read

Aya 123 – 129: Akasema: Ondokeni Humu Nyote

Maana

Akasema: ‘Ondokeni humu nyote; hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukiwafikia uongofu kutoka kwangu, basi atakayefuata uon- gofu wangu, hatapotea wala hatataabika.’

Aliyesema ni Mwenyezi Mungu na wanaoambiwa watoke ni Adam na mkewe Hawa. Makusudio ya nyinyi kwa nyinyi ni kizazi cha Adam na Iblisi. Uongofu ni maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake.

Mwenye kumtii Mwenyezi Mungu katika amri yake na makatazo yake, basi yeye ni katika walioongokoka duniani na wenye kupata mema Akhera. Umetangulia mfano wa Aya hii katika Juz. 1 (2:36).

Na atakayejiepusha na mawaidha yangu, basi hakika atapata maisha yenye dhiki.
Unaweza kuuliza: dhahiri ya Aya inafahamisha kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amepitisha na amekadiria kuwa waasi walio mataghuti waishi katika maisha ya tabu na dhiki, lakini tuyaonayo ni kinyume na hivyo; kila wanavyozidi kuwa na uasi na utaghuti ndivyo wanavyozidi kuwa na jaha na mali?

Wafasiri wamejibu kuwa makusudio ya dhiki, hapa, ni jakamoyo walilon- alo na hadhari ya mwisho mbaya wa ghafla pamoja na tabu baada ya raha.

Lakini inavyoonekana ni kuwa hali hii anayo kila mwenye nacho; awe mtiifu au muasi. Kwa sababu tabia ya hali haipambanui baina ya mwema na muovu, majanga yake hayamuhurumii mdogo wala myonge, wala haijali mawalii au watu wema.

Jawabu lilo na nguvu zaidi ni yale tuliyoyataja katika Juz. 6 (5:64 – 66) kifungu cha ‘Riziki na ufisadi.’ Vile vile katika Juz. 7 (5: 100) kifungu cha ‘Je, riziki ni bahati au majaaliwa.’

Kwa ujumla ni kuwa ufukara unahukumiwa ardhini si mbinguni; ni katika mambo walioyafanya watu kwa mikono yao, wale ambao wameua haki na uadilifu. Lau wangeliisimamisha sharia ya Mungu, asingalipatikana ardhi- ni hata fukara mmoja.

Na tutamfufua siku ya Kiyama hali ya kuwa kipofu.

Baadhi ya wafasiri wanasema kuwa makusudio ya upofu hapa ni upofu wa hoja na dalili; wengine wakasema ni upofu wa Pepo. Lakini ilivyo hasa ni kuwa makusudio ni kwa maana yake yalio dhahiri, ya kutoona, bila ya kuweko haja ya taawili; kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Aseme: Ewe Mola wangu! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? Atasema: Ndivyo hivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahahu na kadhalika leo unasahauliwa.
Yaani, leo wewe unapuuzwa, kama ulivyopuuza hapo mwanzo. Kwa ufupi ni kuwa mwenye kuwa na matendo mabaya hapa duniani atakuwa na mwisho mbaya huko akhera.

Aya hii ni dalili iliyowazi zaidi kwamba matendo ya duniani ndio asili na malipo ya akhera ni tanzu, na kwamba hakuna njia nyingine ya kupata neema yake ispokuwa kwa amali njema.

Pamoja na kuwa Qur’an tukufu inaunganisha Uislamu na maisha na matendo na malipo, lakini vijana wetu wengi wanasema kuwa dini ni upotofu na vigano. Sababu yao katika hilo ni kutoujua Uislamu na kuwa mbali na maarifa ya uhakika wake na siri zake.

Na hivyo ndivyo tutakavyomlipa kila apitaye kiasi katika kuitafuta dunia na asiyeamini ishara za Mola wake zinazofahamisha kuweko kwake na utume wa mitume yake na kuteremshwa vitabu vyake. Au anayeamini yote hayo, lakini hafanyi kwa matendo.

Na Hakika adhabu ya Akhera, ikiwemo nguo za lami, chakula cha Zaqum, kinywaji cha moto na makomeo ya chuma, ni kali zaidi na inadumu, kuliko kutokea upofu na kusahau.

Je, haikuwabainikia, ni vizazi vingapi tuliviangamiza kabla yao nao wanatembea katika maskani zao.

Wanaambiwa washirikina kuwa vipi wanendelea na kung’ania ushirikina baada ya kupewa mwito wa tawhid na hali Mwenyezi Mungu amewabain- ishia njia za uongofu kwenye tawhid; zikiwemo kuangamizwa uma zilizopita; kama vile kaumu ya Nuh, A’d na Thamud waliokuwa na nguvu, mali na watu wengi.

Mwenyezi Mungu akawapelekea Mitume, watoa bishara na maonyo, kama alivyomtuma Muhammad kwa washirikina wa kikuraishi, wakaasi na Mwenyezi Mungu akawaangamiza kwa kufuru yao na uasi wao, wakiwa wametulia kwa amani. Je washirikiana wa kikuraishi wameaminisha kuji- wa na adhabu ya ghafla, kama ilivyowajia walikowa kabla yao?

Hakika katika hayo kuna ishara kwa kwa wenye akili, kwamba yaliowapitia waliopita ni mazingatio na mawaidha kwa watu wenye akili walioko sasa.

Na lau si neno la Mola wako lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako na muda uliotajwa, bila shaka ingelikuwa lazima, kuwafikia adhabu.

Makusudio ya neno na muda uliotajwa ni kupitisha kwake Mwenyezi Mungu. Yaani lau si kupitisha kwake na hekima yake Mwenyezi Mungu ya kuahirisha adhabu hadi muda uliowekwa kwa washirikina wa kikuraishi, basi bila shaka ingeliwafikia tu.

فَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا ۖ وَمِنْ آنَاءِ اللَّيْلِ فَسَبِّحْ وَأَطْرَافَ النَّهَارِ لَعَلَّكَ تَرْضَىٰ {130}

Fanya subra na wayasemayo. Na umsabihi Mola wako kwa kumsifu kabla ya mawiyo jua na kabla ya machweo yake. Na nyakati za usiku pia umsabihi, na ncha za mchana, ili uridhike.

وَلَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِنْهُمْ زَهْرَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا لِنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَرِزْقُ رَبِّكَ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ {131}

Wala usivikodolee macho tulivyowastarehesha aina ya watu miongoni mwao, kwa mapambo ya duniani ili tuwajaribu. Na riziki ya Mola wako ni bora na yenye kudumu zaidi.

وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا ۖ لَا نَسْأَلُكَ رِزْقًا ۖ نَحْنُ نَرْزُقُكَ ۗ وَالْعَاقِبَةُ لِلتَّقْوَىٰ {132}

Na uwaamrishe watu wako kuswali na uwe na subira nayo. Hatukuombi riziki. Sisi tunakuruzuku wewe. Na mwisho mwema ni kwa mwenye takua.