read

Aya 73 – 80:Unawaita Kenye Njia Iliyonyooka

Na hakika wewe unawaita kwenye njia iliyonyooka. Na hakika wale ambao hawaiamini akhera wanajitenga na njia hiyo.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuelezea upotevu wa washirikina na kwamba wao hawana udhuru wowote wa kumkanusha kwao Muhammad (s.a.w.), sasa anamwambia Mtume wake Mtukufu kwamba yeye anazo hoja za kutosha kuwa yeye ni mkweli katika mwito wake na kwamba washirikina ambao wamemkanusha yeye na siku ya mwisho wameiacha haki na wakapotea njia ya kheri na uongofu. Nao, katika hilo, wanajidhu- ru wenyewe na hawatakudhuru wewe na chochote.

Lau tungeliwarehemu tukawaondolea shida waliyo nayo, bila shaka wangeliendelea na upotevu wao wakimangamanga.

Baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) kuhamia Madina kutoka Makka aliwapa dhiki makuraishi kwa kutuma vikosi kuwazuilia njia, mara nyingine alikuwa akiviongoza mwenyewe, na akaamrisha kuwakatia uhu- siano. Basi wakaingia kwenye dhiki, lakini bado waliendelea na upotevu wao na kufuru yao. Lau kama Mwenyezi Mungu (s.w.t) angeliwaondolea shida waliyo nayo, wasingelizingatia kuachana na upotevu wao.

Na hakika tuliwatia katika adhabu, lakini hawakuelekea kwa Mola wao wala hawakunyenyekea.

Ukiwahadharisha wanapinga, ukiwatia adabu hawazingatii na ukiwaondolea wanakuwa jeuri. Watakuwa hivi mpaka siku watakapofufuliwa, watakpoondolewa pazia washuhudie malipo ya mghafala wao na jeuri yao. Hapo watakata tamaa ya kuokoka na kujutia yaliyopita.

Mpaka tulipowafungulia mlango wa adhabu kali, hapo ndipo wakawa wenye kukata tamaa na hali Mwenyezi Mungu (s.w.t) alikwishawahadharisha na adhabu hii kali na kuwapa kiaga, lakini wakapuuza nafsi zao wakazipeleka kwenye maangamizi.

Yeye ndiye aliyewaumbia kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu, ili mnufaike kwa mtakyoyasikia na kuyaona muweze kujua ya kheri na masilahi.

Neema za Mwenyezi Mungu kwa mtu hazina idadi, kubwa yake ni akili kisha usikizi na uoni. Ametangulia kutaja usikizi kwa sababu mtoto anayezaliwa huanza kusikia tangu kuzaliwa kwake, wala haoni mpaka siku ya nne; kama wanavyosema. Ama kuchelewa akili hilo liko wazi.

Ni kuchache mno kushukuru kwenu; yaani kutii kwenu.

Yeye ndiye aliyewaumba katika ardhi na kwake mtakusanywa.

Alituuumba katika ardhi hii kisha atatufufua kwake baada ya mauti. Yeye ndiye anayehuisha na kufisha na Yeye ndiye mwenye mabadiliko ya usiku na mchana. Basi je, hamfahamu? Hakika huu ni utengenezaji wa Mwenye uweza aliye Mjuzi. Tazama Juz. 1 (2:28 -29) na Juz. 3: (3:26-27).

بَلْ قَالُوا مِثْلَ مَا قَالَ الْأَوَّلُونَ {81}

Bali walisema kama walivyosema wa mwanzo.

قَالُوا أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ {82}

Je, tukishakufa tukawa mchanga na mifupa ndio tutafufuliwa?

لَقَدْ وُعِدْنَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا هَٰذَا مِنْ قَبْلُ إِنْ هَٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ {83}

Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni vigano vya wa kale.

قُلْ لِمَنِ الْأَرْضُ وَمَنْ فِيهَا إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ {84}

Sema, ni ya nani ardhi na vilivyomo ndani yake, kama nyinyi mnajua?

سَيَقُولُونَ لِلَّهِ ۚ قُلْ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ {85}

Watasema, ni vya Mwenyzi Mungu. Basi je, hamkumbuki?

قُلْ مَنْ رَبُّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ {86}

Sema, ni nani Mola wa mbingu saba na Mola wa arshi tukufu?

سَيَقُولُونَ لِلَّهِ ۚ قُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ {87}

Watasema, ni vya Mwenyezi Mungu. Sema, basi je, hamuogopi?

قُلْ مَنْ بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ {88}

Sema, ni nani mkononi mwake umo ufalme wa kila kitu? Na yeye ni mlinzi wala hapalindwi kwake, kama mnajua.

سَيَقُولُونَ لِلَّهِ ۚ قُلْ فَأَنَّىٰ تُسْحَرُونَ {89}

Watasema, ni wa Mwenyezi Mungu. Sema, basi vipi mnadanganyika?

بَلْ أَتَيْنَاهُمْ بِالْحَقِّ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ {90}

Bali tumewaletea haki. Na kwa hakika wao ni waongo.