read

Aya 66 –72: Kweli Nitatolewa Hai?

Na mtu husema: hivi nitakapokufa, ni kweli nitatolewa niwe hai? Je hakumbuki mtu ya kwamba tulimuumba kabla na hali hakuwa chochote?

Kwa ufupi ni kuwa, hakuna kitu mbele ya mwenye kupinga ufufuo anachopima nacho isipokuwa kustaajabu; vipi utarudi uhai baada ya kumuondokea binadamu? Jibu ni kuwa ataurudisha mara ya pili yule aliyeuleta kwanza: ‘tulimuumba kabla na hali hakuwa chochote’. Maana ya Aya hii yamekaririka katika Aya kadhaa. Angalia Juz. 1 (2:28-29), Juz. 2 (4:87) na Juz. 13 ( 13:5).

Basi naapa kwa Mola wako! Hakika tutawakusanya na mashetani.

Tutawakusanya hao wanaopinga ufufuo. Makusudio ya kukusanywa ni kutolewa kwao makaburini mwao wakiwa madhalili, wamedharaulika pamoja na wale waliowapoteza

Kisha tutawahudhurisha kandokando ya Jahannam nao wamepiga magoti.

Baada ya kutoka makaburini mwao na hali mbaya hiyo, Malaika watawakalisha wakiwa wamepiga magoti, kandokando ya Jahannam ili waiangalie, wazidi machungu na masikitiko.

Kisha kwa hakika tutawatoa katika kila kundi wale miongoni mwao waliozidi kumwasi Mwingi wa rehema.

Baada ya kuizunguka Jahannam wakiwa wamepiga magoti, wakiwa ni makundi mbali mabali, Mwenyezi Mungu kwanza atachukua kiongozi kutoka kila kundi na kuwatupa katika Jahannam, kisha wanaowafuatia. Kila mmoja atawekwa mahali pake panapomstahiki katika adhabu ya kuungua

Tena hakika sisi tunawajua vizuri wanaostahiki kuunguzwa humo

Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anajua maovu anayoyafanya kisiri na kidhahiri na atamlipa anavyostahili.

Mwenye madhambi makubwa adhabu yake ni kubwa, kisha anayefuatia na mwingine anayefuatia “Na watakuta waliyoyafanya yamehudhurishwa” Juz. 15 (18: 49).

Hakuna miongoni mwenu ila ni mwenye kuifikia. Ni hukumu ya Mola wako, ni lazima itimizwe. Kisha tutuwaokoa wale wenye takua na tutawaacha madhalimu hapo wamepiga magoti.

Makusudio ya kufikia hapa ni kuona na kushuhudia, kwa sababu waumini wataepushwa na moto; kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُمْ مِنَّا الْحُسْنَىٰ أُولَٰئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ {101}


“Hakika wale ambao wema wetu umewatangulia wataepushwa nao” (21:101).

Pia kwamba kuadhibiwa mtiifu kunapingana na uadilifu wa Mungu. Maana ni kuwa hakuna yeyote kati ya mwema na muovu ila atauona waziwazi. Muovu atauona kisha aungie hali amepiga magoti na mwema atauona na aupite hali ya kushukuru neema ya kuokoka na mwako wake:

فَمَنْ زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ {185}


“Mwenye kuepushwa na moto akatiwa Peponi, basi huyo amefuzu” Juz. 4 (3:185


)

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا أَيُّ الْفَرِيقَيْنِ خَيْرٌ مَقَامًا وَأَحْسَنُ نَدِيًّا {73}


Na



wanaposomewa



A


ya



zetu


zilizowazi


,


waliokufuru


huwaambia walioamini: lipi katika makundi mawili lenye


che


o


kizur


i


n


a



lilil


o


bora barazani

وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُمْ مِنْ قَرْنٍ هُمْ أَحْسَنُ أَثَاثًا وَرِئْيًا {74}


N


a


karn


e


ngapi


tuliziangamiza zilizokuwa na


mapamb


o


mazur


i


zaid


i


na


wazuri



zaidi



kwa



mandhari?

قُلْ مَنْ كَانَ فِي الضَّلَالَةِ فَلْيَمْدُدْ لَهُ الرَّحْمَٰنُ مَدًّا ۚ حَتَّىٰ إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ إِمَّا الْعَذَابَ وَإِمَّا السَّاعَةَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ شَرٌّ مَكَانًا وَأَضْعَفُ جُنْدًا {75}


Sema


:



aliy


e


katik


a



upotofu


bas


i


Mwing


i


w


a r


ehema


atampa muda mpaka ayaone aliyoahidiwa





ama



ni



adhabu au ni saa. Hapo ndipo watajua ni nani mwenye makao


mabay


a


n


a


mweny


e


askari


dhaifu

وَيَزِيدُ اللَّهُ الَّذِينَ اهْتَدَوْا هُدًى ۗ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِنْدَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ مَرَدًّا {76}


N


a


Mwenyez


i


Mungu


huwazidishia uwongofu wale walioongoka. Na mema yenye kubaki ni bora katika malipo mbele ya Mola wako na yana mwisho



mwema.