read

Sura Ya Thelathini Na Mbili: As-Sajda

Ina Aya 30. Mwenye Majmaul-bayan anasema: Imeshuka Makka isipokuwa Aya tatu zimeshuka Madina; kuanzia 18 – 20.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

الم {1}

Alif Laam Miim.

تَنْزِيلُ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ {2}

Ni uteremsho wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake, kinachotoka kwa Mola wa walimwengu wote.

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۚ بَلْ هُوَ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ لِتُنْذِرَ قَوْمًا مَا أَتَاهُمْ مِنْ نَذِيرٍ مِنْ قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ {3}

Au wanasema amekizua? Bali hicho ni haki itokayo kwa Mola wako, ili uwaonye watu wasiofikiwa na mwonyaji kabla yako, huenda wakaongoka.

اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ مَا لَكُمْ مِنْ دُونِهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا شَفِيعٍ ۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ {4}

Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake katika siku sita. Kisha akatawala kwenye Arshi. Hamna walii wala mwombezi isipokuwa Yeye. Basi je hamkumbuki?

يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِمَّا تَعُدُّونَ {5}

Hulipanga jambo kutoka mbinguni hadi ardhini, kisha linapanda kwake katika siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyohisabu.

ذَٰلِكَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ {6}

Huyo ndiye Mjuzi wa mambo ya ghaibu na ya dhahiri, Mwenye uwezo, Mwenye kurehemu.

الَّذِي أَحْسَنَ كُلَّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ۖ وَبَدَأَ خَلْقَ الْإِنْسَانِ مِنْ طِينٍ {7}

Ambaye ametengenza vizuri umbo la kila kitu. Na akaanzisha umbo la mtu kwa udongo.

ثُمَّ جَعَلَ نَسْلَهُ مِنْ سُلَالَةٍ مِنْ مَاءٍ مَهِينٍ {8}

Kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji hafifu.

ثُمَّ سَوَّاهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِنْ رُوحِهِ ۖ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۚ قَلِيلًا مَا تَشْكُرُونَ {9}

Kisha akamlinganisha sawa na akampulizia roho yake. Na amewajaalia kusikia na kuona na nyoyo. Ni uchache mnavyoshukuru.