Aya 47 – 54: Wanafiki
Maana
Na wanasema tumeamini Mwenyezi Mungu na Mtume na tumetii. Kisha kikundi katika hao hugeuka baada ya hayo. Wala wao si wenye kuamini.
Ambao husema tumeamini na tumetii, wako aina tatu: Ya kwanza, ni wale wanaosema kwa ulimi yale wanayoyaamini, kuyakubali moyoni na kufanya kwa mujibu wake. Hawa sio waliokusudiwa kwenye Aya tuliyo nayo.
Aina ya pili, ni wale wanaosema na kuamini, lakini wanaasi wala hawatendi kwa mujibu wake; yaani wanamini kinadharia sio kimatendo.
Aina ya tatu, ni wale wanaosema kwa ndimi zao yale ambayo hayamo nyoyoni mwao kabisa. Hawa ndio wanafiki.
Aya tuliyo nayo inahusu aina ya pili na ya tatu; wala haihusiki na wanafiki tu; kama ilivyosemekana. Kwa sababu imani bila matendo haina faida yoyote, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Basi mtu haitamfaa imani yake ambaye hakuamini zamani au hakuchuma kheri kwa imani yake" Ju. 8 (6:158).
Na wanapoitwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili awahukumu baina yao, ndipo kikundi kimoja kinakataa.
Wafasiri wengi wanasema kuwa kulitokea ugomvi wa ardhi baina ya mnafiki mmoja na Yahudi. Mnafiki akasema tukaamuliwe kwa Ka'bul-akhbar, Myahudi, kwa kujua kuwa anakubali rushwa. Myahudi akamwambia tukahukumiwe kwa Muhammad kwa kujua kuwa hakubali rushwa. Lakini mnafiki alikataa. Ndio ikashuka Aya hii. Ni sawa iwe riwaya ni sahihi au la, lakini inafafanua zaidi tafisiri ya Aya.
Ijaribu Dini Yako Na Imani Yako
Na ikiwa haki ni yao wanamjia kwa kutii.
Wao hawaijui haki ila ikiafikiana na matamanio yao; kama ikihalifiana nayo basi wanaikana. Huu ndio ubinafsi ambao hauhusiki na wanafiki tu; isipokuwa uko katika maisha ya baadhi ya waumini au wale wanaojiita waumin. Wanadai kuwa wanaidhihirisha haki na wanipinga batili. Lakini ni haki gani hiyo wanayoidhihirisha na batili gani hiyo wanayoipinga?
Katika ufahamu wao na imani yao, haki ni ile inayoafikiana na masilahi yao na batili ni ile inayohalifiana na masilahi yao. Wao wamejisahau.
Wanaamini kuwa hawatendi isipokuwa haki na hawatamki isipokuwa ukweli, lakini hawapati msukumo wa hilo, isipokuwa kwa msukumo wa hawaa na masilahi yao.
Hawa wana hali mbaya zaidi kuliko wanafiki ambao wanawadanganya watu na hawajidanganyi wao wenyewe. Kwa sababu wana uhakika na uongo wao na riya yao.
Lakini hawa wanafanya uovu wenyewe wakijiona wanafanya wema. Sio siri kusema kuwa wao hawana sifa ya imani. Kwa sababu mumin wa kweli hahadaiki na hila za shetani na ubatilifu wake; bali anajituhumu ikiwa kitendo chake kitampambia sifa. Kwani kazi muhimu ya shetani ni kuwapambia watu matendo yao maovu, kuwaonyesha batili kuwa ni haki na upotevu kuwa ni unyoofu.
Inasemekana kuwa mtu mmoja alimwambia Iblisi: "Wewe huwawezi wau- mini mfano wangu." Ibilisi akacheka na kumwambia maneno yako haya tayari yanaonyesha umekwishaingia kwenye mtego. Ghururi yako hii ni mtekelezaji aliyeingia moyoni mwako, akauharibu na akaupofusha mpaka ukawa hauna hisia.
