Aya 65 – 75: Mjuzi Wa Ghaibu Na Ufufuo
Maana
Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipokuwa Mwenyezi Mungu; wala wao hawajui lini watafufuliwa.
Wapinzani walimtaka Mtume (s.a.w) awawekee muda maalum wa ufufuo, ndio Aliye Mtukufu na kutukuka akamwambia: Waambie kuwa hakuna yeyote katika watu majini na hata malaika anayejua ghaibu na muda wa ufufuo isipokuwa Mwenyezi Mungu tu, na kwamba wao watafufuliwa bila ya kujua.
Bali ujuzi wao umefikia kuijua Akhera.
Yaani Mitume waliwapa habari washirikina, lakini hawakumwaamini; watakapofufuliwa na kuiona Akhera kwa macho watajua kuwa yale waliyoelezwa na mitume kuwa ni kweli.
Bali wao wamo katika shaka nayo.
Vipi wanaulizia wakati wa Akhera na hali wao hawaiamini?
Bali wao ni vipofu nayo.
Nyoyo zao zimekuwa na upofu wa Akhera kwa sababu ya upotevu wao na inadi yao.
Na wakasema wale ambao wamekufuru: Tutakapokuwa mchanga, sisi na baba zetu, hivyo kweli tutakujatolewa? Haya tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni ngano za watu wa kale.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:5) na Juz. 18 (23: 35 – 36 na 82 – 83).
Sema: Nendeni katika ardhi na tazameni ulikuwaje mwisho wa wakosefu.
Haya ni makemeo kwa yule anayekadhibisha utume wa Muhammad (s.a.w.), kuwa atapatwa na maangamizi kama yaliyowapata wengine katika umma zilizotangulia ambao waliwakadhibisha mitume wao.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:137).
Wala usiwahuzunikie wala usiwe katika dhiki kwa hila wanazozi- fanya.
Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 14 (16:127).
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini ikiwa mnasema kweli.
Mtume (s.a.w.) aliwahadharisha makuraishi na mwisho mbaya wa kukadhibisha kwao na uasi wao, wao wakamwambia kwa kumfanyia maskhara: Hilo litakuwa lini? Kila Mtume alisikia jawabu kama hili la dharau kutoka kwa watu wake pale alipowahadharisha.
Sema: Asaa ikawafikia sehemu ya yale mnayoyahimiza.
Huenda adhabu iko nyuma yenu na nyinyi hamjui. Maana ya Aya hii yako kwenye Aya: “Na watasema: lini hayo? Sema: asaa yakawa karibu.” Juz. 15 (17:51).
Na hakika Mola wako ni mwenye fadhila kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anawafadhili kwa kuwapa muda na kuwacheleweshea adhabu ili watubie na warudi kutoka kwenye upotevu wao. Ilikuwa ni wajibu wao washukuru hilo, lakini badala yake wanahimiza adhabu kwa dharau.
Na hakika Mola wako anayajua yanayoficha vifua vyao na wanayoy- atangaza.
Walitangaza kumshirikisha Mwenyezi Mungu na wakaficha njama na shari dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyaficha na wanayoyadhihirisha.
Naye atawalipa tu kwa haya na yale kulingana na wanavyostahili.
Na hakuna siri katika mbingu na ardhi ila imo katika kitabu kinachobainisha.
Hakuna siri katika ujuzi wa Mwenyezi Mungu hilo halina shaka, lakini makusudio ya kulieleza hilo ni onyo na hadhari kwa wahaini na vibaraka ambao wanajificha nyuma ya pazia la unafiki na ria.
إِنَّ هَٰذَا الْقُرْآنَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَكْثَرَ الَّذِي هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ {76}
وَإِنَّهُ لَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِلْمُؤْمِنِينَ {77}
إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ بِحُكْمِهِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ {78}
فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ ۖ إِنَّكَ عَلَى الْحَقِّ الْمُبِينِ {79}
إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا وَلَّوْا مُدْبِرِينَ {80}
وَمَا أَنْتَ بِهَادِي الْعُمْيِ عَنْ ضَلَالَتِهِمْ ۖ إِنْ تُسْمِعُ إِلَّا مَنْ يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُمْ مُسْلِمُونَ {81}
وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِنَ الْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ {82}
وَيَوْمَ نَحْشُرُ مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ فَوْجًا مِمَّنْ يُكَذِّبُ بِآيَاتِنَا فَهُمْ يُوزَعُونَ {83}
حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوا قَالَ أَكَذَّبْتُمْ بِآيَاتِي وَلَمْ تُحِيطُوا بِهَا عِلْمًا أَمَّاذَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ {84}
وَوَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ بِمَا ظَلَمُوا فَهُمْ لَا يَنْطِقُونَ {85}