read

Aya 29 - 32: Huuingiza Usiku Katika Mchana

Maana

Je, huoni kwamba huuingiza usiku katika mchana na huuingiza mchana katika usiku.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 3 (3:26) na Juz. 17 (22:61).

Na amelitiisha jua na mwezi, vyote hupita mpaka wakati uliowekwa. Na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyafanya.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:2).

Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na kwamba walewanaowaomba badala yake ni batili, na hakika Mwenyzi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa.

Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 17 (22:62).

Je, huoni kwamba majahazi hupita baharini kwa neema za Mwenyezi Mungu, ili awaonyeshe ishara zake.

Miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu ni kusahilisha mawasiliano. Miongoni mwa mawasiliano hayo ni majahazi ambayo yanahitajia maji, upepo na mbingu. Sababu hizi zote zunaishia kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Hakika katika hayo kuna ishara kwa kila mwenye subira nyingi mwenye shukrani, anayevumilia machungu na kuchunguza ishara za Mwenyezi Mungu katika maumbile yake na kushukuru Mungu wake.

Na wimbi linapowafunika kama vivuli, humuomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini. Lakini anapowaokoa wakafika nchi kavu, wapo baadhi yao huenda mwendo wa wastani. Wala hazikanushi ishara zetu ila kila mhaini mkuu, kafiri mkubwa.

Baadhi ya wafasiri wamesema makusudio ya mwenye kwenda mwendo wa wastani hapa ni mwenye kuficha ukafiri wake. Razi akasema ni kafiri wa wastani. Lakini usawa hasa ni yule ambaye hakuidhulumu nafsi yake kwa kuipeleka kwenye hasira za Mwenyezi Mungu na adhabu wala hakuwa ni katika waliotangulia kwenye heri:

فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِنَفْسِهِ وَمِنْهُمْ مُقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّهِ ۚ {32}

“Kati yao yupo aliyejidhulumu nafsi yake na yupo wa wastani na yupo aliyetangulia katika mambo ya kheri” (35:32).

Makusudio ya mhaini mkuu hapa ni yule anayevunja ahadi ya umbile aliloumbiwa nalo kila mwenye kuzaliwa.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 11(10:22-23) na Juzuu hii tuliyo nayo (29:65-66)

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ وَاخْشَوْا يَوْمًا لَا يَجْزِي وَالِدٌ عَنْ وَلَدِهِ وَلَا مَوْلُودٌ هُوَ جَازٍ عَنْ وَالِدِهِ شَيْئًا ۚ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُمْ بِاللَّهِ الْغَرُورُ {33}

Enyi watu! Mcheni Mola wenu na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwanawe wala mwana hatamfaa mzaziwe kwa lolote. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Basi yasiwadanganye maisha ya dunia wala asiwadanganye na Mwenyezi Mungu mdanganyifu.

إِنَّ اللَّهَ عِنْدَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ {34}

Hakika ujuzi wa Saa uko kwa Mwenyezi Mungu na huiteremsha mvua na anavijua vilivyo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho, wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, mwenye habari.