Aya 12 – 15: Yahya
Ewe Yahya!
Kauli hii inaelezea moja kwa moja kuwa Yahya amekwishazaliwa, amekuwa na akili ya kufahamu na kutia maanani na ana uwezo wa kutumia Tawrat ambayo ndiyo aliyoikusudia Mwenyezi Mungu aliposema:
Kishike kitabu kwa nguvu.
Maana ya kukishika kwa nguvu ni kukitumia kwa bidii na ikhlasi. Kisha akamsifu Yahya kwa sifa zifuatazo:
Na tulimpa hukumu angali mtoto na tukampa huruma itokayo kwetu na utakaso na alikuwa ni mwenye takua na mwema kwa wazazi wake wala hakuwa jeuri muasi.
Makusudio ya kupewa hukumu udogoni ni kujua dini mapema udogoni. Hii ni neema Mwenyezi Mungu aliyomhusisha nayo Yahya; kama alivyomhusisha kwa kuzaliwa na wazazi wazee. Mwenyezi Mungu humhusisha kwa rehema yake amtakaye. Baadhi ya riwaya zinasema kuwa siku moja watoto walimwambia Yahya: “Twendeni tukacheze.” Yahya akasema: “Hatukuumbwa kwa ajili ya kucheza, twendeni tukaswali.”
Makusudio ya upole ni upole kwa waja. Utakaso ni utwahara na utakatifu. Takua ni kumtii Mwenyezi Mungu. Kuwatendea wema wazazi wawili ni kinyume cha kuwaudhi.
Kauli yake Mwenyezi Mungu: Wala hakuwa ni jeuri muasi ni kuunganisha kwa kufafanua. Kwa sababu Mwenye utakaso na takua hawezi kuwa jeuri muasi.
Na amani iwe juu yake, siku alipozaliwa na siku atakapokufa na sikuatakapofufuliwa
Hili ni fumbo la kuwa Yahya ni Mwenye kuridhiwa mbele ya Mwenyezi Mungu duniani na Akhera. Ilivyo ni kuwa kumridhia kwake Yahya (a.s.) ni matokeo ya sifa alizomsifu nazo Mwenyezi Mungu.
Unaweza kuuliza: Kwanini Mwenyezi Mungu amemuhusisha Yahya na sifa hizi tele akiwa bado angali mdogo?
Jibu: Hakika Mwenyezi Mungu ana mambo yake kwa viumbe vyake. Anaweza akampa fadhila mdogo na akamnyima mkubwa. Na kila kutoa kwake na kuzuia kwake kuna hekima ambayo akili inaweza kujua na isiweze kujua. Lakini akili huwa inajaribu; kama ifuatavyo:
Sio mbali kuwa makusudio ya kusifika Yahya na sifa hizi katika rika hilo ni kutoa hoja kwa Wana wa Israil, watakapohitilafiana naye na wasikilize nasaha zake na mwito wake. Alimuumba Isa bila ya baba, “ili tumfanye kuwa ni ishara kwa watu na rehema itokayo kwetu.” Itakuja Aya hii sehemu inayofuatia hii.
Pamoja na hoja hii ya kunyamazisha, lakini bado walimuasi Yahya na wakamfanyia uadui; mwisho wakamuua yeye na baba yake, si kwa lolote isipokuwa ni kwa kuwakataza mabaya. Hili si ajabu kwa yule aliyesema kuwa mikono ya Mwenyezi Mungu imefunga au Mungu ni fukara na sisi ni matajiri. Rudia Juz. 6 (5:64).
Katika kitabu Qasasul-anbiya (Visa vya mitume) imeelezwa kuwa Herod mfalme wa Palestina, wakati huo, alimpenda Herodias, binti wa kaka yake, kutokana na uzuri wake, na akataka kumuoa. Yahya alipopinga hilo
Herodias alichukia na akatoa sharti kwa ami yake kuwa mahari yake yawe kichwa cha Yahya. Kwa hiyo Mfalme akamchinja Yahya na akampelekea mpenzi wake zawadi hiyo ya kichwa.
KunariwayamashuhuriiliyopokewakutokakwaAlibinHuseinbinAli (a.s.) kwamba baba yake, alipokuwa akielekea Iraq, alikuwa akimkumbuka sana Yahya na akisema: “Ni katika utwevu wa dunia kwa Mwenyezi Mungu, kwamba kichwa cha Yahya bin Zakariya kitolewe zawadi kwa kahaba miongoni mwa makahaba wa ki bani Israil.”
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انْتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا {16}
فَاتَّخَذَتْ مِنْ دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا {17}
قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَٰنِ مِنْكَ إِنْ كُنْتَ تَقِيًّا {18}
قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا {19}
قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا {20}
قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ ۖ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِنَّا ۚ وَكَانَ أَمْرًا مَقْضِيًّا {21}