Aya 27 – 35: Umeleta Kitu Cha Ajabu
Maana
Akaenda naye kwa jamaa zake amembeba.
Baada ya Maryam kuzaa, alimbeba mwanawe kwenda naye kwa watu wake, akiwa na utulivu bila ya kuwa na wasiwasi; kwani mimba ambayo ilikuwa ni sababu ya kutuhumiwa kwake, sasa ndiyo yenye ushahidi wa kweli wa usafi wake.
Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu kwa kudai kupata mimba bila ya kuguswa na mtu, huo ni uzushi.
Ewe dada wa Harun! Huyu ni nduguye Musa, na yeye Maryam ni katika kizazi chao. Makusudio ya kumtaja ni kuwa asili yake ni watu wema na kwamba shina likiwa zuri matawi pia yanatakiwa yawe mazuri, sasa imekuwaje kutokewa na yaliyomtokea ambayo hakuna mfano aliyetokewa na hayo?
Baba yako hakuwa mtu muovu wala mama yako hakuwa kahaba.
Unafanana na nani wewe kwa kitendo chako hiki? Hawezi kufanya hivi ila binti wa muovu au wa mama muovu.
Ndipo akaishiria kwake
Yaani kwa mtoto aweze kushuhudia usafi wake naye ni mkweli zaidi ya wanaoshuhudia, kwa sababu anatamka kwa lugha ya Mwenyezi Mungu.
Wakasema kwa mshangao. Tutamsemezaje aliye bado mdogo susuni?
Lakini yule aliye susuni alianza kuwasemesha kabla wao hawajaanza na akasema: Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu amenipa Kitabu na amenifanya ni nabii.
Yaani atanifanya ni nabii baadaye, kwa sababu kitoto kichanga hakiwezi kuongoza watu na kuwa ni hoja kwao. Ikiwa yeye mwenyewe hana majukumu kwa kauli yake wala vitendo vyake. Atawezaje kuwa na majukumu ya kufikisha risala ya Mwenyezi Mungu kwa waja wa Mwenyezi Mungu?
Huko nyuma tumesema kuwa alitumwa kuwa Mtume akiwa na miaka 30; na kwamba alizungumza utotoni ili kumsafisha mama yake na tuhuma ya zina na uchafu; si kwa kuwa alikuwa ni nabii aliyetumwa. Angalia kifungu ‘Isa na utume wa utoto’ katika Juz.7 (5:109 –111).
Na amaenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo.
Kila anayewanufaisha watu kwa namna moja au nyingine basi ni mweye kubarikiwa na kila mwenye kumdhuru mtu mmoja - sikwambii watu wengi- basi huyo ni muovu na mfisadi.
Na ameniusia Swala na Zaka muda wakuwa niko hai na kumtendea mema mama yangu.
Yeye mwenyewe anakiri utumishi na utiifu kwa Mungu na kukana kuwa ni Mungu, mwana wa Mungu au mshirika wake; kama wanavyodai wanaswara (wakristo).
Wala hakunifanya niwe jeuri muovu; kama wanavyodai mayahudi. Bali ni mja mwema na Mtume; kama wanvyoitakidi waislamu.
Na amani iwe juu yangu, siku niliyozaliwa na siku nitakayokufa na siku nitakayofufuliwa.
Umepita punde mfano wake katika Aya 15 ya sura hii.
Huyo ndiye Isa mwana wa Maryam, kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.
Hilindilonenolakweli,lakielimunalakiadilifu,kuhusuBwanaMasih.
Sio mjeuri kama wanavyosema mayahudi; wala si Mungu, mwanawe au mshirika wake; kama wasemavyo wanaswara. Yeye ni Nabii anayefikisha risala ya Mola wake na ni mja miongoni mwa waja wake, anaswali na kutoa Zaka. Vile vile yeye ni mwenye kubarikia anayewanufaisha watu. Pia ni mnyenyekevu anayemfanyia wema mama yake.
Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Yeye ametakasika! Anapolipitisha jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa
Lau Mwenyezi Mungu angelikuwa na watoto wangelijifichia kheri zote na baraka na kuzizuia wengine wasizipate. Pia wangeharibu yale aliyoten- geneza vizuri baba na ulimwengu wangeliujaza shari na upotevu; sawa na wanavyofanya baadhi ya watoto wa viongozi siku hizi. Umepita mfano wake katika Juz. 3 (3:59) na katika Juz.15 (18: 111).
وَإِنَّ اللَّهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَٰذَا صِرَاطٌ مُسْتَقِيمٌ {36}
فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِنْ بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِلَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ مَشْهَدِ يَوْمٍ عَظِيمٍ {37}
أَسْمِعْ بِهِمْ وَأَبْصِرْ يَوْمَ يَأْتُونَنَا ۖ لَٰكِنِ الظَّالِمُونَ الْيَوْمَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ {38}
وَأَنْذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الْأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ وَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ {39}
إِنَّا نَحْنُ نَرِثُ الْأَرْضَ وَمَنْ عَلَيْهَا وَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ {40}