read

Aya 31-41: Hud

Kisha baada yao tukaanzisha karne nyingine.

Makusudio ya karne hapa ni watu. Mwenyezi Mungu hakuweka wazi ni akina nani hao. Wafasiri wamesema hao ni A'd, kaumu ya Hud. Na hii ni sawa kwa dalili ya yaliyokuja katika Juz.8 (7:65). Yametangulia maelezo katika Juz. 12 (11: 50 - 65). Kwa hiyo tutapita juu juu, kwenye Aya hizi, kama tulivyopita kwenye Aya zilizotangulia hizi.

Tukawapelekea Mtume mingoni mwao.

Mwenyezi Mungu alimtuma Hud kwa A'd naye ni miongoni mwao.

Kwamba mumwabudu Mwenyezi Mungu! Hamna Mungu asiyekuwa Yeye, je hamuogopi?

Aliwapa watu wake mwito wa tawhid na kuacha shirk kwa kutoa bishara ya radhi za Mwenyezi Mungu na thawabu zake na kutoa onyo la hasira za Mweyezi Mungu na adhabu yake.

Na wakuu katika watu wake waliokufuru na wakakanusha mkutano wa Akhera na tukawadekeza kwa starehe katika maisha ya dunia, walisema:

Huyu si chochote ila ni binadamu kama nyinyi, anakula mlacho na anakunywa mnywacho.

Maadamu yuko hivyo hivyo basi hana tofauti wala ubora, basi vipi mnamtii.

Na nyinyi mkimtii mtu kama nyinyi basi hakika mtakuwa hasarani.

Wao ndio wako hasarani kiiudhahiri na kiuhalisi kutokana na kumuasi kwao Nabii. Lakini wamepindua na wakaufinika uhakika. Haya ndiyo mazoweya ya matwaghuti na wanaodeka kila mahali na kila wakati.

Je, anawaahidi ati mtakapokufa na mkawa mchanga na mifupa kwamba mtatolewa?

Makaburini kuwa hai kama mlivyo sasa. Hiki ni kitu cha ajabu.

Hayawi! Hayawi hayo mnayoahidiwa kuwa kuna ufufuo baada ya mauti. Hakuna ila maisha yetu ya dunia tu, tunakufa na tunaishi. Wala sisi si wenye kufufuliwa.

Kwa sababu aliyekufa na yake yamekwisha. Huu ni ubainifu wa yaliyotangulia, ya kuona kwao muhali kufufuliwa baada ya mauti, wakiwa wameghafilika kwamba aliyewaumba kwanza ndiye huyo huyo atakayewarudisha; na kwamba hilo ni rahisi zaidi kuliko kuanzisha, kama ni sawa ibara yao.

Huyo si lolote ila ni mtu anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo, wala sisi si wenye kumwamini.

Hawamwamini Hud kwa sababu anasema uongo juu ya Mwenyezi Mungu, lakini kuabudu kwao masanmu ndio ikhlasi ya kweli kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na takua!! Aliye mtupu zaidi katika watu ni yule anayefanya uovu kisha akajiona amefanya wema.

Akasema: Mola wangu, ninusuru kwa wanavyonikanusha.

Alisema hivi baada ya kukata tamaa na kuongoka kwao.

Akasema - Mwenyezi Mungu - baada ya muda mchache hakika watakuwa ni wenye kujuta, kutokana na shirki yao na uasi wao ambapo Mwenyezi Mungu atawapatiliza kwa mpatilizo wa mwenye nguvu mwenye uwezo.

Basi ukawanyakua ukelele kwa haki.

Makusudio ya ukelele ni adhabu. Kusema kwake kwa haki ni ishara ya kuwa wanastahili adhabu kutokana na waliyoyafanya.

Tukawafanya takataka zinazoelea juu ya maji.

Yaani wako sawasawa na vitu duni vinavyoelea kwenye maji.

Ikapotelea mbali kaumu ya madhalimu.

Wamepotelea mbali na Mwenyezi Mungu na twaa yake naye akawaweka mbali na fadhila zake na rehema zake.

ثُمَّ أَنْشَأْنَا مِنْ بَعْدِهِمْ قُرُونًا آخَرِينَ {42}

Kisha baada yao tukaanzisha karne niyingine.

مَا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ {43}

Hapana umma unaoweza kutanguliza ajali yake wala kuikawiza.

ثُمَّ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا تَتْرَىٰ ۖ كُلَّ مَا جَاءَ أُمَّةً رَسُولُهَا كَذَّبُوهُ ۚ فَأَتْبَعْنَا بَعْضَهُمْ بَعْضًا وَجَعَلْنَاهُمْ أَحَادِيثَ ۚ فَبُعْدًا لِقَوْمٍ لَا يُؤْمِنُونَ {44}

Kisha tukawapeleka mitume wetu mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipowafikia Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatishia baadhi yao wengine, ikapotelea mbali kaumu isiyoamini.

ثُمَّ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ وَأَخَاهُ هَارُونَ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُبِينٍ {45}

Kisha tukamtuma Musa na nduguye Harun pamoja na ishara zetu, na hoja zilizo wazi.

إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا عَالِينَ {46}

Kwenda kwa Firaun na wakuu wake, lakini wakajivu- na na walikuwa ni kaumu waliojikweza.

فَقَالُوا أَنُؤْمِنُ لِبَشَرَيْنِ مِثْلِنَا وَقَوْمُهُمَا لَنَا عَابِدُونَ {47}

Wakasema: Je, tuwaamini watu wawili hawa kama sisi, na ambao watu wao ni watumwa wetu?

فَكَذَّبُوهُمَا فَكَانُوا مِنَ الْمُهْلَكِينَ {48}

Basi wakawakadhibisha wakawa miongoni mwa walioangamizwa.

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ {49}

Na hakika tulimpa Musa Kitabu ili wapate kuongoka.

وَجَعَلْنَا ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ آيَةً وَآوَيْنَاهُمَا إِلَىٰ رَبْوَةٍ ذَاتِ قَرَارٍ وَمَعِينٍ {50}

Tukamfanya mwana wa Maryam na mama yake kuwa ni ishara. Na tukawapa kimbilio kwenda mahali palipoinuka, penye utulivu na chemchem za maji.