read

Aya 56 – 58: Mswalieni Mtume

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.

Makusudio ya Mwenyezi Mungu kumsalia Mtume ni kumridhia kumrehe- mu na kumsifu kwa kila kheri, swala ya malaika ni kumsifu, na kutoka kwa waumini ni kumwombea dua ya kuwa na daraja ya juu. Imam Ar-Ridha (a.s.) aliulizwa kuhusu maana ya Mwenyezi Mungu, malaika na waumini kumswalia Mtume, akasema: “Swala kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni rehema, kutoka kwa malaika ni kumsifu na kutoka kwa waumni ni kumwombea.”

Kuswaliwa huku hakuhusiki na risala ya Muhammad (s.a.w.) peke yake. Kila mtu anayetumia desturi ya risala ya Muhammad (s.a.w.), kuifundisha au kuijulisha au kutaja fadhila yoyote katika fadhila zake basi atakuwa amemswalia, awe mumin au sio mumin, akitaka hilo au asitake.

Imam Ja’far As-Sadiq (a.s.) anasema: “Mtu kumswalia Muhammad (s.a.w.) ni kama kusema: “Subhanallah walhamdulillah walailaha illaha wallahu akbar” (Kutakasika ni kwa Mwenyezi Mungu na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu na hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni mkubwa).

Imam hapa anakusudia kuwa thawabu za kumswalia Mtume ni sawa na thawabu za tasbih, tahmid, tahlil na takbir. Imepokewa Hadith kutoka kwa Mtume mtukufu (s.a.w.), amesema: “Bakhili wa kweli ni yule ambaye niki- tajwa mbele yake haniswalii.

Vipi Tutamswalia Mtume?

Katika Sahih Al-Bukhariy Juz. 8, mlango wa kumswalia mtume, Tafsir At- Tabariy, Tafsir Ar-Raziy, Tafsir Al-Maraghi na wafasiri wengineo, pia katika vitabu vya Hadith, kuna maelezo haya: “Mtume aliulizwa: Vipi tutakuswalia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: semeni:

Allahumma swalli a’la muhammdi wa a’la aali Muhammad, kama swal-layta a’la Ibrahima wa a’laa aali Ibrahim, Innaka hamidum majiid Allahumma barik ala muhammdi wa a’la ali Muhammad, kama barakta a’la Ibrahima wa a’la ali Ibrahim, Innaka hamidum majid.

(Ewe Mwenyezi Mungu mswalie Muhammad na kizazi cha Muhammad, kama ulivyomswalia Ibrahim na kizazi cha Ibrahim, hakika wewe ni mwenye kusifiwa mwenye kutukuzwa. Ewe Mwenyezi Mungu mbariki Muhammad na kizazi cha Muhammad, kama ulivyombariki Ibrahim na kizazi cha Ibrahim. Hakika wewe ni Mwenye kusifiwa Mwenye kutukuzwa.)

Katika tafsir Ruhul-bayan ya Ismail Haqiy, amesema: “Inatakikana mwenye kuswali aseme: Allhumma swali a’la Muhammad wa a’la AliMuhammad” kwa kulirudia neno ‘a’la’; kwani Sunni wanaweka neno hilo kabla ya aali, kuwapinga Shia ambao hawaliweki neno hilo.

Sisi hatuoni tofauti yoyote baina ya anayesema: neno hilo na asiyelisema. Ama kuhusu ile Hadith isemayo: “Mwenye kutenganisha baina yangu na kizazi changu, hatapata shafaa yangu,” Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi usahihi wake.

Imam Shafii naye amesema katika shairi lenye maana hii: Enyi watu wa nyumba ya Mtume pendo lenu ni faradhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu amelieleza katika Qur’an. Inawatosha kuwa ni cheo kikuu kwamba nyinyi asiyewaswalia hana Swala

Hakika wale ambao wanamuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha.

Makusudio ya kumuudhi Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kumghadhabisha, na sababu yenye kuwajibisha hilo ni kumpinga, kumnasibishia mshirika au mtoto, au kuasi hukumu miongoni mwa hukumu zake. Na kuumuudhi Mtume (s.a.w.) ni kupinga utume wake au kupuuza mwenendo wake.

Laana kutoka kwa Mungu ni kwa kuwekwa mbali na rehema yake na kuto- ka kwa watu ni shutuma na kuombewa mabaya. Katika Nahjul-balagha imeelezwa: “Mwenyezi Mungu amewalaani wanaoamrisha mema na kuacha kuyatenda na wanaokataza maovu na wanayoyatenda.”

Na wale ambao wanawaudhi waumini wanaume na waumini wanawake pasi na wao kufanya, hakika wamebeba dhulma kubwa na dhambi kubwa.

Pasi na wao kufanya, yaani kufanya kosa linalostahili udhia. Kuudhi kunakuwa ni kwa kusengenya, vitimbi, uzushi n.k. Kuna Hadith zisemazo: “Mwislamu ni yule ambaye watu wamesalimika na mkono wake na ulimi wake.”

“Utukufu wa mumin ni kwa kujizuia na kuwaudhi watu.” “Aliye dhalili zaidi katika watu ni yule anayewadharau watu.”

Imam Ali (a.s.) anasema: “Mwenye hali mbaya zaidi katika watu ni yule asiyemwaamini yeyote kwa dhana zake mbaya, na asiyeaminiwa na yeyote kwa vitendo vyake vibaya.”

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِنْ جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَنْ يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا {59}

Ewe Nabii! Waambie wake zako na wake za waumini, wajiteremshie jalbab zao. Hilo ni karibu zaidi kuweza kujulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

لَئِنْ لَمْ يَنْتَهِ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ وَالْمُرْجِفُونَ فِي الْمَدِينَةِ لَنُغْرِيَنَّكَ بِهِمْ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَا إِلَّا قَلِيلًا {60}

Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na wale wanaoeneza fitna Madina, hawataacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu.

مَلْعُونِينَ ۖ أَيْنَمَا ثُقِفُوا أُخِذُوا وَقُتِّلُوا تَقْتِيلًا {61}

Wamelaaniwa! Popote waonekanapo, na wakamatwe na wauliwe kabisa.

سُنَّةَ اللَّهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلُ ۖ وَلَنْ تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّهِ تَبْدِيلًا {62}

Ni desturi ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika desturi ya Mwenyezi Mungu.