read

Aya 88 – 98: Wanasema Mwingi Wa Rehema Amejifanyia Mwana

Maana

Na wao wanasema Mwingi wa rehema ana mwana. Hakika mmeleta jambo la kuchusha. Zinakurubia mbingu kutatuka kwa hilo na ardhi kupasuka na milima kuanguka vipande vipande kwa kudai kwao kuwa Mwingi wa rehema ana mwana.

Mwenyezi Mungu amewakemea sana wale waliomfanya Mwenyezi Mungu kuwa ana watoto wa kiume na mabinti na akawapa kiaga kwenye Aya kadhaa; miongoni mwazo ni: Juz.1 (2:116), Juz.5 (4:48), Juz. 6 (4:171) na Juz. 7 (6:101).

Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akataja hapa kauli yao hii kwa mfumo huu wa kutisha. Nao unafahamisha kuwa mtu anamchezea ambaye hachezewi na yeyote aliye mbinguni wala ardhini.

Binadamu anamchezea Muumba wake naye anaishi kwenye himaya yake, na anamnasibisha mambo ambayo kuyasikia tu yanaweza yakaipasua mbingu na ardhi na kuangusha milima.

Unaweza kuuliza, kwanini hasira yote hii ya kilimwengu kwa sababu tu ya maneno ya kijinga na ya udhaifu wa akili?

Jibu: Hasira yote hii, haiko kwa mtu au kikundi cha watu maalum; isipokuwa imetokana na shirki hii ambayo sasa imekuwa ni dini na itikadi wanayoifuata mamilioni, kizazi baada ya kizazi na mifano hii ya mungu mwan na mungu mama.

مَا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ ۗ {75}


“Masih



mwana



wa



Maryam



hakuwa



ila



ni



Mtume.


W


amepita



kabla



yake


Mitume.



Na



mama



yake



ni



mkweli.


W


ote



wawili



walikuwa



wakila



chaku- la”



Juz



6



(5:75).

Hahitajii Mwingi wa rehema kuwa na mwana.

Kwa sababu mwana anafanana na mzazi wake, na Mwenyezi Mungu hana aliyefanana naye. Na kwa sababu kuwa na mtoto ni kumuhitajia, na Mwenyezi Mungu amejitosheleza na walimwengu wote

Hakuna yeyote aliyomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Mwingi wa rehema kuwa ni mtumwa.

Hakuna yeyote aliyeko chini au juu ila huwa ni mja wa Mwenyezi Mungu anayemilikiwa. Kimsingi ni kwamba mwenye kumilikiwa sio mtoto na mmliki sio baba.

Hakika amewadhibiti na amewahisabu sawa sawa na kila mmoja kati yao atamfikia siku ya Kiyama peke yake.

Waliodhibitiwa ni walio mbinguni na ardhini na atakyefikiwa ni Mwenyezi Mungu. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu hapotewi na kujua kitu chochote katika ardhi wala katika mbingu na kwamba kila mmoja atakwenda kwa Mwenyezi Mungu siku ya kiyama akiwa peke yake, hana wa kumnusuru wala kumsaidia au kujisaidia yeye mwenyewe kwa wingi au uchache, sikwambii tena kumsadia mwenginewe. Ambaye atamjia Mwenyezi Mungu katika hali kama hiyo, anawezaje kuwa mtoto wake?

Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi.

Mwenyezi Mungu (s.a.w.) anatia mapenzi katika nyoyo za waja wake kwa watu wenye imani na ikhlasi, si kwa chochote ila kwa kuthamini fadhila na hulka njema.

Muhammad binAhmadAlkalabiy, mwenye kitabu Attas-hil anasema: Inasemekana kuwa Aya hii ilishukwa kwa Aliy bin Abi Twalib. Sheikh Almaraghi, mmoja wapo wa masheikh wa Al-Azhar, anasema: ‘Ibin Mardaywyh na Dilamiy wamepokea kutoka kwa Baraa, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alimwambia Aliy: Sema ewe Mola wangu nijalie ahadi kwako na unijaalie mapenzi katika nyoyo za waumini’ ndipo ikashuka Aya hii”.

Wanaswara Na Bani Hashim

Amesema Abu Hayani Al-andalusi katika tafsir yake Albahrul-Muhit: “Aya hii ilishuka kwa Aliy bin Abi Twalib na amesema Muhammad Alhanafiya: huwezi kumpata mumin ila anampenda Aliy. Maajabu ni yale aliyotueleza Imam wa lugha Ridhad Din, Abu Abdillah Muhammad bin Aliy bin Yusuf Al-Answariy Ashatibiy kuhusu aliyosema, ibn Is-haq Mnaswara:

• Uday na Taym kwa ubaya kamwe sitothubutu kuwataja

• Lakini naona ni vibaya Ali kulaumiwa na waja

• Mimi ni mpenzi wa dhuriya ya Hashimu na wanawe pamoja

• Naswira watukufu kupambiya kwa nini imekuwa ni kioja

• Tawaambiya huku kiusiya moyo wangu umekwisha wachuja

• Kupenda nifuraha nawambiya hata wanyama pia wangoja.

Hakika tumeifanya nyepesi, kwa ulimi wako ili uwabashirie kwayo wenye takua na uwaonye kwayo wabishi.

Yaani Mwenyezi Mungu ameteremsha Qur’an kwa lugha ya kiarabu ili iwe wepesi kuijua na kufahamu maana yake na iwe ni habari njema kwa mwenye kumcha Mwenyezi Mungu na onyo kwa mwenye kukufuru na akafanya uovu. Umepita mfano wake katika Juz. 12 (12:2)

Na karne ngapi tumeziangamiza kabla yao. Je, unawaona hata mmoja katika wao au unasikia hata mchakato wao?

Yaani Mwenyezi Mungu amewaangamiza mpaka wa mwisho wao. Umetangulia mfano wake katika Aya ya 84 ya sura hii. na Juz. 15 (17:17)