read

Aya 9-16: Hadithi Ya Musa

Kukaririka Kisa

Mwenyezi Mungu amekitaja kisa cha Musa, katika Kitabu chake, mara nyingi. Siri - kama tulivyogundua tukifasiri Aya za Dhikr Tukufu – ni kwamba Mwenyezi Mungu ametaja maovu mengi ya Wana wa Israil na Musa akiwakataza na kuwahadharisha, ndio ikawa kutajwa kwao ndio kutajwa kwake. Hii ni kuongezea kisa chake na Shuaib na Firauni, kusuhubiana kwake na mja mwema ambaye aliitoboa safina, kumuua kijana na kujenga ukuta. Vilelele kuzaliwa kwake na kuwekwa kwenye kisanduku katika maji hadi kumua kwake Firaun nk.

Badhi ya wafasiri wamesema: “Mwenyezi Mungu alikariri kisa cha Musa pamoja na Firauni, kwa sababu hikaya ya Musa tangu kuanza kutungwa mimba yake mpaka mwisho wa uhai wake, ni somo, nasaha, onyo, bishara na maliwazo kwa Mtume na waumini.

Ndani yake mna ishara zinazofahamisha elimu ya Mwenyezi Mungu, uweza wake, hekima yake na jinsi Musa alivyowachukua watu wake waliokuwa wapumbavu kuliko watu wote.”

Hii ndio dunia ya Musa: wakati wa kuzaliwa kwake aliwekwa kwenye kisanduku na akatupwa majini, akalelewa yatima katika nyumba ya Firaun, akafukuzwa akawa hana kitu akila mimea ya ardhi, akawa mchungaji kon- doo kisha akawa mtume akipata ugumu kutoka kwa watu wake.

Kwa hiyo si nyongeza kisa chake kikikaririka kutajwa na kuzungumziwa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, maadamu maisha yake yote na kisa chake ni somo na mawaidha. Aya hizi tulizo nazo hivi sasa zinazungumzia kuanza kushuka wahyi kwa Musa nakuzungumzanaMwenyeeziMungu.

Je imekujia hadith ya Musa?

Huu ni mfano wa kusema: ‘unayo habari?’ au ‘una habari gani?’ Makusudio ni kutanabahi msikilizaji asikilize vizuri simulizi. Na hii ifuatayo ndio hadith ya kuanza wahyi kwa Musa pale alipoona moto, akawaambia watu wake: ngojeni! Mimi nimeona moto, huenda nikawaletea kijinga kutoka huko au nikapata uongofu.

Katika Aya 14 na zilizo baada yake Mwenyezi Mungu amekieleza kisa cha Musa. Anaelezea kwamba Musa alipofikia umri wa kukomaa aliwaona watu wawili wakipigana, mmoja ni wa upande wa Firaun na mwingine upande wa mayahudi. Huyu wa upande wa mayahaudi alitaka msaada kwa Musa. Musa akampiga ngumi ikamuua.

Musa akakimbia kutoka Misr kwenda Madyan ambako Shuayb alimuoza mmoja wa mabinti zake kwa kuchunga wanyama wake kwa muda wa miaka minane au miaka kumi:

فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى الْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِ آنَسَ مِنْ جَانِبِ الطُّورِ نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَعَلِّي آتِيكُمْ مِنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِنَ النَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ {29}


“Basi alipotimiza muda wake na akasafiri na ahali zake, aliona moto upande



wa



Mlima



T


u


r


. Akwaambia



ahali



zake:



ngojeni!



Mimi



nimeona moto,



labda



nitawaletea



kutoka



habari



au



kijinga



cha



moto



ili



mpate



kuota” (28:29)

Musa alitokea Madyan kuelekea Misr akiwa na mkewe. Njiani alihitajia moto. Wapokezi wanasema: Musa alipotea njia katika usiku wa kusi kukiwa na baridi na giza. Mkono ukashindwa kupekecha moto na huku mkewe akiwa na uchungu wa kuzaa.

Wakati akiwa amedangana hana la kufanya mara akaona moto kwa mbali, akafurahi na akawaambia watu wake, huenda faraja inakuja katikati ya dhiki, kaeni niende kwenye moto nitawaletea moto muote au nipate habari za faraja.

Basi alipoufikia akaitwa: Ewe Musa! Hakika Mimi ndiye Mola wako Musa (a.s.) alikurubia kile alichofikiria kuwa ni moto; mara ukawa ni nuru adhimu inayoangaza zaidi ya jua; huku sauti ya kuogofya ikisema:
Hakika mimi ndiye Mola wako, basi vua viatu vyako kwa adabu na kun- yenyekea. Kwani hakika wewe uko katika bonde takatifu la Tuwa, mahali palipotwahara palipobarikiwa, ilipojionyesha nuru ya Mungu na katika anga yake ikainuka sauti ya utukufu na ukamilifu.

Musa aliona nuru na akasikia sauti; hakuna kitu kingine zaidi ya hivyo. Imam Aliy (a.s.) anasema:
“Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) haidirikiwi na hisia wala kukisiwa na watu…ambaye alizungumza na Musa na akamuonyesha ishara zake tukufu bila ya viungo wala zana yoyote.

Nami nimekuteua, basi sikiliza unayopewa wahyi.

Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hawateui kwa wahyi wake isipokuwa wale wasafi walio na uaminifu nao. Umetangulia mfano wake katika Juz. 9 (7:144). Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akabainisha kuwa dini aliyompia wahyi Musa inasimamia kwenye misingi mitatu:

Umoja wa Mungu: Hakika mimi ndiye Mwenyezi Mungu, hapana Mungu isipokuwa mimi.
Ikhalsi ya Mungu katika ibada: Basi niabudu mimi na usimamishe swala kwa ajili ya kunikumbuka Ufufuo: Hakika saa (kiyama) itakuja, nimekaribia kuificha, ili kila nafsi ilipwe kwa iliyoyafanya.

Makusudio ya kukurubia kuificha ni kuificha. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameficha kujulikana saa ya kiyama kwa waja wake, ili watarajie kufika kwake wakati wowote, waweze kuwa na hofu nayo na waifanyie kazi, kisha walipwe malipo yao bila ya kudhulumiwa kitu.

Kwa hiyo asikukengeushe nayo yule asiyeiamni na akafuata hawa yake ukaangamia.

Dhamiri ya ‘nayo’ inarudia kwenye hiyo saa, sio swala, kwa sababu ndiyo iliyo karibu na jumla hiyo. Inawezekana kurudia kwenye zote mbili. Maana ni kuwa ewe Musa, shikilia kuamini ufufuo, hisabu na malipo na uyayafanyie kazi wala usifuate hawaa za wapinzani usije ukaangamia kama watavyoangamia wao. Tumeshawahi kudokeza kuwa inafaa kwa mkuu kumkataza aliye chini yake, hata kama ni maasumu; kuongezea kuwa kukataza kitu hakufahamishi kuwa kuna uwezekanao wa aliyekatazwa kukifanya.

وَمَا تِلْكَ بِيَمِينِكَ يَا مُوسَىٰ {17}


N


a


nin


i


hich


o


kilicho


mkononi mwako wa kuume ewe



Musa?

قَالَ هِيَ عَصَايَ أَتَوَكَّأُ عَلَيْهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِي وَلِيَ فِيهَا مَآرِبُ أُخْرَىٰ {18}


Akasema: Hii ni fimbo yangu; ninaiegemea na ninawaangushia majani mbuzi na kondoo wangu; tena inanifaa kwa matumizi mengine.

قَالَ أَلْقِهَا يَا مُوسَىٰ {19}


Akasema:



itupe



ewe



Musa!

فَأَلْقَاهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٌ تَسْعَىٰ {20}


Akaitupa



mara



ikawa



nyoka anayekwenda



mbio.

قَالَ خُذْهَا وَلَا تَخَفْ ۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا الْأُولَىٰ {21}


Akasema: ichukue



wala



usihofu!


T


utairudisha



hali



yake ya



kwanza

وَاضْمُمْ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ آيَةً أُخْرَىٰ {22}

Na uambatanishe mkono wako na ubavu wako, utatoka mweupe pasipokuwa na ubaya wowote. Hiyo ni ishara nyingine.

لِنُرِيَكَ مِنْ آيَاتِنَا الْكُبْرَى {23}


Ili



tukuonyeshe



baadhi



ya ishara



zetu



kubwa.

اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ {24}

Nenda kwa Firauni; kwani hakika yeye amepetuka mpaka.

قَالَ رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي {25}


Aksema:



Ewe



Mola



wangu! Nikunjulie



kifua



changu

وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي {26}


Na



unifanyie



wepesi



jambo langu.

وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِنْ لِسَانِي {27}


Na ulifungue fundo lilo katika



ulimi



wangu.

يَفْقَهُوا قَوْلِي {28}


W


apate



kufahamu



kauli yangu.

وَاجْعَلْ لِي وَزِيرًا مِنْ أَهْلِي {29}

Na nipe waziri katika watu wangu

هَارُونَ أَخِي {30}


Harun



ndugu



yangu.

اشْدُدْ بِهِ أَزْرِي {31}

Niongeze nguvu zangu kwaye

وَأَشْرِكْهُ فِي أَمْرِي {32}


Na umshirikishe



katika jambo



langu.

كَيْ نُسَبِّحَكَ كَثِيرًا {33}

Ili tukutakase sana

وَنَذْكُرَكَ كَثِيرًا {34}


Na



tukukumbuke



sana

إِنَّكَ كُنْتَ بِنَا بَصِيرًا {35}


Hakika



wewe



unatuona.