Imeshuka Makka. Ina Aya 54.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي الْآخِرَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ {1}
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na sifa ni zake katika Akhera. Naye ni Mwenye hekima, Mwenye habari.
يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنْزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۚ وَهُوَ الرَّحِيمُ الْغَفُورُ {2}
Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni na yanayopanda huko na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwingi wa maghufira.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَأْتِينَا السَّاعَةُ ۖ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأْتِيَنَّكُمْ عَالِمِ الْغَيْبِ ۖ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِنْ ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُبِينٍ {3}
Na walisema wale ambao wamekufuru: Haitatufikia Saa. Sema: Ndio! Naapa kwa Mola wangu, itawafikia. Mjuzi wa ghaibu. Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo katika hivyo wala kikubwa zaidi; ila vimo katika Kitabu chenye kubainisha.
لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۚ أُولَٰئِكَ لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ {4}
Ili awalipe wale ambao wameamini na wakatenda mema. Hao watapata maghufira na riziki yenye heshima.
وَالَّذِينَ سَعَوْا فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُولَٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مِنْ رِجْزٍ أَلِيمٌ {5}
Na wale ambao wamehangaika kuzipinga ishara zetu wakiona watashinda, hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu.
وَيَرَى الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ الَّذِي أُنْزِلَ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ هُوَ الْحَقَّ وَيَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ {6}
Na wale ambao wamepewa ilimu wanaona kuwa uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako ni haki na huongoza kwenye njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.