read

Aya 41-50: Ibrahim

Na mtaje Ibrahim katika Kitabu hakika yeye alikuwa mkweli sana, Nabii.

Makusudio ya Kitabu hapa ni Qur’an. Ukweli ni sifa bora na ya ukamilifu zaidi. Tunalolifahamu kutokana na wasifu wa utume baada ya ukweli, ni kuwa yeye kwa maumbile yake ni mkweli hata kama si mtume.

Katika Juz. 7: (6:74) tumetaja tofauti za maulama katika makusudio ya baba wa Ibrahim, aliyetajwa katika Qur’an, kuwa je, ni baba yake wa hakika au ni baba wa kimajazi au ni ndugu wa baba? Tukasema huko, kuwa hakuna faida ya mzozo huu na kwamba lililo wajib kwa mwislamu ni kuamini utume wa Ibrahim (a.s.). Ama kuitakidi uislamu wa baba yake hilo halihusiani na dini; hasa kwa kuwa dhahiri ya Qur’an inafahamisha ukafiri wake.

Kwa vyovyote iwavyo, ni kuwa Ibrahim alimpa mwito baba yake, awe wa kimajazi au wa kihakika, wa uislamu na akamwambia katika yale aliyomwambia:
Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa na chochote?

Baba yake alikuwa akiabudu masanamu, kwa hiyo akamuhoji kwa manti- ki ya kiakili na kimaumbile. Mawe yaliyonyamaza, hayadhuru wala kunufaisha, unayaabudu na kuyasujudia? Iko wapi akili yako na fahamu yako?
Ewe baba yangu! Hakika imenifikia elimu isiyokufikia wewe, Basi nifuate mimi nitakuongoza njia iliyo sawa.

Kila anayekataa ibada ya masanamu anakuwa na ufahamu na akili zaidi kuliko wanayoyaabudu; sikwambii tena mitume wanaopata elimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa kutojua kunakuwa ni udhuru kwa yule asiyejua, lakini masanamu hayo yenyewe hayawezi kuacha udhuru kwa anayeyaabudu.

Ewe baba yangu! Usiabudu shetani. Hakika shetani ni Mwenye kumuasi Mwingi wa rehema.

Makusudio ya kumwabudu shetani ni kumtii, kwa sababu Mwenye kukitii kitu atakuwa amekiabudu. Kwa hiyo basi kila anayemuasi Mwenyezi Mungu atakuwa amemuabudu shetani.

Ewe baba yangu! Mimi nakuhofia isikupate adhabu ya Mwingi wa rehema ukawa ni walii wa shetani.

Walii wa shetani inaweza kuwa kwa maana ya kutawaliwa na shetani au kwa maana ya kuwa mtawala wa shetani katika kuabudu masanamu; sawa na kusema: watu wanajilinda na shetani na shetani anajilinda na watu. Katika makadirio yote, ni kuwa lengo ni kuhofisha na kuhadharisha kumtii shetani na kumfuata.

Akasema: Unaichukia miungu yangu ewe Ibrahim! kama hutakoma, basi lazima nitakupiga mawe na niondokelee mbali kwa muda

Tulipokuwa tukisoma huko Najaf, siku moja tukiwa tumemzunguka mwal- imu wetu akifafanua maswala muhimu ya elimu ya misingi ya fiqh (Usuulul-fiqh) baada ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wake wote wamefahamu, alihitimisha darasa, lakini ghafla mmoja wa wanafunzi akamuuliza swali ambalo lilikuwa mbali kabisa na maudhui ya darasa. Basi mwalimu akaachana naye akawaangalia wanafunzi wengine na akasema:

“Hapo zamani palikuwa na mwanafunzi mmoja aliyejifundisha masuala ya Swaumu kwa mwalimu kwa muda wa zaidi ya mwezi. Baada ya kumaliza darasa yake mwalimu akadhania kuwa mwanafunzi wake ameelewa kila kitu kinachohusiana na Swaumu, lakini mwanafunzi akamwambia umeeleza sana na ukafafanua masuala ya Swaumu, lakini hatukufahamu kuwa Swaumu inakuwa usiku au mchana?!”

