Dibaji
“Mola wangu Mlezi! nijaalie niwe msimamishaji Swala na kizazi changu, Mola wetu! na upokee maombi yangu”1
Himidi zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu, kisha rehma na amani ziwe juu ya mjumbe wa Allah na kizazi chake kitakasifu kitoharifu.
Utumishi wa mja kwa Mwenyezi Mungu ndiyo lengo la kila amali, na Swala ndiyo nyenzo yake, kwani ni ngazi ya muumini na ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu. Anasema Imam Al-Baqir (a.s): “Kitu cha kwanza atakachohesabiwa muumini (Siku ya Kiyama) ni Swala, ikikubaliwa yatakubaliwa matendo mengine, na ikikataliwa basi yatakataliwa matendo mengine.”2
Kutokana na ukweli huu, tumeonelea vyema kukipa kizazi chipukizi fursa ya kuyatambua yale yanayokihusu kwa kutoa mfululizo wa sheria kwa njia rahisi na maudhui nyepesi kufahamika, kwa kuweka kitabu maalumu chenye picha zinazofafanua mada na kumuonyesha mpendwa msomaji namna ya kutekeleza ibada na taratibu zake kwa njia nyepesi na rahisi.
Kitabu hiki tumekiita Swala ni nguzo kuu ya dini. Tunamuomba Mola Mtukufu akifanye kitabu hiki kiwe chenye manufaa kwa Waislamu, na hasa vijana wa umma huu ambao ndio tegemeo la mustakabali wake, na atukubalie kazi yetu hii ndogo katika kuitumikia dini Yake tukufu.
Ewe Mola wetu! Tukubalie, hakika Wewe ni Msikivu, Mjuzi.
Mustafa Ranjibar Shiraz.
E: mail: [email protected]