read

Sura Ya Ishirini Na Tatu: Al-Mu’minun

ImeshukaMakkainaAya118.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ {1}

Hakika wamefaulu waumini.

الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ {2}

Ambao ni wanyenyekevu katika Swala zao.

وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ {3}

Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi.

وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ {4}

Na ambao kwa Zaka ni watendaji.

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ {5}

Na ambao wanazilinda tupu zao.

إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ {6}

Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume. Kwani si wenye kulaumiwa.

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ {7}

Lakini anayetaka kinyume cha hayo basi hao ndio wapetukao mipaka.

وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ {8}

Na wale ambao wanachunga amana zao na ahadi zao.

وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ {9}

Na ambao Swala zao wanazihifadhi.

أُولَٰئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ {10}

Hao ndio warithi.

الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ {11}

Watakaorithi Firdausi, wadumu humo.