read

Sura Ya Ishirini Na Tisa: A’nkabut

Imesemekana kuwa imeshuka Makka, ina Aya 69.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

الم {1}

Alif Laam Miim.

أَحَسِبَ النَّاسُ أَنْ يُتْرَكُوا أَنْ يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ {2}

Je, wanadhani watu wataachwa waseme tumeamini nao wasijaribiwe?

وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ {3}

Hakika tuliwajaribu waliokuwa kabla yao. Kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wakweli na kwa yakini atawatambulisha waongo.

أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ أَنْ يَسْبِقُونَا ۚ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ {4}

Au wanadhani wanaotenda maovu kwamba watatushinda? Ni mabaya wanayohukumu.

مَنْ كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ اللَّهِ فَإِنَّ أَجَلَ اللَّهِ لَآتٍ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ {5}

Mwenye kutaraji kukutana na Mwenyezi Mungu, basi hakika miadi ya Mwenyezi Mungu itafika. Naye ni mwenye kusikia mwenye kujua.

وَمَنْ جَاهَدَ فَإِنَّمَا يُجَاهِدُ لِنَفْسِهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ لَغَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ {6}

Na anayefanya juhudi basi hakika anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu.

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَحْسَنَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ {7}

Na wale ambao wameamini na wakatenda mema, kwa hakika tutawaondolea maovu yao, na tutawalipa mazuri ya waliyokuwa wakiyatenda.

وَوَصَّيْنَا الْإِنْسَانَ بِوَالِدَيْهِ حُسْنًا ۖ وَإِنْ جَاهَدَاكَ لِتُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۚ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ {8}

Na tumemuusia mtu kuwatendea wema wazazi wake wawili. Na wakikushikilia unishirikishe mimi na yale usiyokuwa na ujuzi nayo, basi usiwatii. Kwangu mimi ndio marejeo yenu, na nitawaambia mnayoyatenda.

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُدْخِلَنَّهُمْ فِي الصَّالِحِينَ {9}

Na wale ambao wameamini na wakatenda mema kwa hakika tutawaingiza katika wema.