read

Sura Ya Thelathini Na Tatu: Ahzab

Imeshuka Madina, Ina Aya 73.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ اتَّقِ اللَّهَ وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا {1}

Ewe Nabii! Mche Mwenyezi Mungu wala usiwatii makafiri na wanafiki. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا {2}

Na fuata uliyoletewa wahyi kutoka kwa Mola wako. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyatenda.

وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ وَكِيلًا {3}

Na mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa.