read

Aya 17 – 35: Na Nini Hicho Kilicho Mkononi Mwako Wa Kuume Ewe Musa?

Na nini hicho kilicho mkononi mwako wa kuume ewe Musa?

MwenyeziMungu(s.w.t.)anamuulizaMusaamuelezekilichomkononi mwake, huku akiwa anajua zaidi kuliko huyo Musa mwenyewe. Kwa hiyo hapo kuna siri. Ndio kuna siri kubwa kwenye fimbo hii, aliyotaka kuidhi- hirisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa Musa, ambayo ni kugeuka fimbo kuwa nyoka.

Ikiwa tone la manii lina viini vya binadamu, yai lina viini vya kuku na mbengu kuwa na viini vya mimea, lakini mti huu mkavu hauna viini vyovyote vya nyoka, hata hivyo umegeuka nyoka! Hii ndio siri ya muujiza; na hapa ndio tunapata tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ {95}

“Humtoa aliye hai katika maiti” Juz. 7 (6:95)

Razi anasema: Anayetaka kutoa kitu kikuu kutokana na kidogo, kwanza hukionyesha hadharani kile kidogo huku akiseam: nini hiki? Nao waseme: ni kadha. Hapo ndio anaanza kazi yake. Ndio hivi alivyofanya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na Musa.

Alimuuliza kuhusu fimbo, alipokiri kuwa ni mti tu mkavu, Mwenyezi Mungu akaugeuza nyoka mkubwa, akaipigia bahari ikapasuka na jiwe likatoka chemchem.

Jambo la kushangaza ni kwamba Sheikh Maraghi alinukuu ibara hii ya Razi bila ya kuashiria chimbuko lake; kama ilivyo kawaida yake, katika tafsiri yake kuanzia mwanzo hadi kwenye Aya hii. Na ninadhani inayofu- atia pia ni hivi hivi; sawa na mpangilio wa Nidhamuddin Naysabury, katika tafsiri yake Gharaibulqur’an wa raghaibulfurqan.

Akasema: Hii ni fimbo yangu; ninaiegemea na ninawaangushia majani mbuzi na kondoo wangu; tena inanifaa kwa matumizi mengine.

Tumesoma elimu ya maani na bayan, katika kitabu Al-mutawwal cha Taftazaniy. Tulipofika kwenye mlango wa kufupisha, kurefusha na kulinganisha sawa, mwenye kitabu alitaja faida za kurefusha; zikiwa ni pamoja na: kufafanua, kusisitiza kwa kukaririka na ladha ya elimu. Kisha Ustadh akapiga mfano wa mazungumzo pamoja na mpendwa, kutokana na riwaya ya baadhi ya wategemezi.

Kwa ufupi ni kwmba mpokezi aliota ndoto ya kuonana na Muhammad (s.a.w.) na Musa bin Imran (a.s.). Akamsikia Musa akimlaumu Muhammad huku akimwambia: miongoni mwa mambo uliyasema ni: Ulama wa uma wangu ni kama manabii wa Bani Israil. Hii ndio hadhi yetu kwako ewe Abulqasim sawa na ulama wa uma wako?

Muhammad akataka kumthibitishia, akamwambia: hivi sasa nitakukutan- isha na mmoja wa ulama wa uma wangu ili umjaribu uone usahihi wa niliyoyasema. Musa akamwambia sawa. Akamkutanisha na mwanachuoni Ardabeliy. Musa akamuuliza: waitwaje? Akajibu: Mimi ni Ahmad na baba yangu jina lake ni Muhammad, ninatoka Ardabeliy, nimesoma Najaf na mwalimu wangu ni Shahiduthani.

Musa akamwambia: ni yanini yote hayo? Nimekuuliza jina lako tu, wewe waniambia jina lako, la baba yako, mji wako na mwalimu wako! Ardabeliy akamwambia: wewe si uliulizwa na Mwenyezi Mungu kuhusu kilicho mikononi mwako na ukasema:“Hii ni fimbo yangu; ninaiegemea na ninawaangushia majani mbuzi na kondoo wangu; tena inanifaa kwa matumizi mengine na ingetosha kusema hii ni fimbo yangu tu.”

Hapo Musa akamgeukia Muhammad na kumwambia huku akiomba msamaha: wewe unajua zaidi uliyoyasema.

Ustadh aliongezea riwaya hii kwa kusema: namna hii mtu hurefusha maneno pamoja na yule anayempenda si kwa lolote ila ni kwa kumfungulia moyo na bashasha. Miongoni mwa hayo ni kauli ya malenga mashuhuri anayeitwa Mutanabbi: Maswali mengi hutokana na shauku na mengi majibu ni kwa kutunuku

Akasema: itupe ewe Musa! Akiatupa mara ikawa nyoka anayekwenda mbio. Akasema: ichukue wala usihofu! Tutairudisha hali yake ya kwanza.