Haya hasa ndiyo yaliyompata Ibrahim pamoja na baba yake. Baada ya kumpa dalili zote na kumbembeleza kwa kumwambia ‘ewe baba yangu’ mara nne, lakini alimjibu kwa kumwambia kuwa kweli umeazimia kutowaabudu miungu pamoja nami? Ikiwa ni kweli umeazimia hivi, basi mimi sina jengine ila nikurujumu na kukuua au uniondokelee mbali nisikuone machoni mwangu.

Akasema Ibrahim: Amani iwe juu yako (salamun alayka)! Nitakuombea msamaha kwa Mola wangu. Hakika yeye ananihurumia sana.”

Yaani Mwenyezi Mungu anamwitikia maombi yake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (9:114).

Nami najitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu na ninamuomba Mola wangu asaa nisiwe na bahati mbaya.

Ibrahim aliwabughudhi watu wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akawaondokea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akambadilisha familia bora kuliko wao, pale alipompa Is-haq na baada yake Ya’qub bin Is-haq na akawatukuza kwa utume.
Hayo ndio makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Alipojitenga nao na yale wanayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tulimpa Is-haq na baada ya Is-haq ni Ya’qub na kila mmoja tukamfanya Nabii.

Hakuna aliyeacha kitu katika mambo ya dunia kwa kutengeneza dini yake ila humbadilishia bora zaidi yake.

Na tukawapa katika rehema zetu

Mwenyezi Mungu hakubainisha aina ya alichowapa, kwa sababu neno rehema zetu linaashiria hilo. Inatosha kuwa ni zawadi radhi za Mwenyezi Mungu na neema zake.

Na tukawajaalia kuwa na sifa za kweli tukufu.

Makusudio ya sifa za kweli ni sifa wanazozikariri watu kizazi baada ya kizazi kusifia Ibrahim, Is-haq, Ismail na Ya’qub.

Aya hizi zinatia mkazo kwamba mwenye kumfanyia ikhlasi Mungu naye Mungu humsafisha na anakuwa pamoja naye popote alipo; sawa na alivyomfanyia Ibrahim (a.s.).

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مُوسَىٰ ۚ إِنَّهُ كَانَ مُخْلَصًا وَكَانَ رَسُولًا نَبِيًّا {51}


N


a


mtaj


e


Mus


a



katika


Kitabu, hakika yeye alikuwa


n


i


Mweny


e


kutakasw


a


na


alikuwa



Mtume



Nabii

وَنَادَيْنَاهُ مِنْ جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا {52}


N


a



tulimwit


a


upand


e


wa


kuume



wa


T


ur na



tukamkurubisha



kunong’ona



naye.

وَوَهَبْنَا لَهُ مِنْ رَحْمَتِنَا أَخَاهُ هَارُونَ نَبِيًّا {53}


Na tukampa kutokana na rehema zetu nduguye, Haruna,



awe



Nabii

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِسْمَاعِيلَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صَادِقَ الْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًا نَبِيًّا {54}


N


a



mtaj


e



katik


a



Kitabu,


Ismail. Hakika yeye alikuwa mkweli wa ahadi na alikuwa Mtume,



Nabii.

وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُ بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ وَكَانَ عِنْدَ رَبِّهِ مَرْضِيًّا {55}


N


a


alikuw


a



akiwaamrisha


watu wake swala na zaka na alikuwa mbele ya Mola wake mwenye



kuridhiwa.

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِدْرِيسَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَبِيًّا {56}


N


a



mtaj


e



katik


a


Kitabu,


Idris


.


Hakik


a


yey


e


alikuwa


mkweli wa ahadi na alikuwa Mtume,



Nabii

وَرَفَعْنَاهُ مَكَانًا عَلِيًّا {57}


Na



akamwinua



mahali



pa



juu

أُولَٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مِنَ النَّبِيِّينَ مِنْ ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِنْ ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُ الرَّحْمَٰنِ خَرُّوا سُجَّدًا وَبُكِيًّا ۩ {58}


Hao ndio



ambao Mwenyezi


Mung


u


amewaneemesha


miongoni mwa manabii katika



uzao



wa Adam



na



katika wale tuliowapandisha pamoja na Nuh na katika uzao wa Ibrahim na Israil na katika


wal


e


tuliowaongo


a


na


tukawateua.


W


anaposomewa


A


ya za Mwingi wa


r


ehema huanguka



kusujudu



na



kulia.