Aya 28 – 36: Nawasikitikia Waja Wangu
Maana
Na hatakuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala sisi si wenye kuteremsha. Hakuwi ila ukelele mmoja tu na mara wamezimia.
Kaumu yake, ni kaumu yake yule mumin aliyesema: ‘Wafuateni mitume.’ Makusudio ya jeshi la mbinguni ni malaika, na ukelele ni adhabu.
Maana ni kuwa kuangamia kwa wakadhibishaji ni jambo rahisi kwetu, lisilohitajia majeshi kutoka mbinguni. Bali ukelele mmoja tu, watakousikia, unawatosha kuyafanya majumba yao ni makaburi ya mili yao.
Ni sikitiko kwa waja. Hawakufika mitume ila wanamfanyia stihizai.
Kunga’ng’ania washirikina kukadhibisha mitume na kuwafanyia madharau ndiko kunakoleta masikitiko. Unaweza kuuliza: Ni nani anayesikitika na hali tunajua kuwa Mwenyezi Mungu(s.w.t.)hamsikitikiiyoyote?
Jibu: Masikitiko hapa ni kinaya cha mwendo wao mbaya na mwisho wao muovu ambao utawaletea masikitiko watakapoiona adhabu ya Jahannam na kujuta kwao walivyopoteza fursa katika maisha ya dunia.
Je, hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao?
Wanasikitika na kujuta kwa sababu hawakuchukua somo duniani kwa umma zilizowatangulia zilizoangamizwa na Mwenyezi Mungu walipowakadhibisha mitume.
Hakika hao hawarejei kwao.
Wafasiri wengi wa zamani na wapya, akiwemo Al-Maraghi na mwenye Dhilal, wamesema kuhusu maana ya jumla hii ni: Hawaoni wakadhibishaji kwamba tuliowaangamiza hawarudi tena duniani?
Lakini tafsiri hii inatakikana iangaliwe vizuri. Kwa sababu kukosa kurudi wafu daniani itakuwa ni hoja ya wakadhibishaji kuwa hakuna ufufuo; na wala si hoja juu yao.
Maana ya sawa – kwa tunavyodhania - ni kuwa je, hawakuona wakadhibishaji kwamba Mwenyezi Mungu amewangamiza waliopita wote na hakubaki yeyote wa kuweza kuwarudia wakadhibishaji kuwafahamisha habari ya wakadhibishaji wa mwanzo? Kinachofahamisha kuangamia kwao ni athari tu:
فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خَاوِيَةً بِمَا ظَلَمُوا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ {52}
Jumla hii inafanana na kauli yake Mwenyezi Mungu iliyo katika Aya ya 50 ya sura hii tuliyo nayo: “Basi hawataweza kuusia, wala hawatarejea kwa watu wao”
Na hapana ila wote watahudhurishwa mbele yetu.
Watu wote kesho watasimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuchukuliwa hisabau ya matendo yao, hilo ni lazima.
Na ishara kwao ni ardhi iliyokufa, tunaifufua na tukatoa ndani yake nafaka wakaila. Na tukafanya ndani yake mabustani na mitende na mizabibu, na tukachimbua chemchem ndani yake.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 7(6:99), Juz. 13 (13:4) na Juz. 17 (22:5).
Ili wale katika matunda yake na hayakufanywa kwa mikono yao, je hawashukuru?
Neema za Mwenyezi Mungu hazihisabiki wala hazidhibitiki. Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na waliyofanya kwa mikono yao,’ inaashiria kuwa neema ya kweli ni mali ya halali iliyochumwa kwa jasho, lakini mali ya haramu ni moto:
أُولَٰئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلَّا النَّارَ {174}
إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ {10}
Kutakata na mawi ni kwa ambaye ameumba jozi katika kila vinavyooteshwa na ardhi na katika nafsi zao na katika wasivyovijua.
Ametakasika kutokana na shirk, na ametakata na kutukuka kukubwa ambaye ameumba aina za wanyama, ndege, mimea na binadamu. Pia vile ambavyo hatuvijui katika mbingu na ardhini. Kila aina katika aina hizo inahitalifiana kirangi na kiumbo. Nyingine zinatofauti na kiladha; kama vile mimea na wanadamu kutofautiana kiakhlaki.
Wataalamu wanasema hata vitu vikavu vigumu vinafungamana kutokana na vitu viwili: chanya na hasi, na lau si hivyo basi kusingepatikana vitu. Wala hakuna chimbuko la hayo isipokuwa Mjuzi mwenye hekima. Ama sadfa haina nafasi na hawezi kuuikimbilia ila mzembe mwenye kujikwaza.
وَآيَةٌ لَهُمُ اللَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ النَّهَارَ فَإِذَا هُمْ مُظْلِمُونَ {37}
وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ {38}
وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ {39}
لَا الشَّمْسُ يَنْبَغِي لَهَا أَنْ تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ ۚ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ {40}
وَآيَةٌ لَهُمْ أَنَّا حَمَلْنَا ذُرِّيَّتَهُمْ فِي الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ {41}
وَخَلَقْنَا لَهُمْ مِنْ مِثْلِهِ مَا يَرْكَبُونَ {42}
وَإِنْ نَشَأْ نُغْرِقْهُمْ فَلَا صَرِيخَ لَهُمْ وَلَا هُمْ يُنْقَذُونَ {43}
إِلَّا رَحْمَةً مِنَّا وَمَتَاعًا إِلَىٰ حِينٍ {44}