Aya 7 – 9: Wanaopinga Siku Ya Mwisho
Maana
Na wale ambao wamekufuru walisema: Je, tuwajulishe mtu anayewaambia mtakapochambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya? Amemzulia Mwenyezi Mungu au ana wazimu?
Hivi ndivyo washirikina walivyomwambia Muhammad, ni muongo au mwendawazimu – Mungu apishie mbali. Kwa nini walisema neno la ukafiri kama hilo? Ni Kwa sababu Mtume aliwaambia kuwa mtu atafu- fuliwa baada ya mauti. Hawana dalili yoyote ya kupinga kwao huku isipokuwa kushangaa tu; kama walivyosema:
أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ {5}
Hali yao hii, kama inavyonekana, inategemea vile wanavyofikiria. Maana yake ni kupinga hali halisi kwa fikra na mawazo; pamoja na kuwa fikra haiwi ya kweli ila ikiwa inaakisi hali halisi na kwamba yeyote anayeikum- batia nadharia yoyote hana budi kutafuta dalili ya ukweli wake kwa kuweko uhalisi unaoitafsiri, na haifai kukana uhalisi kwa fikra isiyokuwa na msingi wowote.
Katika hili Imam Ali (a.s.) anaashiria kwa kusema: “Watu wanajulikana kwa haki, wala haki haijulikani kwa watu.”
Bali wale ambao hawaamini akhera wamo adhabuni na upotofu wa mbali.
Hao ni wajinga na wapotevu, kwa sababu wameipima haki na uhalisi kwa fikra zao na mawazo yao; na walitakiwa wapime fikra zao kwa haki na uhalisi.
Je, hawaoni yaliyo mbele yao na nyuma yao ya mbingu na ardhi.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawaambia wakadhibishaji: Kuna ajabu gani ya kufufuliwa kwenu baada ya mauti:
أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَنْ يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ ۚ {81}
Je, umbile hili halifahamishi umoja wake na ukamilifu wa uweza wake; ukiwemo kuwarudisha watu baada ya mauti?
Tumelizungumzia hilo mara nyingi. Tazama Juz. 1 (2:28 -29), Juz. 5 (4:85 – 87) na Juz. 11 (10:3–4).
Tungelipenda tungeliwadidimiza ardhini, au tungeliwateremshia vipande vya mbingu. Hakika katika hayo kuna ishara kwa kila mja aliyetubia.
Hayo ni ishara ya kuumba mbingu na ardhi. Kwa sabubu hilo, kwa mwenye akili, linafahamisha ukuu wa Mwenyezi Mungu na uweza wake wa kuipa uhai mifupa iliyochakafuka. Ama kauli yake Mwenyezi Mungu:
‘Tungelipenda tungeliwadidimiza ardhini,’ ni karipio na makemeo kwa yule anayepinga siku ya mwisho, kwamba anaweza kumezwa na ardhi au kupigwanakimondokutokambinguni,kimuunguze.
وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ مِنَّا فَضْلًا ۖ يَا جِبَالُ أَوِّبِي مَعَهُ وَالطَّيْرَ ۖ وَأَلَنَّا لَهُ الْحَدِيدَ {10}
أَنِ اعْمَلْ سَابِغَاتٍ وَقَدِّرْ فِي السَّرْدِ ۖ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ {11}
وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ غُدُوُّهَا شَهْرٌ وَرَوَاحُهَا شَهْرٌ ۖ وَأَسَلْنَا لَهُ عَيْنَ الْقِطْرِ ۖ وَمِنَ الْجِنِّ مَنْ يَعْمَلُ بَيْنَ يَدَيْهِ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖ وَمَنْ يَزِغْ مِنْهُمْ عَنْ أَمْرِنَا نُذِقْهُ مِنْ عَذَابِ السَّعِيرِ {12}
يَعْمَلُونَ لَهُ مَا يَشَاءُ مِنْ مَحَارِيبَ وَتَمَاثِيلَ وَجِفَانٍ كَالْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَاسِيَاتٍ ۚ اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا ۚ وَقَلِيلٌ مِنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ {13}
فَلَمَّا قَضَيْنَا عَلَيْهِ الْمَوْتَ مَا دَلَّهُمْ عَلَىٰ مَوْتِهِ إِلَّا دَابَّةُ الْأَرْضِ تَأْكُلُ مِنْسَأَتَهُ ۖ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ الْجِنُّ أَنْ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ الْغَيْبَ مَا لَبِثُوا فِي الْعَذَابِ الْمُهِينِ {14}