read

Aya 1-6: Zakariya

Maana

Kaaf Haa Yaa A’yn Swaad.

Umetangulia mfano wake pamoja na tafsiri katika Juz. 1, mwanzo wa Sura Baqara

Huu ni ukumbusho wa rehema ya Mola wako kwa mja wake Zakariya.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamsimulia Mtume wake mtukufu, katika Aya hizi, jinsi alivyompa rehema Zakariya na akamneemesha kwa mtoto wake Yahya. Zakariya anatokana na kizazi cha Suleiman bin Daud. Alimuoa khalat (mama mdogo) wa Maryam. Naye alikuwa ni mlezi wa Maryam. Yametangulia maelezo ya hayo katika Juz. 3 (3:38). Inasemekana kuwa Zakriya alikuwa seremala.

Alipomuomba Mola wake kwa siri Alimuomba Mola wake akiwa peke yake na akasema: Mola wangu! Mfupa wangu umedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi. Mola wangu! Sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba wewe.

Zakariya alizeeka bila ya kuwa na mtoto, kwa hiyo akamnyenyekea Mola wake, akimshtakia udhaifu wake na uzee wake. Miongoni mwa aliyoyasema ni: “Mola wangu usiniache peke yangu na Wewe ndiye mbora wa wanaorithi” (21:89). Ninakuomba ewe Mola wangu, nikiwa na matarajio ya rehema yako bila ya kukata tamaa. Vipi nikate tamaa na hali hujawahi kuyaangusha matarajio yangu kwako.

Na mimi nahofia jamaa zangu baada yangu na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako atakayenirithi mimi na arithi ukoo wa Ya’qub. Ewe Mola wangu mjaaliye mwenye kuridhisha.

Neno la kiarabu ‘mawalii’ lililofasiriwa jamaa, lina maana ya ndugu wa upande wa baba. Kwa hiyo Zakariya akiwa mzee na mkewe akiwa tasa, alihofia kurithiwa na binamu zake ambao ni wana wa Israil. Inasemekena walikuwa ni waovu.

Na hilo si mbali kwa Waisrail, kuwa wakirithi watawafanyia uovu watu na kuwafanyia ufisadi kwenye dini yao na dunia yao. Pamoja na uzee wake Zakariya na utasa wa mke wake, bado alikuwa na mategemeo makubwa kwa muumba wake, ndio maana akamuomba amtimizie haja yake.

يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَلْ لَهُ مِنْ قَبْلُ سَمِيًّا {7}


Ewe Zakariya! Hakika sisi tunakubashiria mwana, jina lake



ni


Y


ahya,



hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.

قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا وَقَدْ بَلَغْتُ مِنَ الْكِبَرِ عِتِيًّا {8}


Akasema: Ewe Mola wangu!


V


ipi nitakuwa na mwana na hali mke wangu ni tasa, na mimi nimekwishafikia ukongwe



katika



uzee?

قَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَقَدْ خَلَقْتُكَ مِنْ قَبْلُ وَلَمْ تَكُ شَيْئًا {9}


Akasema, ndio hivyo hivyo Mola wako amesema, haya kwangu ni mepesi. Na hakika nilikuumba wewe zamani na hukuwa



kitu.

قَالَ رَبِّ اجْعَلْ لِي آيَةً ۚ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَ لَيَالٍ سَوِيًّا {10}


Akasema: Mola



wangu nijaalie



ishara. Akasema, ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa masiku matatu,



na



hali



ni



mzima.

فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ مِنَ الْمِحْرَابِ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ أَنْ سَبِّحُوا بُكْرَةً وَعَشِيًّا {11}


Akawatokea



watu



wake



kutoka mihirabuni, akawaashiria kuwa mumsabihi asubuhi na jioni


.