Aya 36 – 41: Umepewa Maombi Yako Ewe Musa
Maana
Akasema: Hakika umepewa maombi yako ewe Musa, ya kukunjuliwa kifua, kufanyiwa wepesi kazi, kufunguka ulimi, kuongezewa nguvu kwa nduguyo na kushirikishwa kwenye utume pamoja nawe. ImamAliy(a.s.)anasema:“Kuwakwenyelileusilolitarajikuwaunalitarajia zaidi kuliko lile unalolitaraji. Kwani Musa Bin Imran alitoka akitafuta moto, akazungumza na Mwenyezi Mungu akarejea akiwa ni Mtume”
Na hakika tulikwisha kuneemesha mara nyingine.
Neema za Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa Musa zilkuwa nyingi; miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:-
Pale tulipompa wahyi mama yako yale yaliyotolewa wahyi. Kwamba mtie katika kisanduku kisha kitupe mtoni na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu na adui yake. Na nimekutilia mapenzi kutoka kwangu na ili ulelewe machoni mwangu
Makusudio ya wahyi hapa ni ilham – msukumo wa kufanya jambo. Macho ya Mwenyezi Mungu ni ulinzi wake.
Firauni alikuwa akimchinja kila anayezaliwa wa kiume katika waisrail na akizaliwa wa kike humfanya mjakazi. Mke wa Imran alipomzaa Musa alihofia Firauni, ndipo Mwenyezi Mungu akampa ilhamu ya kumweka kwenye sanduku kisha alitupe kwenye mto Nile, naye akafanya. Mungu akampa uthabiti wa moyo. Mto Nile ukalibebea sanduku hadi ufukweni. Inasemekana kuwa wajakazi wa Asiya, Mke wa Firaun, walitoka kwenda kuoga, wakakuta sanduku, wakalichukua. Mara tu mke wa Firauni alipolifungua na kuona mtoto, Mungu alimtia mahaba katika moyo wake:
وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِي وَلَكَ ۖ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰ أَنْ يَنْفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا {9}
Kwa hiyo Faruni akambakisha na akalelewa katika kasri yake akilindwa na Mwenyezi Mungu.
Dada yako alipokwenda na akasema: Je, niwajulishe mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurujesha kwa mama yako, ili macho yake yaburudike wala asihuzunike.
Mwenyezi Mungu alitaka Musa arejee kwa mama yake, ili asiwe mbali naye na asiwe na wasiwasi. Mungu akitaka jambo, huliandalia sababu zake. Alizuwiya matiti yote yasiweze kumnyonyesha Musa, kiasi ambacho Firauni alihangaika.
Akaenda dada yake kwenye kasri ya Firauni na kusema mimi nitawafahamisha atakayemnyonyesha. Ndio akaenda na mama yake akakubali matiti yake, Firauni akamkabidhi na akampa ujira wake.
Na ulimuua mtu nasi tukakuokoa katika dhiki
Siku moja Musa alikuwa akipita njiani, akawaona watu wawili wakipigana; mmoja ni wa upande wa Firaun na mmoja ni wa upande wake. Huyu wa upande wake akataka usaidizi kwa Musa. Akampiga ngumi yule mpin- zani, bila ya kukusudia kumuua, lakini akamuua. Musa akahofia kulipiziwa kisasi; Mwenyezi Mungu akamuondolea dhiki hiyo ya kisasi.
Haya yameashiriwa na Aya isemayo:
فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَٰذَا مِنْ شِيعَتِهِ وَهَٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ ۖ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِنْ شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ ۖ {15}
Na tukakujaribu kwa majaribio.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) humjaribu mja wake kwa furaha na dhiki. Mwenye kushukuru hayo na akavumilia haya, humkurubisha na kumpa thawabu. Na ambaye hazijali neema na akakufuru wakati wa shida, Mwenyezi Mungu humweka mabali na rehema yake. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Alimjaribu Musa kwa aina nyingi ya shida na misukosuko, akampata ni mwenye kuvumilia na mwenye kumkumbuka Mungu, ndipo Mwenyezi Mungu akamtukuza kwa utume na kamuinua daraja ya juu.
Ukakaa miaka kwa watu Madyana
Hapo ni baada ya kuchunga wanyama wa Shuayb, kama ilivyoashiria kauli yake Mwenyezi Mungu:
فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِنْدِكَ ۖ {27}
Na aliitimiza kumi, kama inavyoelezwa katika baadhi ya riwaya.
Kisha ukaja kama ilivyokadiriwa ewe Musa
Umekuja mahali hapa, kwenye jangwa takatifu la Tuwa; umekuja wakati ule alioukadiria Mwenyezi Mungu kukutuma wewe kwa utume.
Na nimekuchagua kwa ajili yangu.
Yaani nimekuchagua kwa ajili ya wahyi wangu na risala yangu. Kutegemezwa Musa kwa Mwenyezi Mungu ni ukomo wa utukufu na hes- hima; ambapo inaashiria kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemjalia ni katika watu wake mahususi.
اذْهَبْ أَنْتَ وَأَخُوكَ بِآيَاتِي وَلَا تَنِيَا فِي ذِكْرِي {42}
اذْهَبَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ {43}
فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَيِّنًا لَعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ {44}
قَالَا رَبَّنَا إِنَّنَا نَخَافُ أَنْ يَفْرُطَ عَلَيْنَا أَوْ أَنْ يَطْغَىٰ {45}
قَالَ لَا تَخَافَا ۖ إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ {46}
فَأْتِيَاهُ فَقُولَا إِنَّا رَسُولَا رَبِّكَ فَأَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَا تُعَذِّبْهُمْ ۖ قَدْ جِئْنَاكَ بِآيَةٍ مِنْ رَبِّكَ ۖ وَالسَّلَامُ عَلَىٰ مَنِ اتَّبَعَ الْهُدَىٰ {47}
إِنَّا قَدْ أُوحِيَ إِلَيْنَا أَنَّ الْعَذَابَ عَلَىٰ مَنْ كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ {48}