Aya 62 – 70: Wako Wapi Washirika Wangu
Maana
Na siku atakapowaita na akasema: Wako wapi mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu.
Kesho Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atawafufua waabudu mizimu, vyeo na mali awaulize kwa kuwatahayariza, wako wapi mliokuwa mkiwatumikia na kuwasafia matendo yenu badala ya Mwenyezi Mungu?
Watasema wale iliyothibiti juu yao kauli: Mola wetu! Hawa ndio tuliowapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyopotea sisi. Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi.
Makusudio ya waliothibitikiwa na kauli ni viongozi wa ushirikina na upotevu. Makusudio ya kauli ni tamko la adhabu lilikuja katika Aya isemayo:
قَالُوا بَلَىٰ وَلَٰكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ الْعَذَابِ عَلَى الْكَافِرِينَ {71}
Neno ‘Hawa’ ni ishara ya wafuasi wadhaifu.
Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) wakati atakapowauliza washirikina, wako wapi washirika wangu, wanyonge watajibu: Ewe Mola wetu! Sisi tuliwatii wakubwa zetu wakatupoteza njia.
Wakubwa nao watasema: Hapana, hatukuwalazimisha kufuata ushirikina na upotevu, lakini tuliwaita nao wakaitikia kwa hiyari yao; sawa na sisi tuliyoyaitikia matamanio yetu na kuyatii.
Nasi tunajitenga nao na matendo yao. Hawakuwa wakituabudu sisi, isipokuwa walikuwa wakiabudu masanamu na mashetani.
Hivi ndivyo wanavyofanya watu wa masilahi, wanawadanganya wapumbavu na wajinga na kuwafanya ni njia ya kupatia mlengo yao; mpaka yakiwafika wanawaruka.
Hawa watawaambia kama atakavyosema shetani kesho:
وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُمْ مِنْ سُلْطَانٍ إِلَّا أَنْ دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي ۖ فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنْفُسَكُمْ ۖ {22}
إِنِّي بَرِيءٌ مِنْكُمْ…إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ ۚ {48}
Na itasemwa: Waiteni waungu wenu wa kishirikina.
Itasemwa kesho kwa wasaidizi wa dhulma na wafuasi wao, wako wapi wale mliokuwa mkiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, waiteni waje wawaokoe na adhabu.
Basi watawaita, lakini hawatawaitikia.
Amedhoofika muombaji na anayeombwa.
Na wataiona adhabu; laiti wangelikuwa wameongoka.
Watajua kuwa adhabu inakuja tu. Hapo watatamani lau wangelikuwa waumini.
Na siku atakapowaita na akasema: Mliwajibu nini Mitume.
MarayapiliMwenyeziMungu(s.w.t.)anawaulizakwakukusudiakuwatahayariza kuwa niliwaletea mitume wangu wakawasomea Aya zangu na wakawaonya na kukutana kwenu na siku hii, basi mtafanya nini? Je, mliwaitikia na mkawatii au mliwapinga na kuwaasi?
Basi zitawapotea habari siku hiyo.
Watakuwa hawana la kujibu kwa jinsi watakavyopigwa na butwaa.
Nao hawataulizana.
Hawataulizana kuhusu litakalowaokoa na adhabu. Vipi wataulizana na hali wao wamekata tamaa na kila kitu.
Ama mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, asaa akawa miongoni mwa wenye kufanikiwa.
Hii ni desturi ya Qur’an – kuuunganisha kutaja utiifu na thawabu zake uasi na adhabu yake na kinyume chake.
Neno ‘asaa’ katika maneno ya viumbe linafahamisha kutarajia kitu kinachopendwa na kuhurumia jambo linalochukiza. Ama katika maneno ya muumba linafahamisha ulazima na uhakika. Kwa hiyo basi ni uhakika kuwa mwenye kutubia aliye mwema ni katika wenye kufaulu na wenye kuridhiwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Na Mola wako huumba na huteua atakavyo; hawana hiyari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanaowashirikisha naye.
Mwenyezi Mungu ndiye muumba na ni mmliki, hakuna anayemiliki kitu kwake. Vitendo vyake vyote ni hekima, heri na usawa. Hakuna yeyote anayeweza kupinga na kutaaradhi, basi vipi wanamnasibishia washirikina?
Na Mola wako anayajua yaliyoficha vifua vyao na wanayoyatangaza.
Vile vile yeye ni mjuzi wa ghaibu na dhahiri na washirika wanaodaiwa hawajui kitu.
Naye ni Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipokuwa yeye peke yake, mwenye kustahiki ibada.
Ni zake sifa njema, mwanzo na mwisho.
Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu duniani kutokana na fadhila zake na katika akhera kwa thawabu zake.
Na hukumu ni yake yenye kutokeza katika kila kitu. Na kwake yeye mtarejeshwa.
Wala haiwezekani kulikimbia hili. Mwema ni yule ambaye zitathibiti hoja zake na kukubaliwa udhuru wake.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ جَعَلَ اللَّهُ عَلَيْكُمُ اللَّيْلَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَٰهٌ غَيْرُ اللَّهِ يَأْتِيكُمْ بِضِيَاءٍ ۖ أَفَلَا تَسْمَعُونَ {71}
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ جَعَلَ اللَّهُ عَلَيْكُمُ النَّهَارَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَٰهٌ غَيْرُ اللَّهِ يَأْتِيكُمْ بِلَيْلٍ تَسْكُنُونَ فِيهِ ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ {72}
وَمِنْ رَحْمَتِهِ جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِنْ فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ {73}
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنْتُمْ تَزْعُمُونَ {74}
وَنَزَعْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا فَقُلْنَا هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ فَعَلِمُوا أَنَّ الْحَقَّ لِلَّهِ وَضَلَّ عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَفْتَرُونَ {75}