Aya 90 – 98: Musa Amlaumu Harun
Maana
Na hakika Harun alikwisha waambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihani tu kwa kitu hiki. Na kwa hakika Mola wenu ni Mwingi wa rehema. Basi nifuateni na mtii amri yangu.
Musa alipokwenda mlimani, alimwambia ndugu yake Harun: “Shika mahali pangu katika watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya wafisadi.” Juz. 9 (7:142). Harun akatengeneza, kama alivyoamrishwa na ndugu yake; akatoa nasaha na kuwahadharisha wana wa Israil kutokana na Msamaria na ndama wake. Miongoni mwa maneno Aliowaambia ni: ‘Ni jambo gani lililowahadaa na ndama huyu mpaka mkashindwa na mtihani wake, mkamwelekea badala ya Muumba wa mbingu na ardhi? Basi nifu- ateni nitawaongoza njia ya uwongofu.’
Basi halikuwa jawabu la watu wake ispokuwa wakasema: Hatutaacha kumwabudu mpaka Musa atakaporejea kwetu, tuone rai yake kwenye hili. Kama kwamba wanamgonja amlaumu Harun kwenye hilo na awaunge mkono wao.
Kila mwenye kuathirika na mali kuliko dini yake na dhamiri yake, au akamfuata mpotezaji kwenye upotevu wake, basi yeye ni katika wafuasi wa Msamaria na chama chake. Mwenyezi Mungu amewatia mtihani waja wake kila wakati kwa ndama mwenye kutoa sauti Aliyetengenezwa kwa dhahabu au kuwa bendera inayofuta upepo.
Akasema (Musa): Ewe Harun! Ni nini kilichokuzuia ulipowaona wamepotea, hata usinifute? Je, umeasi amri yangu?
HiikwadhahiriinaonyeshanilawamakwaHarun,lakinikiuhakikani lawama na kuwatahariza wale walioabudu ndama. Kwa sababu Musa alijua fika kwamba ndugu yake Harun hakumukhalifu wala hatamkhalifu kwenye jambo lolote; na kwamba yeye alitekeleza wajibu wake kwa ukamilifu, kwa sabu yeye ni mshirika wake katika utume na kuwa ni maasumu.
Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 9 (7:150).
Kwa hakika niliogopa usije ukasema umewafarikisha Wana wa Israil na hukungojea kauli yangu.
Musa alimwambia Harun: “Kwa nini hukuwaacha wana wa Israil na kuun- gana nami ulipowaona wanakuasi wewe na kumfuata Msamaria?” Harun akamjibu: “Niliona nikiwaaacha itatokea fitna ya umwagikaji damu baina ya makundi mawili, lililo na imani na lile lilioritadi, hapo ndio utakuwa unaweza kunilaumu na ukaniambaia: umewaacha ili yatokee yaliotokea? Kwa ufupi ni kuwa aliyepo ndiye anayeona hali ilivyo.Musa akakinai na akasema:
“Mola wangu! Nisamehe mimi na ndugu yangu na utuingize katika rehe- ma yako na wewe ni mwenye kurehemu kushinda wote wenye kurehemu.” Juz. 9 (7:151).
Kisha akamwelekea Msamaria na akasema: Una nini wewe Msamaria?
Yaani,nijamboganilililokuachaukafanyauliyoyafanya?
Akasema:Nimeyaona wasiyoyaona wao na nikashika sehemu chache ya mwendo wa Mtume kisha nikaitupa, na hivyo ndivyo ilivyonielekeza nafsi yangu.
Imesemekana kuwa makusudio ya mtume hapa ni mjumbe Jibril; na sehe- mu chache ya mwendo ni mchanga alioukanyaga kwa unyayo wake au kwa kwato za farasi wake. Pia imesemekana kuwa makusudio ya mtume ni Musa na sehemu ya mwendo wake ni desturi yake.
Vile vile imesemekana kuwa Msamria ni muongo na kwamba yeye hakuona chochote katika sehemu ya mwendo wa Mtume; ispokuwa alitaka kujitoa kwa alioyafanya.
Kauli hii ina nguvu kuliko ile ya mguu wa Jibril au farasi wake. Mwenye kutengeneza ndama kwa mkono wake na akataka aabudiwe badala ya Mwenyezi Mungu kusema uongo na uzushi kwake ni jambo jepesi. Ama sauti inawezekana kutengenezwa kwa ndama kwa namna ambayo upepo ukiingia unatoa sauti; kama tulivyoeleza katika Juz. 9 (7: 148).
Vyovyote iwavyo, dhahiri ya maana inayofahamishwa na Qur’an ni kwamba Msamaria ndiye aliyefanya ufisadi, akawapoteza wana wa Israil katika kuabudu ndama. Ama jinsi alivyofanya, hatuna lazima nako kukujua wala hakuna uhusiano wowote na itikadi yetu na maisha yetu.