Musa alipatwa na hofu kutokana na mandhari haya yakutisha na akarudi nyuma; kama inavyofahamisha Aya isemayo:

فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَا مُوسَىٰ لَا تَخَفْ إِنِّي لَا يَخَافُ لَدَيَّ الْمُرْسَلُونَ {10}

“Alipoiona inayumba kama nyoka akageuka kurudi nyuma wala hakungoja. Ewe Musa! Usikhofu hakika hawakhofu mbele yangu mitume” (27:10).

Yaani Mitume hawaogopi kwa yale ninayowaamrisha, kwa vile wanajua kuwa siwaamrishi isipokuwa kheri wala siwakatazi isipokuwa shari. Mara tu, Musa alipoweka mkono wake kwenye nyoka iligeuka fimbo.

Na uambatanishe mkono wako na ubavu wako, utatoka mweupe pasipokuwa na ubaya wowote. Hiyo ni ishara nyingine. Ili tukuonyeshe baadhi ya ishara zetu kubwa.

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Amesema uambatanishe mkono na ubavu wako. Na mahali pengine akasema:

وَأَدْخِلْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ {12}

“Na ingiza mkono wako kwenye uwazi wa vazi lako” (27:12).

Pasipokuwa na ubaya wowote ni kutokuwako madhara.

Mkono wa Musa ulikuwa wa rangi ya kahawiya, kwa sbabu yeye alikuwa wa rangi hiyo. Alipouingiza mkono wake na akautoa, ulitoa mwanga kama wa jua. Umetangulia mfano wa Aya hii katika Juz. 9 (7:108).
Nenda kwa Firauni; kwani hakika yeye amepetuka mpaka

Mwenyezi Mungu alimwamrisha Musa kumkemea Firauni na dhulma yake, akiwa ni mwenye nguvu na uwezo; kiasi cha kujigamba na kusema:

أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ {24}

“Mimi ndiye Mola wenu Mkuu” (79:24),

مَا عَلِمْتُ لَكُمْ مِنْ إِلَٰهٍ غَيْرِي {38}

“Simjui kwa ajili yenu Mungu asiyekuwa mimi” (28: 38) tena akmwambia Musa:

أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ {18}

“Je hatukukulea kwetu ukiwa mtoto na ukakaa kwetu miaka ya umri wako?” (26:18).

Musa alikulia katika kasri ya Firauni kama yatima; kisha akawa mkimbizi akila majani. Imam Aliy (a.s) anasema katika Nahjulbalagha: Rangi ya kijani ya majani ilikuwa ikionekana kwenye ngozi ya tumbo lake kwa wembamba wake na kutenga na nyama yake.

رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنْزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ {24}

“Mola wangu! Hakika mimi ni muhitaji wa kheri utakayonitermshia” (28:24).

Imam anasema: “Wallah hakumuomba isipokuwa mkate wa kula tu” na Mungu alimwitikia maombi yake, akapata mkate kwa Shuayb kwa kufanya kazi ya kuchunga wanyama wake.

Hii ndiyo dunia ya Musa bin Imran: Wakati wa kuzaliwa kwake aliwekwa kwenye sanduku, akatupwa majini. Akakulia kwenye nyumba ya Firauni akiwa yatima; akawa mkimbizi akila mimea ya ardhi, kisha akawa mchunga mbuzi na kondoo.

Mtu huyu oheahe asiye na chochote anaenda kumkabili kigogo mwenye kila kitu, itawezekana kweli? Ndio iliwezekana! Alikwenda Musa kwa Firauni na wakuu wake na fimbo yake ikameza vyote walivyovizua na mkono wake ulioonyesha ukweli wake na usafi wake. Mbali ya fimbo na mkono Musa aliomba mambo mengine zaidi, kama ifuatavyo:-

Ewe Mola wangu! Nikunjulie kifua changu.

Inajulikana kuwa Musa alikuwa ni mwepesi wa kukasirika kwa jambo linalomchukiza. Haya yametamkwa na Qur’an. Imeeleza kuwa alishika ndevu za nduguye Haruna na kichwa chake, pale wana wa Israil walipoabudu ndama. Akampiga ngumi mtu wa upande wa Firauni na kum- maliza na akahalifu amri ya mja mwema baada ya kumwambia kuwa nitavumilia.

Hakuna mwenye shaka kwamba matatizo aliyopamabana nayo Musa katika maisha yake yameacha athari ya hasira hizi za harakaharka. Kwa kuwa Utume unahitajia uvumilivu wa machukivu na tabu, ndio akamuomba Mola wake awe mpole na mkunjufu.

