Aya 10-14: Wakosefu Wanainamisha Vichwa Vyao.
Maana
Na husema: Ati tutakapopotea ardhini, kweli tutakuwa kwenye umbo jipya?”
Hii ni sawa na kauli yao:
أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ ۗ أُولَٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ ۖ {5}
Bali wao wanakanusha kukutana na Mola wao.
Unaweza kuuliza: Washirikina walitangaza waziwazi kufuru yao ya kukutana na Mwenyezi Mungu waziwazi. Sasa kuna haja gani ya kusema wanakanusha kukutana na Mola wao? Si ni sawa na kumwambia aliyetangaza ukafiri kuwa wewe ni kafiri?
Jibu: makusudio ni kuwa wao hawakuipinga akhera kwa ujuzi, bali ni kwa ujinga na kuiga; sawa na kumwambia aliyetangaza ukafiri: wewe ni mjinga.
Sema, atawafisha malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu.
Yaani, ewe Muhammad! Waambie waliokufuru kuwa nyinyi mtakufa tu, hilo halina shaka. Baada ya mauti hakika itawafunukia na mtajua kuwa bila shaka saa ya Kiyama itakuja na kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua walio katika makaburi.
Na ungeliwaona wakosefu wanavyoinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao.
Walipinga ufufuo na wakawafanyia maskhara waliouamini, waliowapa mwito wake na kuwahadhari na mwisho mbaya. Watapofufuliwa na kusimama mbele ya Mola wao kwa ajili ya hisabu watainamisha vichwa vyao kwa kuona haya na majuto na kusema:
Mola wetu! Tumeona na tumesikia, turejeshe tutatenda mema, kwani hakika sisi tuna yakini.
Umetangulia mfano wake katika Juz.7 (6:27) na Juz. 18 (23:99 – 100).
Na lau tungelitaka tungeipa kila nafsi muongozo wake.
Razi anasema: “ Hii ni wazi kuwa madhehebu yetu yako sahihi pale tunaposema: Mwenyezi Mungu hakutaka imani kutoka kwa kafiri na hakutaka kwake isipokuwa kufuru.”
Nasi tunamwambia Razi: Ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyetaka kufuru kwa kafiri, na hakuna anayerudisha matakwa yake, basi kwa nini atamwadhibu. Vipi na Yeye ndiye aliyesema: “Wala hatukuwadhulumu, bali wao ndio waliokuwa madhalimu” (43:76).
Usahihi ni kuwa makusudio ya matakwa ya Mwenyezi Mungu hapa ni matakwa ya kiuumbaji ambayo ni kusema ‘kuwa.’
Yaani lau Mwenyezi Mungu angelitaka kuwalazimisha uongofu wangeliongoka. Na kama angelifanya hivyo, basi kusingekuwa na thawabu wala adhabu. Hayo tumeyaeleza mara kadhaa. Tazama Juz. 6 (5:49 – 50).
Lakini imehakikika kauli kutoka kwangu: Kwa hakika nitaijaza Jahannam kwa wote majini na watu.
Imehakikika kauli kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba ataijaza Jahannam kwa wafisadi na wale walioasi kwa hiyari na matakwa yao wenyewe. Ama wale ambao walimwitikia Mola wao wana maghufira na malipo makubwa. Kuna Hadith Qudsi inayosema: “Nimeiumba Pepo kwa anayenitii hata kama ni mtumwa Muhabeshi; na moto kwa anayeniasi hata kama ni bwana wa kikuraishi.”
Basi onjeni kwa sababu ya kusahau mkutano wa siku yenu hii, hakika sisi tumewasahau. Na onjeni adhabu yenye kudumu kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
Hakuna yoyote aliyefuata matamanio yake na hawa yake ila atamsahau Mwenyezi Mungu na hisabu na ataikufuru haki na dhamiri. Na kesho malaika wa adhabu watamwambia mkosaji huyu: umelewa utamu wa dunia basi leo onja uchungu wa akhera. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:51) na Juz. 10 (9:67).
إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا الَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِهَا خَرُّوا سُجَّدًا وَسَبَّحُوا بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ۩ {15}
تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ {16}
فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {17}
أَفَمَنْ كَانَ مُؤْمِنًا كَمَنْ كَانَ فَاسِقًا ۚ لَا يَسْتَوُونَ {18}
أَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ جَنَّاتُ الْمَأْوَىٰ نُزُلًا بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {19}
وَأَمَّا الَّذِينَ فَسَقُوا فَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۖ كُلَّمَا أَرَادُوا أَنْ يَخْرُجُوا مِنْهَا أُعِيدُوا فِيهَا وَقِيلَ لَهُمْ ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ الَّذِي كُنْتُمْ بِهِ تُكَذِّبُونَ {20}
وَلَنُذِيقَنَّهُمْ مِنَ الْعَذَابِ الْأَدْنَىٰ دُونَ الْعَذَابِ الْأَكْبَرِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ {21}
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنْتَقِمُونَ {22}