Aya 29 – 35: Aliyejidhulumu, Aliye Katikati, Na Aliyetangulia Kwenye Kheri
Maana
Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakasi- mamisha Swala, na wakatoa kwa siri na kwa uwazi katika tuliyowapa, wanataraji biashara isiyoangamia.
Makusudio ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni Qur’an Tukufu. Kusoma ni kuzingatia maana yake na kuyatumia. Kwa sababu kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu.... ‘iliyokuja baada ya kauli yake: ‘Hakika si mengineyo wanaomcha Mwenyezi Mungu, katika waja wake ni wale wajuzi.’ Inaashiria hivyo.
Katika Nahjul-Balagha kuna maelezo: “... Katika zama hizo hakutakuwa na kitu kisichokuwa na thamani zaidi kuliko kusomwa Qur’an inavyopaswa kusomwa kwake. Wala hakutakuwa na kitu kilicho na thamni zaidi kuliko Qur’an kutowekwa mahali pake.”
Maana ya Aya ni kuwa wale ambao wanazingatia Qur’an na wakatumia hukumu zake, wakikusudia radhi ya Mwenyezi Mungu, basi watakuwa wamepata faida kwenye biashara yao na watakuwa ni wenye kufuzu.
Amesema tena kwenye Nahjul-Balagha: “ ... Na wameuza machache kati- ka dunia hii isiyodumu kwa mengi ya akhera isiyoisha.”
Ili awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na awazidishie kutokana na fad- hila zake. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye shukrani.
Waliamini na wakamfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu, kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, thawabu zake, msamaha wake na rehema zake, na wakapata waliyoyataka.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 3 (2:274) na Juz. 13 (13:22).
Na yale tuliyokupa wahyi kutoka Kitabuni ni haki.
Makusudio ya Kitabu ni Qur’an ikiwa inachukua dalili na hoja za ukweli wake na uhakika wake; ambazo ni hukumu zake na mafundisho yake yanayoipa kipaumbele imani ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu na umoja wake na heshima ya mtu na uhuru wake.
Yenye kusadikisha yaliyokuwa kabla yake katika vitabu na sharia zinazosimama kwenye misingi hii – misingi ya kumwamini Mwenyezi Mungu na utu.
Hakika Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni Mwenye habari, Mwenye kuona yale yaliyo na masilahi kwao na yaliyo na ufisadi. Anawaamrisha lile na kuwakataza hili. Lakini Waislamu wameacha yaliyoamrishwa na Qur’an na wakafanya waliyokatazwa nayo. Wamesadikisha aliyoyasema Mtume mtukufu (s.a.w.) aliposema: “Utakuja wakati kwa umma wangu watakataza mema na kuamrisha maovu.” Kwa hiyo si ajabu kusalitika na viumbe waovu.
Kisha tumewarithisha Kitabu wale ambao tumewachagua katika waja wetu.
Makusudio ya Kitab ni Qur’an, hilo halina shaka yoyote; isipokuwa wafasiri wametofautiana katika makusudio ya waliochaguliwa. Wengi wakasema ni umma wa Muhammad (s.a.w.).
Tuonavyo sisi ni Muhammad (s.a.w.), Ahlu bayti wake, maswahaba wake na maulama wa umma wake wanaokwenda na sera yake na wakatumia sunna yake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hawezi kuwachagua isipokuwa wenye takua walio wema.
Qur’an Tukufu imelitumia neno hili kwa maana haya katika Aya kadhaa; miongoni mwazo ni:
إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ {33}
Ama dhamiri katika kati yao yupo aliyejidhulumu nafsi yake, na yupo wa katikati, na yupo aliyetangulia katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inarudia neno waja wetu, kwa vile ndilo lililo karibu.
Mwenye kujidhulumu ni yule ambaye maovu yake yamekuwa makubwa kuliko mema yake. Aliyetangulia katika heri ni ambaye mema yake yamekuwa makubwa kuliko maovu yake; hasa yule ambaye hana maovu. Aliye katikati ni ambaye mema yake na maovu yake yamekuwa sawa.
Hiyo ndiyo fadhila kuu. Mabustani ya milele watayaingia. Humo watavikwa vikuku vya dhahabu, na lulu, na mavazi yao humo ni hariri.
‘Hiyo’ ni hiyo hali ya kurithi na kuchaguliwa. Mabustani ya milele na kuendelea, ni ubainifu wa hiyo fadhila kuu ambayo ameifanya ni malipo ya wale aliowachagua.
Dhahabu,lulunahaririniibaranyingineyakauliyakeMwenyeziMungu:
وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنْفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ ۖ {71}
Kuna Hadith kuwa bedui mmoja alimuuliza Mtume: “Je, Peponi kuna samai, yaani nyimbo? Mtume (s.a.w.) akasema: “Ndio.”
Na watasema:, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu (Alhamdu lillah) ambaye ametuondoloea huzuni. Hakika Mola wetu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye shukrani. Ambaye ametuweka katika nyumba ya kukaa, humo haitugusi tabu wala humo hakutugusi kuchoka.
Watamshukuru Mwenyezi Mungu na kumsifu kwa kuwandolea hofu na kuokoka na moto na adhabu. Pia kuondokana na tabu na mashaka na kudumu kwenye neema na shangwe.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ نَارُ جَهَنَّمَ لَا يُقْضَىٰ عَلَيْهِمْ فَيَمُوتُوا وَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمْ مِنْ عَذَابِهَا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي كُلَّ كَفُورٍ {36}
وَهُمْ يَصْطَرِخُونَ فِيهَا رَبَّنَا أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ ۚ أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُمْ مَا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَنْ تَذَكَّرَ وَجَاءَكُمُ النَّذِيرُ ۖ فَذُوقُوا فَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ نَصِيرٍ {37}
إِنَّ اللَّهَ عَالِمُ غَيْبِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ {38}
هُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ ۚ فَمَنْ كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ ۖ وَلَا يَزِيدُ الْكَافِرِينَ كُفْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ إِلَّا مَقْتًا ۖ وَلَا يَزِيدُ الْكَافِرِينَ كُفْرُهُمْ إِلَّا خَسَارًا {39}