Na unifanyie wepesi jambo langu.

Yaani unisaidie, ewe Mola wangu, kwa masaada na tawfiki ya kuweza kutekekeleza yale uliyonikalifisha na unifanye niweze kuyabeba. Hakuna kitu cha kheri kinachotimia kwa mtu, isipokuwa kwa tawfiki na msaada wa Mwenyezi Mungu; hata akiwa na nyenzo zote.

Na ulifungue fundo lilo katika ulimi wangu. Wapate kufahamu kauli yangu

Aya hii tukiunganisha na ile isemayo:

وَأَخِي هَارُونُ هُوَ أَفْصَحُ مِنِّي لِسَانًا فَأَرْسِلْهُ {34}

“Na ndugu yangu Harun ni fasaha zaidi kuliko mimi kwa ulimi” (28:34).

Na pia:

وَلَا يَكَادُ يُبِينُ {52}

Wala hawezi kusema waziwazi” (43:52).

Tukiunganisha Aya zote hizi tatu, tunapata ushahidi wa yule asemaye kwamba Musa alikuwa na kigugumizi. Ama kuwa kigugumizi hiki ni cha maumbile au kilitokana na kaa la moto alilolitia mdomoni, pale alipojaribiwa na Firauni utotoni, ujuzi wake uko kwa Mola wangu.

Kwa hakika Aya hii inaonyesha kuwa ufasaha wa ulimi na kubainisha maneno ni katika sifa kuu na neeema kubwa ya Mwenyezi Mungu kwa mtu:

خَلَقَ الْإِنْسَانَ {3}

عَلَّمَهُ الْبَيَانَ {4}

“Amemuumba mtu akamfundisha kusema” (55:3-4).

Imam Aliy (a.s.) anasema: “Mtu si mtu lau si ulimi (kuzungumza); isipokuwa mnyama mwenye kupuuzwa au picha”

Na nipe waziri katika watu wangu, Harun ndugu yangu, niongeze nguvu zangu kwaye na umshirikishe katika jambo langu, ili tukutakase sana na tukukumbuke sana. Hakika wewe unatuona.

Katika Majmaul-bayan imeelezwa kuwa Harun alikuwa ni nduguye Musa kwa baba na mama, na alikuwa ni mkubwa wake kwa miaka mitatu. Alikuwa mwenye kimo, mwenye mwili mwangavu, mwenye nyama nyingi na mfasaha wa kuzungumza. Ni kutokana na sifa hizi ndio Musa akamuomba Mola wake amfanye nduguye Harun ni mshirika wake katika utume. Mwenye Majmaul-bayan anasema kuwa alikufa kabla ya kufa nduguye Musa kwa miaka mitatu.

Hakika Ya Utume

Kwa vyovyote ilivyo ni kuwa mwenye ujumbe hana budi kuwa na mwen- za msaidizi mwenye ikhlasi na atakayejitolea muhanga. Kwani unabii, katika hakika yake, ni habari inayotoka kwa Mungu anayoinukuu mtu; sio nguvu tekelezi au kusema ‘kuwa’ na ikawa.

Nabii ni mtu asiyeweza kujizuia na madhara wala kujiletea manufaa. Utekelezaji wake unatumia nyenzo zilezile anazozitumia mumin na asiyekuwa mumin.

Hakuna tofauti isipokuwa ni habari za kutoka kwa Mungu na kwamba Mwenyezi Mungu anamchukua mtu aliye mtukufu zaidi na kumteua mwenye sifa nzuri zaidi. Lakini sifa takatifu hazifanyi mwenye nazo asiwe na haja na desturi ya maumbile. Hapana! Manabii na wasiokuwa manabii, wote wanahitaji nyenzo.

Nabii anahitajia tabibu akiwa mgonjwa; sawa na asiyeamini Mungu na siku ya mwisho anavyohitajia. Vile vile anahitaji nguvu; kama anavyohitajia mtu mwingine. Mitume wote waliudhiwa na wengi wao wakuawa.

Hapa inatubainikia kujiingiza sana hadi kupotea kwa yule anayesema kuwa Muhammad (s.a.w.) ndiyo hakika ambayo Mwenyezi Mungu ameiumbia viumbe na ni roho ambayo imeenea kwenye viumbe vyote vya juu na vya chini:

وَلَوْ كُنْتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ {188}

“Na lau kama ningelijua ghaibu ningelijizidishia kheri nyingi, wala isingelinigusa dhara. Mimi si chochote ila ni mwonyaji na mtoaji bishara kwa watu wanaoamini.” Juz. 9 (7:188)

Hii ndio hakika ya utume: kuonya na kuleta bishara. Anapopatikana muonyaji na mbashiri akiwa pamoja na msaidizi, basi kuongoza kutakuwa na nguvu ya hoja. Ni kwa ajili hii ndio maana Musa akamuomba Mola wake ampe nguuvu kwa ndugu yake.

