read

Aya 130-132: Fanya Subra Na Wayasemayo

Maana

Fanya subra na wayasemayo.

Washirikina walimkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), wakamwambia ni mchawi, mshairi, mzushi na hata mwenda wazimu; ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha awe na subira kwa sababu subira huvuta kheri.

Na umsabihi Mola wako kwa kumsifu.

Makusudio ya kumsabihi hapa sio kusoma tasbihi tu, bali ni pamoja na kumwelekea na kumtegemea Yeye tu.

Kabla ya mawiyo jua ni kuashiria swala ya Alfajiri na kabla ya mach- weo yake ni swala ya Alasiri na nyakati za usiku pia umsabihi ni swala ya Maghrib na Isha na ncha za mchana ni Swala ya Adhuhuri.

Limetumika neno ncha ya mchana kwa maana ya katikati ya mchana, kwa kuangalia kuwa ni ncha ya mwisho ya nusu ya kwanza ya mchana na ncha ya mwanzo ya nusu ya pili yake.

Sio mbali kuwa makusudio ya nyakati hizi ni amri ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu kila wakati; sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Ambao wanamataja Mwenyezi Mungu katika hali ya kusimama na kukaa na kulala” Juz. 4 (3:191).

Ili uridhike.

Kila anayemridhisha Mwenyezi Mungu duniani, humridhia Mwenyezi Mungu Akhera. “Mwenyezi Mungu yuko radhi nao na wao wako radhi naye.” (98:9).

Wala usivikodolee macho tulivyowastarehesha aina ya watu miongoni mwao, kwa mapambo ya duniani ili tuwajaribu. Na riziki ya Mola wako ni bora na yenye kudumu zaidi.

Makusudio ya usikodolee ni usitilie umuhimu; baadhi ni aina ya makafiri, wawe washirikina au watu wa kitabu.

Maana ni kuwa usijishughulishe ewe Muhammad na utajiri na unayoyaona kwa makafiri wa aina yoyote; wawe washirikina, wanaswara au mayahudi. Kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametaka kuwapa mali ili idhihiri hakika yao na awalipe kwa kupituka kwao mipaka.

Imam Ali (a.s.) anasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anawajaribu kwa mali na watoto, ili abainike anayeichukia riziki ya Mwenyezi Mungu na anayeiridhia; ingawaje Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anajua zaidi hakika yao, lakini ni kudhihirisha vitendo ambavyo vinastahiki thawabu na adhabu.”

Katika Tafsir At-Twabariy imeelezwa kwamba Mtume (s.a.w.) alituma kwa Myahudi akopeshwe, lakini yule myahudi akakataa ispokuwa kwa rahani Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) akahuzunika, ndipo ikashuka Aya hii. Ni sawa riwaya hii iwe sahihi au la, lakini ni mfano wazi wa kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Wala usivikodolee macho tulivyowastarehesha aina ya watu miongoni mwao, kwa mapambo ya duniani’

Ufukara Wa Mtume Ni Muujiza Mkubwa

Sisi hivi sasa tuko katika mwaka 1969; kiasi cha miaka 35, aliaandika mwandishi mashuhuri, Aliyeitwa Mustafa Sadiq Arrafi’y, makala mbili kuhusu ufukara wa Mtume (s.a.w.) yenye kichwa cha maneno: ‘Ufukara mtukufu.’
Tutanukuu kutoka katika makala hizo jumla zifutazo pamoja na nyongeza kidogo katika baadhi ya matamko, ili kuleta ufafanuzi:

“Ni jambo la kushangaza katika maisha kwa mtu fukara kuendelea na ufukara naye anajua kuwa kazi yake katika mji ni kufanya watu wawe matajiri. Na kuwa mtu tajiri anaendelea na utajiri na anajua kuwa kazi yake ni kuwafanya watu wawe mafukara.”

Muhammad (s.a.w.) aliishi fukara, lakini ufukara wake ulikuwa ukihisabi- ka kuwa ni katika muujiza wake mikubwa ambao hakuugundua yeyote hadi sasa. Muhammad (s.a.w.) alikuwa akimiliki mali, lakini alikuwa akiitoa kwa haraka kuliko upepo, hakutaka izaliane kwake; bali haikuwa ikitulia kwake.

Alikuwa – naye ndiye bwana mkubwa wa uma wake na mwenye sharia – ni mtu fukara akijitaabisha kutafuta maisha yake, siku nyingine anabaki na njaa na siku nyingine anashiba. Lengo lake la kwanza katika hilo ni kuuthibisha umoja wa ubinadamu na kuleta uuwiano baina ya watu na ajue kila mtu kwamba tatizo lake ni tatizo la jamii na kwamba mafanikio yake yawe mafanikio ya wote, sio kula mafanikio ya wengine ili waangamie.”

Na uwaamrishe watu wako kuswali na uwe na subira nayo.

Kuwa na subira na swala ni kutoathiriwa na jambo lolote. Katika Tafsir Arrazi, imeelezwa kuwa baada ya kushuka Aya hii Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikuwa akienda kwa Fatima (a.s.) kila asubuhi na kusema: Swala! Swala! Alifanya hivyo kwa miezi kadhaa.

Hatukuombi riziki.

Yaaniwewehuuombwirizikiyayoyote,sichakulachakewalakinywaji chake Sisi tunakuruzuku wewe na familia yako.

Haya yametajwa baada ya Swala; kuashiria kuwa Swala haizuii kitu chochote katika kazi ya kutafuta riziki na kwamba kuyachanganya yote mawili ni jambo jepesi. Kwa sababu Swala ina wakati maalumu ambao haumalizi ispokuwa dakika chache tu.

Na mwisho mwema ni kwa mwenye takua mwenye kucha kumwasi Mungu na alioyaharamisha kwa siri na kwa dhahiri.

Imam Ali (a.s.) anasema: “Hakuna utukufu zaidi kuliko Uislamu, wala enzi kuliko takua, wala ngome kuliko kuchunga haki, wala muombezi mwenye kufaulu kuliko toba, wala hazina kubwa kuliko kukinai... na mwenye kutosheka na kiasi cha haja atakuwa na raha.”

وَقَالُوا لَوْلَا يَأْتِينَا بِآيَةٍ مِنْ رَبِّهِ ۚ أَوَلَمْ تَأْتِهِمْ بَيِّنَةُ مَا فِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ {133}

Na walisema: “Kwa nini hakutuletea ishara kutoka kwa Mola wake? Je, haikuwajia dalili wazi ya yaliomo katika vitabu vya mwanzo?”

وَلَوْ أَنَّا أَهْلَكْنَاهُمْ بِعَذَابٍ مِنْ قَبْلِهِ لَقَالُوا رَبَّنَا لَوْلَا أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ آيَاتِكَ مِنْ قَبْلِ أَنْ نَذِلَّ وَنَخْزَىٰ {134}

Na lau tungeliwaangamiza kwa adhabu kabla yake, wangelisema: Ewe Mola wetu! Kwa nini usituletee mtume tukazifuata ishara zako kabla hatujadhalilika na tukahizika?

قُلْ كُلٌّ مُتَرَبِّصٌ فَتَرَبَّصُوا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ أَصْحَابُ الصِّرَاطِ السَّوِيِّ وَمَنِ اهْتَدَىٰ {135}

Sema: Kila mmoja anangoja; basi ngojeni punde mtajua nani mwenye njia sawa na nani aliyeongoka.