Aya 63 – 69: Wanakuuliza Kuhusu Saa
Maana
Watu wanakuuliza kuhusu Saa. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu tu. Na nini kitakachokujulisha? Pengine hiyo saa iko karibu.
Makusudio ya saa ni Kiyama Umetangulia mfano wake katika Juz. 9 (7:187).
Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri moto unaowaka. Watadumu humo milele. Hawatapata mlinzi wala wa kuwanusuru. Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungelimtii Mwenyezi Mungu na tungelimtii Mtume!
Makafiri na waasi kesho watasukumwa kwenye adhabu ya moto, hawatakuwa na msaidizi wala udhuru. Watauma vidole vyao kwa kujutia walivyomuasi Mwenyezi Mungu na Mtume, lakini ‘majuto ni mjukuu.’
Umetangulia mfano wake katika Juz. 19 (25:27).
Na watasema: Mola wetu! Hakika sisi tuliwatii mabwana zetu na wakubwa wetu, wakatupoteza njia. Mola wetu wape adhabu mara mbili, na walaani laana kubwa.
Makusudio ya mabwana na wakubwa ni viongozi wa dini na dunia. Laana ni kufedheheka. Wadhaifu watawageuzia adhabu na watamtaka Mwenyezi Mungu awaongezee adhabu.
Mwenye kuichunguza historia ataona kwamba aghlabu umma wa kijinga unaongozwa na mataghuti na waovu. Lakini watu wenye mwamko na maarifa hawaamini kuweka masilahi yao isipokuwa kwa waaminifu wenye ikhlasi.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:38).
Enyi ambao mmeamini! Msiwe kama wale ambao walimuudhi Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtaksa na waliyoyasema; naye alikuwa ni mwenye heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.
Waliomuudhi Musa (a.s.) ni Wana wa Israil, hilo halina shaka; ambapo walimsifu sifa zisizokuwa za mitume.
Aya hii inaashiria kwamba badhi ya swahaba walimuudhi Mtume mtukufu (s.a.w.) na wakambandika mambo asiyokuwa nayo, ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawakataza waislamu hilo.
Kuna riwaya inayosema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) siku moja aliapa, basi mtu mmoja katika Answar akasema: “Kiapo hiki hakikusudiwa radhi ya Mwenyezi Mungu.” Hapo uso wa Mtume ukaiva wekundu na akasema: “Amrehemu Musa, hakika aliudhiwa zaidi ya hivi na akasubiri.”
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا {70}
يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا {71}
إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَنْ يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنْسَانُ ۖ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا {72}
لِيُعَذِّبَ اللَّهُ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْمُشْرِكِينَ وَالْمُشْرِكَاتِ وَيَتُوبَ اللَّهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا {73}