Aya 73-76: Lipi Kati Ya Makundi Mawili
Na wanaposomewa Aya zetu zilizowazi, waliokufuru huwaambia walioamini: lipi katika makundi mawili lenye cheo kizuri na lililo bora barazani?
Aya za Mwenyezi Mungu zilizo wazi ni dalili, makundi mawili ni waumi- ni na washirikina. Maana ni kuwa Mtume na maswahaba wanawapa washirikina hoja ya mantiki, kiakili na kimaumbile na wao wanajibu kwa mantiki ya tumbo na falsafa yake.
Falsafa Ya Tumbo
Epikouros alikuwa ni mwanafalsafa wa kiyunani (ugiriki) katika wanafunzi wa Aristatle, alikuwa na madhehebu yake peke yake yaliyotofautiana na wenzake na pia wale waliomtangulia.
Kwa ufupi anasema ladha ndio kheri kuu na machungu ndio shari kuu na kwamba thamani ya fadhila inategemea ladha za kimaana; kama ukweli, maisha ya utulivu na raha na pia ladha za kihisia; kama chakula na kinywaji...
Katika mwongozo wa falsafa hii anasema: Mtu asisukumwe na hawa yake na upendeleo wake kwenye ladha fupi itakayofuatiwa na machungu marefu.
Kwa maneno mengine ni kuwa, kwake yeye Epikouros – akiwa haamini ufufuo- ni kwamba kheri yote inakuwa kwenye ladha ya kidunia; ni sawa iwe kwenye tumbo au kwengineko. Kama itakutana na machungu basi linalozingatiwa ni wingi, lile lenye ladha nyingi litakuwa ni kheri na lenye machungu mengi basi ni shari.
Kuna falsafa ya kale inayoaifikiana na Epikouros kwamba kheri yote iko kwenye ladha ya dunia. Yeye anasema kheri iko kwenye ladha ya kimaana na kihisia pamoja nayo anasema kheri iko kwenye ladha ya tumbo na mengineyo ya hisia.
Miongoni mwa wenye falsafa hii ni Firauni na washirikina wa kiquraysh. Firauni alipinga utume wa Musa (a.s.), akaleta sababu ya kupinga kwake kwa kusema:
“Aumimisiborakuliohuyualiyemnyongewalahawezikusemawazi. Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu...” (43: 52 – 53)
Akasema tena:
فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ {24}
Kisha akaendela:
أَلَيْسَ لِي مُلْكُ مِصْرَ وَهَٰذِهِ الْأَنْهَارُ تَجْرِي مِنْ تَحْتِي ۖ {51}
Makurishi nao, kama Firauni, walikanusha utume wa Muhmmad (s.a.w.) na wakatoa hoja kwa kusema:
لَوْلَا أُنْزِلَ عَلَيْهِ كَنْزٌ {12}
Falsafa hii haihusiki na Firauni na washirikina wa Makka tu, wala na watanuzi na wenye utajiri; isipokuwa inahusika na kila anayemuheshimu mtu na akampima kwa mali yake, basi yeye ni katika walioamini falsafa ya tumbo.
Miongoni mwa niliyoyasoma ni maneno ya kibaraka mmoja aliyesema: “Hawa wanaoilaumu Marekani na majeshi yake na wanavyowapiga wakombozi kila mahali na vile wanavyopora mali za wanyonge kila mahali, wamesahau au wanajitia kusahahu kuwa Marekani ina nguvu za kielimu na mali; na kwamba mwenye nguvu mpishe.”
Nilikuwa nikidhania kuwa falsafa ya tumbo ilikwisha kwenye zama za dhulma, lakini makala haya nilyoyasoma yamenifanya nitambue kuwa falsafa hii imekita mizizi kwenye nafsi za wapiga debe wa ukoloni na vibaraka wake.
Na karne ngapi tuliziangamiza zilizokuwa na mapambo mazuri zaidi na wazuri zaidi kwa mandhari?
Umetangulia mfano wake katika Juz.7 (6:6)
Sema: aliye katika upotofu basi Mwingi wa rehema atampa muda mpaka ayaone aliyoahidiwa – ama ni adhabu au ni saa. Hapo ndipo watajua ni nani mwenye makao mabaya na mwenye askari dhaifu.
Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake awaambie wale wanaoona kheri iko kwenye tumbo tu, kwamba hayo wanayojifaharisha nayo katika nafasi ya maisha waliyo nayo, kuwa ni mtihani wa Mwenyezi Mungu anowajaribu nao waja wake na anawapa muda mwingi.
Wakishukuru Mwenyezi Mungu atawapa thawabu na marejeo mazuri na wakizidi ukafiri na uasi basi atawasalitia ambaye atawatesa katika maisha haya ya duniani au atawaadhibu Mwenyezi Mungu huko Akhera. Huko watajua ni nani wenye hali mbaya, waumini walio mafukara au makafiri walio matajiri?
Lau mtu atamiliki kila kinacho chomozewa na jua, miliki hiyo si chochote kulinganisha na adhabu ya chini ya Jahannam. Amesema Amirul-mu’min, Aliy (a.s): “Heri siyo kheri ikiwa baada yake ni moto; na shari si shari ikiwa baada yake ni Pepo. Na kila neema isiyokuwa Pepo ni kazi bure na kila balaa isiyokuwa moto ni nafuu.”
Na Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu wale walioongoka
Hilo ni kwa kuwafahamisha hakika yao na sehemu za makosa na za sawa. Hii ni hidaya na neema kubwa.
Na mema yenye kubaki ni bora katika malipo mbele ya Mola wako na yana mwisho mwema.
Memayanayobakianielimunamamboyamanufaa.Hayomawilinibora kuliko mali na jaha. Kwa sababu yanadumu na kubakia manufaa yake na thawabu zake hazikatiki, lakini jaha na mali zinaisha na kuangamia.
أَفَرَأَيْتَ الَّذِي كَفَرَ بِآيَاتِنَا وَقَالَ لَأُوتَيَنَّ مَالًا وَوَلَدًا {77}
أَطَّلَعَ الْغَيْبَ أَمِ اتَّخَذَ عِنْدَ الرَّحْمَٰنِ عَهْدًا {78}
كَلَّا ۚ سَنَكْتُبُ مَا يَقُولُ وَنَمُدُّ لَهُ مِنَ الْعَذَابِ مَدًّا {79}
وَنَرِثُهُ مَا يَقُولُ وَيَأْتِينَا فَرْدًا {80}
وَاتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ آلِهَةً لِيَكُونُوا لَهُمْ عِزًّا {81}
كَلَّا ۚ سَيَكْفُرُونَ بِعِبَادَتِهِمْ وَيَكُونُونَ عَلَيْهِمْ ضِدًّا {82}
أَلَمْ تَرَ أَنَّا أَرْسَلْنَا الشَّيَاطِينَ عَلَى الْكَافِرِينَ تَؤُزُّهُمْ أَزًّا {83}
فَلَا تَعْجَلْ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّمَا نَعُدُّ لَهُمْ عَدًّا {84}
يَوْمَ نَحْشُرُ الْمُتَّقِينَ إِلَى الرَّحْمَٰنِ وَفْدًا {85}
وَنَسُوقُ الْمُجْرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرْدًا {86}
لَا يَمْلِكُونَ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَنِ اتَّخَذَ عِنْدَ الرَّحْمَٰنِ عَهْدًا {87}