Baada ya hayo! Mwenye kutaka kuijaribu imani na dini yake, inatakikana aangalie, kuwa je, anaituhumu nafsi yake au anaiona ni safi isiyokuwa na kasoro? Je, anaikubali haki hata kama ni dhidi yake? Ikiwa atajituhumu na kuikubali haki kwa namna yoyote itakayokuwa basi yeye ni katika waumini, vinginevyo atakuwa katika walioangamia.
Je, wana maradhi katika nyoyo zao au wanaona shaka au wanahofia kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake watawadhulumu? Bali wao ndio madhalimu.
Walikataa kuhukumiwa kwa Mtume; wala hakuna lililopelekea hilo ila chuki yao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu au kuutilia shaka utume wake au kuhofia kuwa atawadhulumu. Sababu yoyote itakayokuwa, lakini hakatai hukumu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) isipokuwa kafiri au aliyeidhulumu nafsi yake na ya mwingine.
Haiwi kauli ya waumini wanapoitwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ila ni kusema: Tumesikia na tumetii. Na hao ndio wenye kufaulu.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kutaja wanafiki na kwamba wao wana- jizuia kuiendea mahakama ya Mtume wanapoitwa huko, sasa anataja waumini, kwamba ni wale wanaomwitikia kila atakayewapa mwito wa kwenda kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wanaitikia mwito wake kwa unyenyekevu na utiifu. Hawa ndio wanachama wa Mwenyezi Mungu "Hakika wanachama wa Mwenyezi Mungu ndio wenye kufanikiwa." (58:22)
Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakamwogopa Mwenyezi Mungu na wakamcha, basi hao ndio wenye kufuzu kwa kupata radhi za Mwenyezi Mungu na pepo yake.
Kuunganisha hofu na uchaji kwenye utiifu, ni kwa upande wa kuunganisha kitafsiri. Kwa sababu mwenye kumtii Mwenyezi Mungu atakuwa amemuhofia na kumcha. Lakini wafasiri hawakukubali ila kutafoutisha baina ya matendo haya. Wakasema: kumtii Mwenyezi Mungu kunakuwa katika aliyoyaamrisha na kuyakataza, kumhofia kunakuwa katika maasi na kumcha kunakuwa katika yatakayokuja.
Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwa ukomo wa viapo vyao ya kwamba ukiwaamrisha, hakika watatoka.
Walioapa ni wanafiki. Wao waliaapa kwa kiapo cha nguvu kwamba Mtume akiwaamrisha waache majumba yao na mali zao basi watamsikiliza na kumtii, ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawakemea na imani yao hiyo ya uongo kwa kusema:
Sema: msiape! Utiifu unajulikana. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.
Yaani ewe Muhammad! Waambie wanafiki, msiape kwani Mwenyezi Mungu anajua kuwa utiifu wenu huu ni wa uongo na wa kujionyesha (ria) na kwamba nyinyi ni maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na amewaandalia adhabu chungu mnayostahiki.
Sema: Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa dhahiri na batini, sio kwa unafiki na ria.
Kama mkikengeuka basi yaliyo juu yake ni aliyobebeshwa, na yaliyo juu yenu ni mliyobebeshwa.
Wanaambiwa wanafiki, na yaliyo juu yake ni juu yake Mtume. Maana ni kuwa Mtume ni mwenye kukalifiwa kufikisha na nyinyi ni wenye kukalifiwa kutii. Atakayepuuza basi hisabu ya kupuuza itakuwa ni yake; ni sawa awe ni Mtume au yule aliyetumiwa Mtume.
Na mkimtii yeye mtaongoka na hapana juu ya mtume ila kufikisha (ujumbe) wazi wazi. Mwenye kutekeleza aliyokalifishwa, basi malipo yake yako kwa Mwenyezi Mungu.
Mtume amekwishafikisha na kutekeleza wajibu wake, yaliyobaki, kazi kwenu.
وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ {55}
وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ {56}
لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ وَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۖ وَلَبِئْسَ الْمَصِيرُ {57}