KwamnasabahuuitakuwanivizuritutajealiyoyasemaW.L.Dewarnet kuhusu Muhammad katika ensaiklopidia yake ya Historia ‘Kisa cha maendeleo katika ulimwengu:’ “Maskani zote alizowahi kuishi Muhammad zilikuwa na upana usiozidi hatua 12 na kwenda juu hatua zisizozidi 8. Dari yake ilikuwa ya miti ya mitende, milango yake ikitokana na manyoya ya mbuzi au ya ngamia. Tandiko lake lilitandikwa ardhini na mto wake ulikwa wa ndifu.

Alikuwa akirekebisha mwenyewe viatu vyake na nguo zake, akiwasha moto, kufagia nyumba, kukama maziwa ya mbuzi, kununua chakula chake sokoni na akila kwa mkono na kuramba vidole vyake. Chakula chake kikuu kilikuwa ni tende na mkate wa shairi. Maziwa na asali ndio ilikuwa anasa yake baadhi ya wakati”

Aliy Na Harun

Hivyohivyo ilimtokea Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.). Suyuti, katika Durrilmanthur anasema wakati wa kufasiri: ‘Ewe Mola wangu! Nikunjulie kifua changu ‘ “Ametoa Hadith Ibn Mardawyh, Khatib na Ibn Asakir kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alisema:

Ewe Mola wangu! Hakika mimi ninakuomba aliyokuomba ndugu yangu Musa kuwa unikunjulie kifua changu, ufanye wepesi jambo langu na unifungue fundo lilo katika ulimi wangu na nipe waziri katika watu wangu, Aliy ndugu yangu, niongeze nguvu zangu kwaye na umshirikishe katika kazi yangu, ili tukutakase sana na tukukumbuke sana. Hakika wewe unatuona.

Amesema Muslim katika Sahihi yake Juz. 2 uk. 108, chapa ya 1348 AH: Hakika Mtume alimwambia Aliy: Je, huridhii kuwa wewe kwangu uko katika daraja ya Harun na Musa? Katika Juz. 1 ya Musnad Ahmad bin Hambal: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliwaita Hassan wawili (Hassan na Hussein) kwa kumfuata Harun katika kuwaita wanawe Shubbar na Shabir, yenye maana ya Hassan na Hussein.

قَالَ قَدْ أُوتِيتَ سُؤْلَكَ يَا مُوسَىٰ {36}

Akasema: Hakika umepewa maombi yako ewe Musa

وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَيْكَ مَرَّةً أُخْرَىٰ {37}

Na hakika tulikwisha kuneemesha mara nyingine

إِذْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّكَ مَا يُوحَىٰ {38}

Pale tulipompa wahyi mama yako yale yaliyotolewa wahyi

أَنِ اقْذِفِيهِ فِي التَّابُوتِ فَاقْذِفِيهِ فِي الْيَمِّ فَلْيُلْقِهِ الْيَمُّ بِالسَّاحِلِ يَأْخُذْهُ عَدُوٌّ لِي وَعَدُوٌّ لَهُ ۚ وَأَلْقَيْتُ عَلَيْكَ مَحَبَّةً مِنِّي وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي {39}

Kwamba mtie katika kisanduku kisha kitupe mtoni na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu na adui yake. Na nimekutilia mapenzi kutoka kwangu na ili ulelewe machoni mwangu

إِذْ تَمْشِي أُخْتُكَ فَتَقُولُ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ مَنْ يَكْفُلُهُ ۖ فَرَجَعْنَاكَ إِلَىٰ أُمِّكَ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ ۚ وَقَتَلْتَ نَفْسًا فَنَجَّيْنَاكَ مِنَ الْغَمِّ وَفَتَنَّاكَ فُتُونًا ۚ فَلَبِثْتَ سِنِينَ فِي أَهْلِ مَدْيَنَ ثُمَّ جِئْتَ عَلَىٰ قَدَرٍ يَا مُوسَىٰ {40}

Dada yako alipokwenda na akasema: Je, niwajulishe mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurujesha kwa mama yako, ili macho yake yaburudike wala asihuzunike. Na ulimuua mtu nasi tukakuokoa katika dhiki. Na tukakujaribu kwa majaribio. Ukakaa miaka kwa watu Madyana. Kisha ukaja kama ilivyokadiriwa ewe Musa

وَاصْطَنَعْتُكَ لِنَفْسِي {41}

Na nimekuchagua kwa ajili yangu.