read

Aya 83 – 89: Msamaria Na Ndama

Maana

Baada ya kuangamia Firauni na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kumwahidi Musa kuwa atamteremshia Tawrat na kumpa muda wake, Musa alikwenda kwa Mola wake kuichukua na kumwachia uongozi nduguye Haruna kwa Wana wa Israil. Hapo waliitumia fursa ya kuondoka Nabii wao Musa, wakaabudu ndama. Yakahakikika yale Aliokuwa wakiyawazia hapo mwanzo, pale walipowaona watu:

يَعْكُفُونَ عَلَىٰ أَصْنَامٍ لَهُمْ ۚ قَالُوا يَا مُوسَى اجْعَلْ لَنَا إِلَٰهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ ۚ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ {138}

“Waliokuwa wakiyaabudu masanamu yao; wakaema: “Ewe Musa! Hebu nasi tufanyie waungu kama hawa walivyo na waungu.” Akasema: “Hakika nyinyi ni watu wafanyao ujinga.” Juz.9 (7:138).

Yametangulia maelezo ya hayo katika Juz. 1 (2:51) na Juz 9 (7: 148). Aya hii tuliyo nayo na zinazofuatia hadi ya 98, zote zinazungumzia maudhui haya na yanayoambatana nayo.

Ni lipi lililokuharakisha ukaawaacha watu wako ewe Musa?

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamuuliza kuhusu haraka yake huku akijua sababu. Anataka kumfahamisha yaliyoowatokea watu wake - kuabudu ndama.

Akasema: Hao hapo nyuma yangu wananifuatia. Na nimefanya haraka kukujia, Mola wangu, ili uridhie.

Dhahiri ya maneno inafahamisha kuwa Musa alitakiwa aje na watu wake, lakini akaja peke yake, ndio akajibu kuwa wao wanakuja bila ya kuchelewa, nimewatangulia ili kukuridhisha. Alisema haya akiwa hajui waliyoyazua watu wake baada yake.

Akasema Mwenyezi Mungu: Hakika sisi tumewatia mtihani watu wako baada yako na msamaria amewapoteza.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewatia mtihani ili idhihirike hakika yao Waisrail. Namna ya mtihani ni kuwa Mwenyezi Mungu amewakataza kuabudu ndama kupitia kwenye ulimi wa Musa na shetani akawaamrisha kuabudu ndama kupitia ulimi wa Msamaria; wakamwasi Mungu na wakatii shetani. Ikadhihiri hakika yao ya udhaifu wa imani na ukafiri wao; sawa na afanyavyo muovu anapopata nafasi.

Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika.

Umetangulia mfano wake katika Juz. Juz.9 (7:150).

Akasema: Enyi watu wangu! Kwani Mola wenu hakuwaahidi ahadi nzuri?”

Anaashira kwa hili, kwamba Mwenyezi Mungu amewaahidi kuteremshiwa Tawrat kwa Mtume wao, ndani yake mna upambanuzi wa kila wanayoyahitajia katika kujua halali na haramu na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atawamilikisha makao ya wafasiki; kama ilivyoelezwa katika Juz. 9 (7:145):

وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ مَوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِكُلِّ شَيْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا ۚ سَأُرِيكُمْ دَارَ الْفَاسِقِينَ {145}

“Na tukamwandikia katika mbao kila kitu mawaidha na ufafanuzi wa kila jambo. Basi yashike kwa imara na uwaamrishe watu wako washike mazuri yake zaidi. Nitawaonyesha makao ya wafasiki.”

Je ahadi imerefuka?

Yaani muda wa kutokuwepo Musa umekuwa mrefu?

Au mmetaka iwafikie ghadhabu kutoka kwa Mola wenu

Yaani mimi sikuwa mbali nanyi kwa muda mrefu, kwa nini basi mkamshirikisha Mwenyezi Mungu? Au mlitaka iwafikie ghadhabu yake na adhabu yake?

Hii inaonyesha kuwa wao wanaamini maadamu Musa amewasimamia kwenye vichwa vyao, akiondoka wanageuka na kuipotoa dini kwa hawa zao, kama ilivyotokea.

Ndio maana mkavunja ahadi yangu.

Mmegeuka kwenye dini ya Mwenyezi Mungu baada ya kuniahidi kuwa mtakuwa thabiti.

Wakasema:Hatukuvunja ahadi yako kwa hiyari yetu.

Huku ni kukubali wazi kwamba wao walikufuru, kurtadi na kuvunja ahadi. Udhuru wao pekee ni kwamba wao ni kama wanoendeshwa hawawezi kujizuia na kufuru na hiyana; ni kama kwamba wao wametengenezwa hivyo. Hivi ndivyo inavyodhihiri hakika ya waisraili kwenye ndimi zao kuongezea vitendo vyao.

Lakini tulibebeshwa mizigo ya vipambo vya watu.

Vipambo vya watu ni vipambo vya wanawake wa watu wa Firauni. Wafasiri wamesema kuwa Waisraili walipojua kuwa wataipituka bahari na kwamba Mwenyezi Mungu atamwangamiza Firauni majini, waliwafanyia hila wanawake wa watu wa Firauni; wakawaazima vipambo vyao kwa kutoa visingizio vya harusi na mengineyo. Hili haliko mbali na tabia za kiisraili na hila zao za kuchuma mali kwa mbinu yoyote.

Basi tukaitupa na kadhalika Msamaria akatupa.

Tabari anasema katika Tafsiri yake: “Bani Israil walitupa vipambo walivyokuwa navyo ndani ya shimo, naye Msamaria akatupa alivyokuwa navyo. Vyote akavifua kwenye umbo la ndama.” akawaundia ndama, kiwiliwili chenye sauti.

UmepitamfanowakekatikaJuz.9(7:148).

Wakasema: “Huyu ndiye Mungu wenu na Mungu wa Musa, lakini amemsahau.”

Waliosema ni Msamaria na wenzake wakikusudia kuwa huyo ni Mungu wa wa viumbe vyote akiwemo Musa lakini amemsahu na kwenda kumtafua milimani, hajui kuwa ni mgeni wetu na tunaye majumbani mwetu.
Hii inaashiria kuwa kila anayesema kuwa Mungu ana kiwiliwili yuko pamoja na waabudu ndama atake asitake.

Je, hawakuona kuwa hakuwarudishia neno, wala hakuweza kuwad- huru wala kuwafaa.

Vipi atakuwa ndama ni Mola wao na wamemtengeneza kwa mikono yao? Hasikii maneno yao wala harudishi jawabu; hawawaletei manufaa wala hawazuii na madhara. Baadhi ya wafasiri wamesema: “Zaidi ya hayo hawezi kupiga pembe wala teke.”

Katika Tafsir Razi, imelezwa kuwa Myahudi mmoja alimwambia Imam Ali (a.s.): “Hamkuzika Mtume wenu mpaka mlipohitalifiana.”

Imam akasema: “Hatukuhitalifiana naye, bali tulihitalifiana kuhusiana naye, nanyi hata maji ya bahari hayajakauka miguuni mkaanza kumwambia Nabii wenu, tutengenezee mungu kama walivyo na mungu wao.”

Kama ingelifaa kufasiri Qur’an kwa rai na taawili ya hisia basi tungesema kuwa kutengeneza ndama kutokana na dhahabu na kumfanya ni mungu wao ni nembo ya kwamba wao tangu zamani wana maumbile ya kuabudu mali na kwamba hiyo ndio mungu wao wa pekee asiyekuwa na mshirika.

Historia yao ya zamani na ya sasa inafahamisha hilo waziwazi. Wao wanahalalisha kila kitu kwa ajili ya mali, hata kumwaga damu na umalaya.

وَلَقَدْ قَالَ لَهُمْ هَارُونُ مِنْ قَبْلُ يَا قَوْمِ إِنَّمَا فُتِنْتُمْ بِهِ ۖ وَإِنَّ رَبَّكُمُ الرَّحْمَٰنُ فَاتَّبِعُونِي وَأَطِيعُوا أَمْرِي {90}

Na hakika Harun alikwisha waambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihani tu kwa kitu hiki. Na kwa hakika Mola wenu ni Mwingi wa rehema. Basi nifuateni na mtii amri yangu.

قَالُوا لَنْ نَبْرَحَ عَلَيْهِ عَاكِفِينَ حَتَّىٰ يَرْجِعَ إِلَيْنَا مُوسَىٰ {91}

Wakasema: Hatutaacha kumwabudu mpaka Musa atakaporejea kwetu.

قَالَ يَا هَارُونُ مَا مَنَعَكَ إِذْ رَأَيْتَهُمْ ضَلُّوا {92}

Akasema (Musa): Ewe Harun! Ni nini kilichokuzuia ulipowaona wamepotea.

أَلَّا تَتَّبِعَنِ ۖ أَفَعَصَيْتَ أَمْرِي {93}

Hata usinifute? Je, umeasi amri yangu?

قَالَ يَا ابْنَ أُمَّ لَا تَأْخُذْ بِلِحْيَتِي وَلَا بِرَأْسِي ۖ إِنِّي خَشِيتُ أَنْ تَقُولَ فَرَّقْتَ بَيْنَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَمْ تَرْقُبْ قَوْلِي {94}

Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika niliogopa usije ukasema umewafarikisha Wana wa Israil na hukungojea kauli yangu.

قَالَ فَمَا خَطْبُكَ يَا سَامِرِيُّ {95}

Akasema: Una nini wewe Msamaria?

قَالَ بَصُرْتُ بِمَا لَمْ يَبْصُرُوا بِهِ فَقَبَضْتُ قَبْضَةً مِنْ أَثَرِ الرَّسُولِ فَنَبَذْتُهَا وَكَذَٰلِكَ سَوَّلَتْ لِي نَفْسِي {96}

Akasema: Nimeyaona wasiyoyaona wao na nikashika sehemu chache ya mwendo wa Mtume kisha nikaitupa, na hivyo ndivyo ilivyonielekeza nafsi yangu.

قَالَ فَاذْهَبْ فَإِنَّ لَكَ فِي الْحَيَاةِ أَنْ تَقُولَ لَا مِسَاسَ ۖ وَإِنَّ لَكَ مَوْعِدًا لَنْ تُخْلَفَهُ ۖ وَانْظُرْ إِلَىٰ إِلَٰهِكَ الَّذِي ظَلْتَ عَلَيْهِ عَاكِفًا ۖ لَنُحَرِّقَنَّهُ ثُمَّ لَنَنْسِفَنَّهُ فِي الْيَمِّ نَسْفًا {97}

Akasema (Musa): Basi ondoka na kwa hakika utakuwa katika maisha ukisema: ‘Usiniguse.’ Na hakika una miadi kwako isiyovunjwa. Na mtazame huyo mungu wako uliyeendelea kumwabudu; hakika tutamuunguza kisha tutamtawanya baharini atawanyike.

إِنَّمَا إِلَٰهُكُمُ اللَّهُ الَّذِي لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَسِعَ كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا {98}

Hakika Mungu wenu ni Mwenyezi Mungu tu, hapana mungu mwingine ispokuwa Yeye, ujuzi wake umeenea kila kitu.