Aya 10 – 13: Katika Watu Kuna Wanaosema, Tumeamini
Imani Au Sarabi?
Maana
Na katika watu kuna wanaosema: Tumemwamini Mwenyezi Mungu. Lakini wanapoudhiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wanayafanya maudhi ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Aya hii inaleta picha ya uhakika ya baadhi ya watu tunaowajua na kuishi nao. Shetani amewapambia watu hawa kwa hila na wasiwasi wake, mpaka wakamsadiki, wakajiona ni katika watu wa takua na imani; kumbe hawaitakidi wala kuona kitu chochote isipokuwa manufaa na masilahi yao.
Hakuna kitu kinachofahamisha zaidi kuwa imani zao ni njozi na sarabi, kuliko kule kuhofia kwao watu japo kwa kitu kidogo tu. Wanawahofia itakapodhihiri haki na usawa kwa kauli au kwa vitendo; sawa na mawalii na wenye takua wanavyomhofia Mwenyezi Mungu.
Imetangulia ishara ya kundi hili katika Aya isemayo:
فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِنْهُمْ يَخْشَوْنَ النَّاسَ كَخَشْيَةِ اللَّهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً ۚ {77}
Huko nyuma tulisema kuwa hakuna yoyote anayeifuata haki ila ataitolea thamani kwa nafsi yake na vitu vyake. Vinginevyo watu wa haki na wanaoinusuru, wasingekuwa na ubora wowote. Tazama Juz. 2 (2: 153 – 157), kifungu cha ‘Thamani ya Pepo.’
Kuna Hadith isemayo: “Mwenye kumwogopa Mwenyezi Mungu huogopewa na kila kitu, na asiyemwogopa Mwenyezi Mungu haogopewi na chochote.”
Na itakapokuja nusra kutoka kwa Mola wako lazima watasema: Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi.
Waowakopamojanadiniikiwanibiasharayenyemasilahi,nawaoni maadui wa dini ikiwa itawataka wajitolee muhanga japo kidogo. Kauli fasaha zaidi katika maana haya ni ile ya Bwana wa mashahidi, Husein bin Ali (a.s.) pale aliposema: “Watu ni watumwa wa dunia na dini wameilamba kwa ndimi zao tu, inachukulika yanapokuwa mazuri maisha yao. Wapatwapo na misukosuko, wenye dini wanakuwa wachache.”
Umetangulia mfano wake katika Juz. 5 (4:141).
Kwani Mwenyezi Mungu hayajui yaliyomo vifuani mwa walimwengu?
Mnataka kumhadaa Mwenyezi Mungu na kumfanyia hila na yeye ni mjuzi wa mnayoficha na mnayoyadhihirisha?
Kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha wale ambao wameamini na kwa yakini atawatambulisha wanafiki.
Umetangulia mfano wake katika Aya 3 ya sura hii na Juz. 4 (4:154).
Na wale ambao wamekufuru waliwaambia walioamini: Fuateni njia yetu nasi tutayabeba makosa yenu.
Washirikina wa Makka waliwaambia wale walioitikia mwito wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.): Vipi mnamfuata Muhammad na kuvumilia mengi kwa ajili yake? Mwacheni na mrudi kwenye dini yetu. Ikiwa mnahofia adhabu ya Mwenyezi Mungu baada ya mauti, kama anavyowahofisha Muhammad, basi sisi tutawabebea. Walisema hivi wakikusudia kuwa ufufuo baada ya mauti ni porojo.
Wala wao hawatabeba katika makosa yao chochote kile. Hakika hao ni waongo.
Kwa sababu kila mtu atalipwa kwa matendo yake, hatabeba mzigo wa wengine au kuulizwa kwa niaba yake:
قُلْ لَا تُسْأَلُونَ عَمَّا أَجْرَمْنَا وَلَا نُسْأَلُ عَمَّا تَعْمَلُونَ {25}
Na kwa hakika wataibeba mizigo yao na mizigo mingine pamoja na mizigo yao.
Kila anayempoteza mwingine atabeba dhambi zake na dhambi za kupoteza; kwa sababu amesababisha kupatikana upotevu na kuenea. Ama yule anayemfuata mpotevu atabeba dhambi zake bila ya kupungua, kwa sababu aliitikia upotevu kwa hiyari yake.
Kwa maneno mengine ni kuwa mpotezaji ana dhambi mbili: Moja kwa upotevu wake na nyingine ni kwa kupoteza. Na mfuasi ana dhambi moja ya kupotea kwa hiyari yake.
Na kwa hakika wataulizwa siku ya Kiyama juu ya waliyoyazua ya kudai kwao kuwa Mwenyezi Mungu ana mshirika, kusema kwao kuwa Mtume (s.a.w.) ni mchawi, kuwaambia waumini kuwa watawabebea dhambi zao n.k.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُونَ {14}
فَأَنْجَيْنَاهُ وَأَصْحَابَ السَّفِينَةِ وَجَعَلْنَاهَا آيَةً لِلْعَالَمِينَ {15}