipaka, lakini watu wazuri huifanya neema hiyo kuwa ni nyenzo ya kumtii Mwenyezi Mungu na kumridhisha, kama alivyofanya Dhul-qar- nain.
Kisha akafuata sababu Yaani akafuata njia. Dhul-qarnain alirejea kutoka magharibi na akaelekea mashariki ambako Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekuashria kwa kauli yake:
Mpaka alipofika mawiyo ya jua aliona linawachomozea watu tusiowawekea sitara ya kuwakinga nalo.
Makusudio ya mawiyo ya jua hapa ni upande wa mashariki, na sitara ni jengo na mfano wake, kama hema, vibanda na mapango. Maana ni kuwa Dhul-qarnain alipowasili miji ya mashariki aliwakuta watu wanaishi kwenye nchi iliyo wazi ikifikiwa na jua, wakiishi maisha ya kiporini, kama wanyama.
Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa nchi hiyo ilikuwa ufuoni mwa Afrika mashariki. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakutaja alichofanya Dhul-qarnain huko; kuwa je alimfanyia wema mwenye kuamini na aka- tenda mema na kumwadhibu mwenye kunga’ang’ania ukafiri na inadi au aliwaacha kama walivyo? Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi.
Kama hivyo tulizijua vizuri habari zake.
Yaani hii ndiyo habari ya Dhul-qarnain, tunaijua yote.
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ بَيْنَ السَّدَّيْنِ وَجَدَ مِنْ دُونِهِمَا قَوْمًا لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ قَوْلًا {93}
قَالُوا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجًا عَلَىٰ أَنْ تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدًّا {94}
قَالَ مَا مَكَّنِّي فِيهِ رَبِّي خَيْرٌ فَأَعِينُونِي بِقُوَّةٍ أَجْعَلْ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ رَدْمًا {95}
آتُونِي زُبَرَ الْحَدِيدِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا سَاوَىٰ بَيْنَ الصَّدَفَيْنِ قَالَ انْفُخُوا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَعَلَهُ نَارًا قَالَ آتُونِي أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْرًا {96}
فَمَا اسْطَاعُوا أَنْ يَظْهَرُوهُ وَمَا اسْتَطَاعُوا لَهُ نَقْبًا {97}
قَالَ هَٰذَا رَحْمَةٌ مِنْ رَبِّي ۖ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ رَبِّي جَعَلَهُ دَكَّاءَ ۖ وَكَانَ وَعْدُ رَبِّي حَقًّا {98}
وَتَرَكْنَا بَعْضَهُمْ يَوْمَئِذٍ يَمُوجُ فِي بَعْضٍ ۖ وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَجَمَعْنَاهُمْ جَمْعًا {99}
وَعَرَضْنَا جَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ لِلْكَافِرِينَ عَرْضًا {100}