Aya 101 – 106: Jahannamu Na Waliohasirika
Maana
Na siku hiyo tutawaonyesha wazi Jahannam makafiri waione.
Wenye makosa, kesho, watashuhudia kwa macho yao Jahannam kabla ya kuingizwa humo, ili wachomeke kwa aina mbili za moto: Moto wa hofu na moto wa kuungua.
Wale ambao macho yao yalikuwa kwenye pazia ya kunitaja.
Kutajwa huwa kunasikiwa na masikio. Kwa hiyo hapa maana ya pazia ya macho ni mfundo wa makafiri kwa Mtume na waumini, na kwamba wao walikuwa hawawezi kumwangalia Mtume (s.a.w.) wala waumini.
Na wakawa hawawezi kusikia utajo wa Mungu kutoka kwa Mtume wake Mtukufu.
Kwa maneno mengine ni kuwa wakosefu hawawezi kusikiza haki wala kuwatazama watu wa haki. Haya ndiyo tunayoyashuhudia kwa macho, ikiwa ni matokeo ya mzozo baina ya haki na batili na kheri na shari.
Je wanadhani waliokufuru kuwafanya waja wangu ndio walinzi badala yangu?
Makusudio ya waja wangu hapa ni viumbe ambao washirikina wali- wafanya ndio walinzi wao badala ya Mwenyezi Mungu. Hapa kuna maneno yanayokadiriwa kuwa: Je, wana dhani hawa kuwa tumeghafilika nao? Hapana! Hakika sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ni mashukio ya makafiri.
Mashukio ni mahali anapoandaliwa mgeni, vile vile linatumika neno hilo kwa maana ya nyumba. Maana ni kuwa tumewaandalia Jahannam kuwa ndio tosha yao. Hii ni sawa na kumwambia yule unayemdharau: unadhani mimi sikuwezi wewe nawe ni kama hiki kiatu?
Thamani Ya Mtu
Sema je, tuwaambie wale wenye hasara mno ya vitendo? Ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kuwa wanafanya kazi nzuri?
Ufupi wa maana ni kuwa mwenye hasara zaidi katika watu na mwenye kuhangaika bure, ni yule mjinga sana anayeuona ujinga wake kuwa ni elimu, shari yake kuwa ni kheri na uovu wake kuwa ni wema.
Hapana mwenye shaka kuwa huyo ni mwenye hasara duniani, kwa vile yeye anaishi asivyokuwa. Vile vile huko akhera, kwa vile atakutana na Mola wake akiwa na ujinga, ghururi na matendo maovu. Aya inaashiria kuwa thamani ya mtu haiwezi kupimwa kwa kuiona yeye mwenyewe. Kwa sababu mgomvi hawezi kujihukumu. Wala pia haiwezi kupimwa kwa mtazamo wa watu.
Ispokuwa mtu hupimwa kwa kipimo cha Qur’an na misingi yake na kushikamana na mafunzo yake na hukumu zake. Hupimwa kwa ukweli na uadilifu, kuinusuru haki na watu wake na kujitolea kwa hali na mali. Qur’an imejaa aina nyingi za mafunzo haya; kama vile kauli zake Mwenyezi Mungu Mtukufu zifuatazo: “...Na kuweni pamoja na wa kweli” Juz. 11 (9:119)
كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ {135}
كُونُوا أَنْصَارَ اللَّهِ {14}
كُونُوا رَبَّانِيِّينَ {79}
وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنْفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ {41}
إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ ۚ {13}
Unaweza kuuliza: Mkosaji anaweza kujiona kuwa amepatia na kwamba amefanya vizuri. Je atakuwa ni miongoni mwa waliohasirika; pamoja na kujua kuwa hakuna mwenye isma (kuhifadhiwa na madhambi) isipokuwa yule mwenye isma?
Jibu: Wenye kukosea wako aina mbili: Wa kwanza ni yule mwenye kukosea baada ya kutafiti na kuhakikisha; sawa na wanavyofanya wale wanaojitahidi, kiasi ambacho natija inayopatikana inaweza kuwa sawa na ya mtaalmu.
Hapana mwenye shaka kuwa mkoseaji huyu hawezi kuwa ni katika wale ambao juhudi zao zimepotea bure, au kuwa ni aibu ukoseaji wake; bali huyu analipwa thawabu kutokana na juhudi yake; kama ilivyoelezwa katika Hadith. Lakini kwa sharti awe na nia ya kujikosoa, yatakapofichuka makosa.
Ainayapili,nikukoseakulikotokananakujiaminikwajuujuu,kulikotokana na mawazo, bila ya kufanya utafiti, kwa vile hajui misingi ya utafiti na elimu. Au anaweza kuwa anaijua, lakini asiitumie au aitumie nusunusu, aitumie kabla ya kuikamilisha. Huyu ndiye aliye miongoni mwa wale waliopata hasara katika kazi zao, hilo halina shaka. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameamrisha kuwa na mazingatio na uthabiti na akakataza pupa na kusema bila ya ujuzi.
Baada ya hayo somo tunalolipata kutokana na Aya hii, ni kuwa tusijidanganye, tukajipa sifa tusizo nazo wala kujidanganya kwa maneno.
Vile vile ni wajibu tujihisabu nafsi zetu zinapokuwa na ghururi na kujitukuza, kabla hajatuhisabu Mwenyezi Mungu na watu. Pia rai zetu na kauli zetu tusizione kuwa ndio sawa mia kwa mia. Makosa yanatokea kwa yeyote.
Hao ndio ambao wamezikanusha ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana naye.
Mfumo wa maneno unafahamisha kuwa makusudio ya wale waliokanusha ishara za Mola wao na kukutana naye ndio wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure; ni sawa wawe wameamini ufufuo au wameukanusha. Linalozingatiwa ni imani na matendo kwa pamoja; sio imani peke yake.
Kwa hiyo vitendo vyao vimepomoka na wala siku ya kiyama hatutawapa uzito wowote.
Yaani hatutawathamini, kwa sababu hakuna heshima mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa yule mwenye takua.
Hiyo Jahanamu ndiyo malipo yao kwa walivyokufuru na wakazifanyia kejeli ishara zangu na Mitume wangu.
WalimkufuruMwenyeziMungunawakaifanyiamasikharahakinawatu wake. Moto ndio mwisho na ukomo wa ufisadi na upotevu.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا {107}
خَالِدِينَ فِيهَا لَا يَبْغُونَ عَنْهَا حِوَلًا {108}
قُلْ لَوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَنْ تَنْفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا {109}
قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَمَنْ كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا {110}