read

Aya 59 – 65: Wakaja Baada Yao Walio Wabaya

Wakafuata baadae wazawa wabaya walioiacha swala na wakafuata matamanio

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwataja Mitume watakatifu, anaashiria waovu waliowafuatilia, akawapa wasifu wa kuwacha ibada ya mwingi wa rehema na kumfuata shetani. Maana haya yanafupika kwenye ibara hii: ‘Bora ni waliopita, wabaya ni waliokuja’

Basi watakujakuta malipo ya ubaya. Shari na adhabu ikiwa ni malipo ya maasi yao na inadi yao.

Ispokuwa waliotubu, wakaamini na wakatenda mema. Hapo basi wataingia Bustani (Peponi) wala hawatadhulumiwa chochote.

Tafsiri nzuri ya Aya hii ni kauli ya Mtume mtukufu (s.a.w.): “Mwenye kutubia dhambi ni kama asiye na dhambi”. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:54).

Bustani za milele. Zipo daima, neema yake haikatiki wala hakimwi mkaaji wake.

Ambazo Mwingi wa rehema aliwaahidi waja wake kwa ghaibu.

Makusudio ya waja wake hapa ni waumini wenye ikhlasi. Kwa ghaibu ni kuwa wao waliamini Pepo ikiwa iko ughaibuni. Mwenyezi Mungu ame- wasifu waumini kuwa wanaoamini ghaibu katika Aya kadhaa.

Hakika Yeye ahadi yake itafika.

Yaani Mwenyezi Mungu havunji ahadi.

Hawatasikia humo upuuzi isipokuwa salama tu na watapata humo riziki zao asubuhi na jioni.

Katika maisha ya dunia ni upuuzi uwongo na matusi, lakini Peponi ni kauli njema na riziki isiyokoma. Asubuhi na jioni ni fumbo la kudumu, kwa sababu Peponi hakuna asubuhi wala jioni.

Hiyo ndiyo Pepo tutakayowarithisha katika waja wetu waliokuwa na takua.

Neni ‘tutawarithisha’ linatambulisha kuwa Pepo ni ya wenye takua. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Hao ndio warithi ambao watarithi Firdausi. Humo watadumu” (23: 11)

Wala hatuteremki ila kwa amri ya Mola wako. Ni yake Yeye yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu na yaliyoko baina ya hayo.

Katika Tafsiri Tabariy na Tabrasi, imeelezwa kwamba wahyi ulichelewa kushuka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.). Aliposhuka Jibril, Mtume akamuuliza ni lipi lililokuzuia hata usitutembelee mara kwa mara, kama ulivyokuwa ukifanya? Ikashuka Aya hii. dhahiri yake inaafikiana na Aya hii, hasa kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na Mola wako si mwenye kusahau.

Maana ni kuwa amri ya kuteremshwa wahyi ni ya Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye ndiye mmiliki wa kila kitu na ujuzi wake umekizunguka kila kitu na kila mahali, kilipokuwa na kitakapokuwa.

Kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘yaliyoko mbele yetu’ ni ishara ya yatakayokuja, na ‘yaliyoko nyuma yetu’ ni yaliyopita na ‘yaliyoko baina ya hayo’ ni yaliyoko sasa.

Mola wa mbingu na rdhi na vilivyo baina yake.

Ambaye ni Mola wa ulimwengu itakuwa muhali kwake kusahahu.

Basi muabudu Yeye na uwe na subira kwa ibada yake.

Hii ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake kwamba aendelee na na umuhimu wake wa kufikisha (tabligh) mwito, kwa sababu hiyo ni katika ibada kubwa, na kuvumilia maudhi katika njia yake.

Je, unamjua somo yake?

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hana kifani na chochote, katika sifa zake za utukufu na ukamilifu. Basi anayekuwa hivyo anawajibikiwa na kuabudiwa na kutiiwa.

وَيَقُولُ الْإِنْسَانُ أَإِذَا مَا مِتُّ لَسَوْفَ أُخْرَجُ حَيًّا {66}



N


a


mt


u


husema


:



hivi


nitakapokufa, ni kweli nitatolewa



niwe



hai?

أَوَلَا يَذْكُرُ الْإِنْسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِنْ قَبْلُ وَلَمْ يَكُ شَيْئًا {67}


Je



hakumbuki



mtu



ya



kwamba tulimuumba kabla na hali hakuwa



chochote?

فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَالشَّيَاطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ جَهَنَّمَ جِثِيًّا {68}


Basi



naapa



kwa



Mola



wako!


Hakik


a


tutawakusany


a


na


mashetani. Kisha tutawahud


hurish


a


kandokand


o


ya Jahanna


m


na


o


wamepiga


magoti

ثُمَّ لَنَنْزِعَنَّ مِنْ كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى الرَّحْمَٰنِ عِتِيًّا {69}


Kisha



kwa



hakika



tutawatoa katika kila kundi wale miongoni



mwao



waliozidi



kumwasi Mwingi



wa



r


ehema

ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِالَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا {70}


T


ena



hakika



sisi



tunawajua


vizur


i


wanaostahik


i


kuun


guzwa



humo.

وَإِنْ مِنْكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَقْضِيًّا {71}


Hakuna



miongoni



mwenu



ila ni mwenye kuifikia. Ni hukumu ya Mola wako, ni lazima itimizwe.

ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوْا وَنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا {72}


Kish


a


tutuwaoko


a


wale


wenye takua na tutawaacha


madhalim


u


hap


o


wamepiga


magoti.