read

Sura Ya Thelathini na Mmoja: Luqman

Imeshuka Makka isipokuwa baadhi ya Aya. Ina Aya 34.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

الم {1}

Alif Laam Miim.

تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ {2}

Hizo ni Aya za Kitabu chenye hekima.

هُدًى وَرَحْمَةً لِلْمُحْسِنِينَ {3}

Ni uongofu na rehema kwa wafanyao wema.

الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ بِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ {4}

Ambao wanasimamisha Swala; na wanatoa Zaka na wana yakini na akhera.

أُولَٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِنْ رَبِّهِمْ ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ {5}

Hao ndio walio na uongofu utokao kwa Mola wao na hao ndio wenye kufanikiwa.

وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُهِينٌ {6}

Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipokujua na wanaichukulia ni mzaha. Hao watapata adhabu ya kufedhehesha.

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا وَلَّىٰ مُسْتَكْبِرًا كَأَنْ لَمْ يَسْمَعْهَا كَأَنَّ فِي أُذُنَيْهِ وَقْرًا ۖ فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ {7}

Na anaposomewa Aya zetu huzipa mgongo kwa kujivuna, kama kwamba hakuzisikia, kama kwamba masikioni kwake mna uziwi. Basi mbashirie adhabu chungu.

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتُ النَّعِيمِ {8}

Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema watakuwa na bustani zenye neema.

خَالِدِينَ فِيهَا ۖ وَعْدَ اللَّهِ حَقًّا ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ {9}

Watadumu humo. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kweli. Na Yeye ndiye Mwenye uwezo, Mwenye hekima.

خَلَقَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَنْ تَمِيدَ بِكُمْ وَبَثَّ فِيهَا مِنْ كُلِّ دَابَّةٍ ۚ وَأَنْزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنْبَتْنَا فِيهَا مِنْ كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ {10}

Ameumba mbingu bila ya nguzo mnazoziona na ameweka katika ardhi mlima ili ardhi isiwayumbishe na amewatawanya humo kila namna ya wanyama; na tumeteremsha maji kutoka mbinguni na tukaotesha katika ardhi mimea mizuri ya kila namna.

هَٰذَا خَلْقُ اللَّهِ فَأَرُونِي مَاذَا خَلَقَ الَّذِينَ مِنْ دُونِهِ ۚ بَلِ الظَّالِمُونَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ {11}

Huu ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Basi nionyesheniwameumba nini hao wasiokuwa Yeye! Lakini madhalimu wamo katika upotevu ulio dhahiri.