Aya 42-48: Nenda Wewe Na Nduguyo
Maana
Nenda wewe na nduguyo pamoja na ishara zangu, wala msichoke kunikumbuka.
Makusudio ya ishara hapa ni miujiza, amabayo ni fimbo, mkono mweupe na miujiza mingineyo, tuliyoiashiria katika Juz. 15 (17:101). Maana ya msichoke kunikumbuka ni msipuuze risala yangu na kukumbusha amri yangu na makatazo yangu.
Nendeni kwa Firauni, hakika yeye amepituka mipaka.
Nendeni ni kusisitiza ile kauli ya ‘nenda wewe na nduguyo.’ Umetangulia mfano wa Aya hii katika Aya ya 23 ya sura hii tuliyo nayo.
Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.
Kama wenye mashirika ya ukandamizaji watazingatia na kuogopa, basi Firauni angelizingatia na kuogopa.
Aya hii inapangilia mfumo wa kutoa mwito wa dini ya Mwenyezi Mungu. Kwa usahihi zaidi; inapanga mfumo wa kukinaisha haki. Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُمْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ {125}
Mawaidha mazuri ni kujua mwenye hatia, makosa yake na mpotevu kujua ubaya wake na kujiona kuwa yuko mbali na haki na hali halisi ya mambo:
وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ {10}
Sharti la kwanza la mawaidha mazuri ni kutotaka lolote anayetoa mwaid- ha, zaidi ya kutengeneza. Kwamba lengo la kwanza na la mwisho liwe ni kuongoza na kurekebisha.
Sharti la pili ni kuwa mawaidha kwa kauli laini. Miongoni mwa aliyoyasema Musa kwa Firauni ni: Je, unapenda kujitakasa? Nami nitakuongoza kwa Mola wako upate kumcha.(79:19).
Wakasema: Ewe Mola wetu! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri.
Ewe Mola wetu unajua ubabe wa Firauni na kwamba hakuna anayeweza kumzuia akiamrisha tuuawe kabla hata hajasikia dalili na hoja tutaka- zomwambia. Je unaweza kutuongeza kitu kitakachohakikisha usalama wetu?
Akasema: msiogope! Hakika mimi niko pamoja nanyi. Nasikia na ninaona.
Mimi ninadhamini usalama wenu. ‘Mwenyezi Mungu ni tosha wa kuhi- fadhi na kunusuru’ Unaweza kuuliza kuwa dhamiri ya wakasema: ni ya wawili, Musa na Harun, na inajulikana kuwa Harun hakuwa na Musa katika majibizano, sasa je, kuna wajihi gani wa hilo?
Baadhi ya wafasiri wamejibu kuwa kauli hii ilikuwa ni ya Musa kwa kusema na ya Harun kwa kihali. Kwa sababu Harun anamfuata Musa. Inawezekana kauli hii inatokana na wote wawili pamoja baada ya kuondoka Musa kwenda Misr na kuungana na nduguye, kabla hawajakwenda kwa Firani. Ni kawaida ya Qur’an kuacha maneno ambayo yatafahamika kutokana na mazingira au na maneno mengine.
Basi mwendeeni na mumwambie: hakika sisi ni wajumbe wa Mola wako, basi tuachie wana wa israil wala usiwaadhibu kwa kuwachukua mateka, kuwadhalilisha, kuwachinja watoto wao wa kiume na kuwatumia watoto wao wa kike. Umetangulia mfano wa Aya hii katika Juz.9 (7:104 –105).
Tumekuletea ishara itokayo kuwa Mola wako, kwa dalili za kutosha na hoja mkataa juu ya ukweli wetu.
Na amani itakuwa juu ya aliyefuata uongofu.
Uingofu ni dini ya Mwenyezi Mungu na amani ni kusalimika na adhabu yake. Yaani mwenye kuingia dini ya Mwenyezi Mungu amesalimika na adhabu ya kuungua.
Hakika tumepewa wahyi kwamba adhabu itampata anayekadhibisha na akapuuza.
Ni makemeo na maonyo kwa Firauni kuwa ataangamia na kubomoka kama atampuuz Musa na Harun kwa kuukana utume wao na kuenedelea kwenye upotevu wake na jeuri yake.
قَالَ فَمَنْ رَبُّكُمَا يَا مُوسَىٰ {49}
قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَىٰ كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَىٰ {50}
قَالَ فَمَا بَالُ الْقُرُونِ الْأُولَىٰ {51}
قَالَ عِلْمُهَا عِنْدَ رَبِّي فِي كِتَابٍ ۖ لَا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنْسَى {52}
الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَسَلَكَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا وَأَنْزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِنْ نَبَاتٍ شَتَّىٰ {53}
كُلُوا وَارْعَوْا أَنْعَامَكُمْ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِأُولِي النُّهَىٰ {54}
مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَىٰ {55}
وَلَقَدْ أَرَيْنَاهُ آيَاتِنَا كُلَّهَا فَكَذَّبَ وَأَبَىٰ {56}