Aya 22 – 26: Mimba Ya Isa
Maana
Basi akachukua mimba yake akaondoka nayo mahali mbali
Inasemekana kuwa Jibril alimpulizia kwenye gauni lake, ikawa ndiyo sababu ya kushika mimba. Rejea ya kauli hii ni dhahiri ya Aya hii:
وَالَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهَا مِنْ رُوحِنَا {91}
وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِنْ رُوحِنَا {12}
MarakwamaratumeishiriakuwaQur’an inajifasiriyenyewe;yaaniAya zinafasiri Aya nyingine. Kwa sababu chimbuko lake ni moja. Tukiangalia msingi huu tutafahamu, kwa ujumla wake wote kuwa makusudio ya kupulizia ni kuumba na kutengenezwa mimba, na makusudio ya Roho ni Isa mwenyewe; kama inavyofahamisha Aya hii: “Masih Isa bin Maryam ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na neno lake tu alilompelekea Maryam, na ni roho iliyotoka kwake.” Juz.6 (4:171)
Maana ya ‘neno lake’ ni neno ‘kuwa,’ambalo anaumbia nalo vitu. Na maana ya ‘alilompelekea Maryam’ ni kuwa Maryam au tumbo lake ndio mahali pa kuumbwa. Kwa ufafanuzi zaidi angalia huko. Kwa vyovyote ilivyo ni kwamba Maryam alipojihisi ana mimba alijitenga kando na watu wake kwa kuona haya.
Uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya nikawa mwenye kusahaulika kabisa.
Haya ni maneno anayoyasema mtu yeyote anapozongwa na matatizo makubwa, anatamka kupunguza msongo wa moyo na huzuni yake.
Pakanadiwa kutoka chini yake kwamba usihuzunike; hakika Mola wako amejaalia chini yako kijito cha maji.
Yanayokuja akilini mwanzo, kutokana na mfumo wa maneno, ni kuwa aliyenadi ni Isa (a.s.) na wala sio Jibril, kama wanavyodai wafasiri wengi. Kunadi huku ni miongoni mwa miujiza ya Isa; sawa na kuzaliwa na kufufua kwake wafu.
Isa aliendelea kumwambia mama yake:
Na litikise kwako shina la mtende utakuangushia tende freshi zilizo mbivu.
Inasemekana huo haukuwa msimu wa tende. Kwa hiyo kupatikana tende ilikuwa ni muujiza. Hili haliko mbali, kwa sababu kila kitu hapa ni muujiza tu na tamko lenyewe pia linafahamisha hivyo.
Basi kula tende na kunywa kutoka kwenye kijito na uburudishe jicho.
Yaani poa moyo kwa kupata mtoto mwenye kubarikiwa.
Na pindi ukimuona mtu yeyote na akakuuliza kuhusu mtoto, basi sema kwa ishara kuwa hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema ya kufunga kwa kunyamaza. Hiyo ndiyo iliyokuwa Swaumu ya waisrail wakati huo.
Kwa hiyo leo sitasema na mtu.
Hapana haja ya ufafanuzi hapa, isipokuwa kufasiri matamshi, kwa sababu akili haina nafasi katika maudhui haya maadamu dhahiri ya maneno haigongani na hukumu ya kiakili katika maudhui haya. Tazama Juz. 3 (3:45 – 51) kifungu cha ‘Lisilowezekana kiakili na kidesturi.’
فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ ۖ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا فَرِيًّا {27}
يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا {28}
فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ ۖ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَنْ كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا {29}
قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا {30}
وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنْتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا {31}
وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا {32}
وَالسَّلَامُ عَلَيَّ يَوْمَ وُلِدْتُ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا {33}
ذَٰلِكَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قَوْلَ الْحَقِّ الَّذِي فِيهِ يَمْتَرُونَ {34}
مَا كَانَ لِلَّهِ أَنْ يَتَّخِذَ مِنْ وَلَدٍ ۖ سُبْحَانَهُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ {35}