Aya 59 – 62: Wajibu Wa Hijabu
Lugha
Kuna kauli nyingi kuhusu neno Jalbab: kuna wanaosema kuwa ni nguo inayomfunika mwanamke kutoka kichwani hadi nyayoni. Wengine wakasema ni ushungi unaofunika kichwa cha mwanamke na uso wake. Kauli hii ndio aliyo nayo mwenye Majmaul-Bayan.
Maana
Zimekwishatangulia Aya mbili zinazofahamisha wajibu wa hijabu kwa wanawake:
Ya kwanza ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Wala wasidhihirishe uzuri wao ila kwa waume zao.” Juz. 18 (24: 31). Ya pili ni ile Aya ya 53, katika Sura hii tuliyo nayo: “Na mnapowaomba chombo cha nyum- bani, basi waulizeni nyuma ya mapazia.”
Aya iliyo wazi zaidi ya hizi mbili ni hii tuliyo nayo, isemayo:
Ewe Nabii! Waambie wake zako na wake za waumini, wajiteremshie nguo zao.
Kusema kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘wajiteremshie nguo zao’ inaenea kusitiri na kufunika sehemu zote za mwili, kikiwemo kichwa na uso. Hilo linatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:
Hilo ni karibu zaidi kuweza kujulikana wasiudhiwe.
Waislamu, mwanzoni walikuwa wakitoka bila ya kujitanda, kama ilivyokuwa desturi ya kijahiliya, ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akamtaka Mtume wake mtukufu, katika Aya hii, awaamrishe wake zake kujisitiri na kuvaa hijabu. Na amri inafahamisha wajibu. Kwa hiyo hijabu ni wajibu.
Hata hivyo uso na viganja viwili havimo kwenye wajibu huu, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ {31}
Hilo ni karibu zaidi kuweza kujulikana kutokana na kujistahi na kujichunga. Kwani hijabu ni kinga baina ya mwanamke na tamaa ya watu wenye shakashaka na mafasiki, wasiudhiwe kwa kuangaliwa na mafasiki.
Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
Anasamehe yaliyopita na anamuhurumia mwenye kutubia na kurejea nyuma.
Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na wale wanaoeneza fitna Madina, hawataacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu.
Wanafiki walificha ukafiri na wakadhihirisha imani. Wanaoeneza fitna ni watu katika wananfiki waliokuwa wakieneza propaganda dhidi ya Mtume (s.a.w.) na maswahaba na wakawatia shaka wale wadhaifu wa imani ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewaletea ibara ya wenye mardhi nyoyoni mwao. Aya inatoa onyo la kuuawa na kufukuzwa wanafiki, waeneza fitna na wale watakaowasikiliza, ikiwa hawatajizuia na upotevu na ufisadi wao.
Vita Vya Nafsi
Siku hizi kueneza fitna kunaitwa ‘vita vya nafsi.’ Nguvu ya shari imetafuta njia nyingi sana za kueneza uongo na mambo ya ubatilifu kwa kila nyenzo. Kuanzia magazeti, radio, runinga, sinema, hotuba, vipeperushi, shule, vyuo, vitabu n.k.
Vyombo hivi vimekaririka masikioni mwa watu kila siku, kiasi ambacho uhakika haupati nafasi kwa watu na wenye ikhlasi, isipokuwa kwa mwamko mkamilifu na elimu itakayotangulia propaganda za wakoloni na wazayuni.
Nimesoma kwenye gazeti linaloitwa Akhabar Al-yawm la Misr, la 13/12/69, kwamba Israil ina magazeti ya propaganda yanayofikia 890 ulimwenguni kwa ajili ya kueneza habari za uongo. Zaidi ya hayo wametawala vyombo vingi vya habari ulimwenguni, kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja; kama vile runinga, radio n.k.
Kwenye mahisabu haya hayaingii magazeti ya Beiruti yenye uhusiano mkubwa na wakoloni na wazayuni.
Kwa vyovyote iwavyo, Alhamdu lillah, Israil imehisi mapigo kutoka kwa waarabu na kwamba propaganda zao zilizotengenezwa na Marekani, na kutangazwa na vibaraka, zimeanza kujulikana.
Wamelaaniwa! Popote waonekanapo na wakamatwe na wauliwe kabisa.
Wamelaaaniwa na kila ulimi, kwa sababu dini yao ni pesa na matendo yao ni udanganyifu, uwongo na hadaa. Hawana dawa isipokuwa kuuawa popote walipo; kama kiungo kilichoharibika, kisipokatwa kitaharibu mwili wote.
Ni desturi ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika desturi ya Mwenyezi Mungu.
Makusudio ya desturi ya Mwenyezi Mungu hapa ni hukumu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa mpotevu anayepoteza, ambayo ni kuuliwa ambako amekuwekea sharia, ambaye imetukuka hekima yake, tangu zamani. Hukumu hii itabakia milele bila ya mabadiliko wala mageuzi.
يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِنْدَ اللَّهِ ۚ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا {63}
إِنَّ اللَّهَ لَعَنَ الْكَافِرِينَ وَأَعَدَّ لَهُمْ سَعِيرًا {64}
خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ لَا يَجِدُونَ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا {65}
يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا {66}
وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا {67}
رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا {68}
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ آذَوْا مُوسَىٰ فَبَرَّأَهُ اللَّهُ مِمَّا قَالُوا ۚ وَكَانَ عِنْدَ اللَّهِ وَجِيهًا {69}