Akasema (Musa): Basi ondoka na kwa hakika utakuwa katika maisha ukisema: ‘Usiniguse.’
Haya ndiyo malipo yako duniani – kutengwa na watu wote, hutachanganyika na watu wala hakuna atakayetaka kuchanganyika na wewe kwa kauli wala vitendo. Ama adhabu yako huko Akhera, itakuwa chungu zaidi. Inasemekana kuwa Msamaria aliishi mwituni na wanyama.
Na hakika una miadi kwako isiyovunjwa.
Hakuna kukimbia wala kuihepa nayo ni kukutana na Mungu na kuhisabi- wa yale uliyoyazua na malipo yako ni adhabu na kuungua na moto.
Na mtazame huyo Mungu wako uliyeendelea kumwabudu; hakika tutamuunguza kisha tutamtawanya baharini atawanyike.
Huu ndio mwisho wa kila mzushi mwenye vitimbi, kuhizika na utwevu. Hakika Mungu wenu ni Mwenyezi Mungu tu, hapana mungu mwingine ispokuwa Yeye, ujuzi wake umeenea kila kitu.
Yeye peke yake ndiye Mungu wa haki, hakuna muabudiwa ispokuwa Yeye, rehema yake imeenea kwenye kila kitu; na hakuna kitu chochote ispokuwa kinamwabudu na kumsabihi kwa kusifu.
Waisrail Wanashangaza
Ni vizuri tumalizie Aya hii kwa yale yalioelezwa katika Tafsir ya Razi. Ninamnukuu: “Ameseam Abul-Qasim Al-Ansariy, amesema: “Wachawi walikuwa ni washirikina, lakini walipoona muujiza mmoja tu wa fimbo kugeuka nyoka, walimwamini Mwenyezi Mungu na Musa, wakavumilia adhabu kali kwa ajili ya imani yao hiyo, wala hawakurudi nyuma. Lakini Wana wa israil waliiona fimbo ilivyovunjilia mbali uchawi, wakawaona wachawi walivyokubali kushindwa; kisha wakaona miujiza mingine tisa, zaidi ya hayo wakaona bahari ilivyopasuka njia kumi na mbili. Pamoja na yote hayo, baada ya kutoka baharini na kuona watu wengine wakiabudu ng’ombe nao wakamwambia Musa tufanyie Mungu kama wao na waliposikia sauti ya ndama tu wakaanza kumwabudu.”
Wakati nikifasiri Aya zinazohusianan na wana wa israil, nimekuwa nikitamani sana, kuundwe kamati ya wataalamu wa maumbile ya binadamu wafanye utafiti juu ya waisral na tabia zao. Wachunguze historia yao na:
كَذَٰلِكَ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنْبَاءِ مَا قَدْ سَبَقَ ۚ وَقَدْ آتَيْنَاكَ مِنْ لَدُنَّا ذِكْرًا {99}
مَنْ أَعْرَضَ عَنْهُ فَإِنَّهُ يَحْمِلُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وِزْرًا {100}
خَالِدِينَ فِيهِ ۖ وَسَاءَ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حِمْلًا {101}
يَوْمَ يُنْفَخُ فِي الصُّورِ ۚ وَنَحْشُرُ الْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ زُرْقًا {102}
يَتَخَافَتُونَ بَيْنَهُمْ إِنْ لَبِثْتُمْ إِلَّا عَشْرًا {103}
نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ إِذْ يَقُولُ أَمْثَلُهُمْ طَرِيقَةً إِنْ لَبِثْتُمْ إِلَّا يَوْمًا {104}
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْجِبَالِ فَقُلْ يَنْسِفُهَا رَبِّي نَسْفًا {105}
فَيَذَرُهَا قَاعًا صَفْصَفًا {106}
لَا تَرَىٰ فِيهَا عِوَجًا وَلَا أَمْتًا {107}
يَوْمَئِذٍ يَتَّبِعُونَ الدَّاعِيَ لَا عِوَجَ لَهُ ۖ وَخَشَعَتِ الْأَصْوَاتُ لِلرَّحْمَٰنِ فَلَا تَسْمَعُ إِلَّا هَمْسًا {108}
يَوْمَئِذٍ لَا تَنْفَعُ الشَّفَاعَةُ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَٰنُ وَرَضِيَ لَهُ قَوْلًا {109}
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا {110}
وَعَنَتِ الْوُجُوهُ لِلْحَيِّ الْقَيُّومِ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنْ حَمَلَ ظُلْمًا {111}
وَمَنْ يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا يَخَافُ ظُلْمًا وَلَا هَضْمًا {112}