Aya 6-10: Kuapizana Mume Na Mke
Maana
Katika vitabu vya Fiqh kuna mlango unaoitwa Lian, ambao chimbuko lake ni Aya hizi. Inafanana na kuapizana baina ya mume anayemtuhumu mkewe na zina bila ya kuwa na ushahidi wa madai yake, na mke kuikana tuhuma ya zina yeye mwenyewe. Lengo la kulaniana huku ni kuondoka adhabu ya kutuhumu au kumkana mtoto. Liani haiwi ila katika hali mbili:
Kwanza: Mtu kumtuhumu na zina mkewe wa kisharia aliyemuoa kwa ndoa ya daima. Ni lazima mke awe si kiziwi wala bubu, mume adai kushuhudia na asiwe na ubainifu wa kisharia juu ya hiyo zina, zikikosekana sharti hizi basi haijuzu kulaniana.
Pili: Kumkana mume mtoto wa kitanda chake, ikiwa mimba haikupungua miezi sita au kuzidi mwaka. Vinginevyo anaweza kumkana mtoto bila ya kulaniana.
Basi ikiwa mume atamtuhumu mkewe na zina au kumkana mtoto,anatakikana apate adhabu (had) ya kutukana, ila akileta ushahidi au kulaniana.
Sura ya kulaniana ni kusema mbele ya hakimu wa sharia: Ninashuduia kuwa mimi ni mkweli kwa ninayoyasema kuhusu mke wangu fulani. Atasema hivyo mara nne; kisha atasema mara ya tano baada ya kuonywa na hakimu wa sharia: Laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yangu ikiwa ni muongo.
Mke naye atashuhudia mara nne kwamba huyo mume ni muongo kwa aliyomtuhumu nayo. Mara ya tano atasema ghadhabu za Mwenyezi Mungu zimshukie ikiwa huyo mume ni mkweli.
Ni lazima wote wawili wawe wamekaa wakati wa kulaniana. Kukishatimia kulaniana kwa masharti yake, matokeo yatakuwa ni mambo yafuatayo:-
1. Ndoa itavunjika.
2. Uharamu wa milele baina ya mume na mke (hawawezi kurudiana tena).
3. Adhabu ya kutuhumu itaondoka kwa mume.
4. Mtoto hatakuwa wa mume. Hawatarithiana wala halazimiki kumtunza. Lakini atakuwa ni wa mama kisharia.
Tukijua kulaniana baina ya mume na mke, itakuwa tumejua makusudio ya Aya hizi. Kwa hiyo basi tutafupiliza kufasiri kwa kutaja matamko yanayoashiriwa na mfumo wa maneno.
Na wale wanaowasingizia wake zao kwa zina na hawana mashahidi ila nafsi zao kutokana na madai yao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba hakika yeye ni katika wasema kweli.
Atayasema hayo mbele ya hakimu wa sharia.
Na mara ya tano kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo.
Yaani ikiwa ni muongo katika madai yake. Na mke itamwondokea adhabu kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu, kwamba huyo mume ni miongoni mwa waongo. Mke naye atatoa ushahidi wake mbele ya hakimu wa sharia kama alivyofanya mume.
Na mara ya tano kwamba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, kama mume ni miongoni mwa wasemao kweli katika haya madai yake kwangu.
Na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeliangamia.
Na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutakabali, toba Mwenye hekima.
Hii ni kuashria hekima ya sharia ya kuapizana, kwamba lengo ni kusitiri na kuondoa adhabu kwa mume na kutoa nafasi kwa mke kujitetea na tuhumu za mume.
إِنَّ الَّذِينَ جَاءُوا بِالْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِنْكُمْ ۚ لَا تَحْسَبُوهُ شَرًّا لَكُمْ ۖ بَلْ هُوَ خَيْرٌ لَكُمْ ۚ لِكُلِّ امْرِئٍ مِنْهُمْ مَا اكْتَسَبَ مِنَ الْإِثْمِ ۚ وَالَّذِي تَوَلَّىٰ كِبْرَهُ مِنْهُمْ لَهُ عَذَابٌ عَظِيمٌ {11}
لَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ الْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بِأَنْفُسِهِمْ خَيْرًا وَقَالُوا هَٰذَا إِفْكٌ مُبِينٌ {12}
لَوْلَا جَاءُوا عَلَيْهِ بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ ۚ فَإِذْ لَمْ يَأْتُوا بِالشُّهَدَاءِ فَأُولَٰئِكَ عِنْدَ اللَّهِ هُمُ الْكَاذِبُونَ {13}
وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ لَمَسَّكُمْ فِي مَا أَفَضْتُمْ فِيهِ عَذَابٌ عَظِيمٌ {14}
إِذْ تَلَقَّوْنَهُ بِأَلْسِنَتِكُمْ وَتَقُولُونَ بِأَفْوَاهِكُمْ مَا لَيْسَ لَكُمْ بِهِ عِلْمٌ وَتَحْسَبُونَهُ هَيِّنًا وَهُوَ عِنْدَ اللَّهِ عَظِيمٌ {15}
وَلَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ قُلْتُمْ مَا يَكُونُ لَنَا أَنْ نَتَكَلَّمَ بِهَٰذَا سُبْحَانَكَ هَٰذَا بُهْتَانٌ عَظِيمٌ {16}
يَعِظُكُمُ اللَّهُ أَنْ تَعُودُوا لِمِثْلِهِ أَبَدًا إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ {17}
وَيُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمُ الْآيَاتِ ۚ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ {18}
إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَنْ تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ {19}
وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ وَأَنَّ اللَّهَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ {20}