Aya 77 – 82: Wapigie Njia
Maana
Na tulimpa wahyi Musa: Toka usiku na waja wangu na uwapigie njia kavu baharini, usikhofu kukamatwa wala usiogope.
Firauni aling’ang’ania inadi yake na akataa kila kitu isipokuwa kiburi na ujabari na kumpa sifa Musa kuwa ametoka nje na ni mchawi. Akapata wa kumuunga mkono katika hilo:
وَقَالَ الْمَلَأُ مِنْ قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُ لِيُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ{127}
Firauni alishikilia kutaka kumuua Musa, ndipo Mwenyezi Mungu akampa wahyi atoke Misr usiku pamoja na wana waisrail na apige bahari kwa fimbo yake ipasuke itokee njia waifuate waisrail hadi upande mwengine wasalimike na maangamizi na Firauni na shari yake:
فَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنِ اضْرِبْ بِعَصَاكَ الْبَحْرَ ۖ فَانْفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ {63}
وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ الْآخَرِينَ {64}
وَأَنْجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَنْ مَعَهُ أَجْمَعِينَ {65}
ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ {66}
Firauni akawafuata pamoja na majeshi yake. Basi kiliwafudikiza baharini kilichowafudikiza.
Kusema kiliwafudikiza kilichowafudikiza ni kulikuza jambo. Hapo kuna maneno mengi ya kukadiriwa; kama ilivyo kawaida ya Qur’an. Kwa sababu mfumo wa maneno unafahamisha hivyo.
Kukadirwa kwake ni: Musa alitoka na watu wake usiku. Alipofika baharini akapiga kwa fimbo yake na bahari ikapasuka kukawa na njia isiyokuwa na maji, wakaifuata waisrail. Firauni na jeshi lake wakawaandama. Walipofika waisrail upande wa pili na mjeshiya Firauni kuingia yote, bahari ilirudi wakafamaji wote na waisraili wakasalimika wote.
Na Firauni aliwapoteza watu wake na hakuwaongoza.
Aliwapoteza na haki na akawapoteza baharini vilevile. Hapo mwanzo alikuwa akiwaambia:
وَمَا أَهْدِيكُمْ إِلَّا سَبِيلَ الرَّشَادِ {29}
“Wala siwaongozi ila kwenye njia ya uongofu” (40:29)
Enyi wana wa israil! Hakika tuliwaokoa na adui yenu!
Firauni aliyekuwa akiwapa adhabu mbaya ya kuwachinja watoto wenu wa kiume na kuwaacha wanawake.
Na tukawaahidi upande wa kuume wa mlima.
Anaishiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ahadi aliyomwahidi Musa baada ya kufa maji Firauni. Ahadi yenyewe ni kwenda Musa upande wa mlimani, ateremshiwe Tawrat, amabayo ndani yake mna ubainifu wa sharia na hukumu.
Na tukawateremshia Manna na Salwa: Kuleni katika vizuri tulivyowaruzuku
Umetangulia mfano wake, kwa herufi zake, katika Juz. 1 (2:57)
Wala msipituke mipaka katika hayo isije ikawashukia ghadahabu yangu. Na inayemshukia ghadahabu yangu basi huyo amepotea.
Katika hayo ni hayo tuliyowaruzuku. Kupetuka mpaka katika hayo, ni kuchukua au kutoa kwa njia isiyokuwa yake ya kisharia.
Maana ni kuwa mwenye kuchuma mali kwa njia isiyokuwa ya halali au kuitumia kwa njia isiyokuwa ya halali, basi malipo yake mbele ya Mwenyezi Mungu ni maangamizi na adhabu ya kuunguza; sawa na Firauni na wengineo katika waasi walio mataghuti.
Hakika mimi ni mwingi wa maghufira kwa anayetubia na akaamini na akatenda mema tena akaongoka.
Mwenyezi Mungu husamehe madhambi kwa masharti mane:
1. Kwanza, kutubia nako ni kujuta kwa maasi yaliyokuwa pamoja na kuomba msamaha.
2. Pili, kuiamini haki, popote itakapokuwa na itakavyokuwa; ni sawa iafikiane na malengo yake au yahalifiane.
3. Tatu, kuitumia haki. Kwani imani bila ya matendo ni kama matamshi bila ya maana.
4. Nne, ni kuongoka. Makusudio yake ni kuendelea kuifuata haki mpaka kufa. Na hapa ndio tunapata jibu la mwenye kuuliza kuwa, kuna haja gani ya kuunganisha mwenye kuongoka na mwenye kuamini na akatenda mema.
وَمَا أَعْجَلَكَ عَنْ قَوْمِكَ يَا مُوسَىٰ {83}
قَالَ هُمْ أُولَاءِ عَلَىٰ أَثَرِي وَعَجِلْتُ إِلَيْكَ رَبِّ لِتَرْضَىٰ {84}
قَالَ فَإِنَّا قَدْ فَتَنَّا قَوْمَكَ مِنْ بَعْدِكَ وَأَضَلَّهُمُ السَّامِرِيُّ {85}
فَرَجَعَ مُوسَىٰ إِلَىٰ قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ أَلَمْ يَعِدْكُمْ رَبُّكُمْ وَعْدًا حَسَنًا ۚ أَفَطَالَ عَلَيْكُمُ الْعَهْدُ أَمْ أَرَدْتُمْ أَنْ يَحِلَّ عَلَيْكُمْ غَضَبٌ مِنْ رَبِّكُمْ فَأَخْلَفْتُمْ مَوْعِدِي {86}
قَالُوا مَا أَخْلَفْنَا مَوْعِدَكَ بِمَلْكِنَا وَلَٰكِنَّا حُمِّلْنَا أَوْزَارًا مِنْ زِينَةِ الْقَوْمِ فَقَذَفْنَاهَا فَكَذَٰلِكَ أَلْقَى السَّامِرِيُّ {87}
فَأَخْرَجَ لَهُمْ عِجْلًا جَسَدًا لَهُ خُوَارٌ فَقَالُوا هَٰذَا إِلَٰهُكُمْ وَإِلَٰهُ مُوسَىٰ فَنَسِيَ {88}
أَفَلَا يَرَوْنَ أَلَّا يَرْجِعُ إِلَيْهِمْ قَوْلًا وَلَا يَمْلِكُ لَهُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا {89}