Aya 71 – 76: Mikono Ya Mwenyezi Mungu Ndio Desturi Ya Ulimwengu Na Maumbile
Maana
Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono yetu wanyamahowa, na wao ni wenye kuwamiliki. Na tumewatiisha kwao. Basi baadhi yao wako wanaowapanda, na baadhi yao wanawala. Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru?
Wanyamahowa ni wanyama wa mifugo ambao ni ngamia, ngo’mbe, mbuzi na kondoo. Ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake; wanawala, wanakunywa maziwa yao, kutengenza majumba, samani, mavazi kutokana na ngozi, sufu na manyoya. Vile vile kuwabeba wao na mizigo yao kutoka sehemu moja hadi nyingine ambayo wangelifika kwa tabu.
Hilo amelikariri Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika Aya kadhaa; kama vile Juz. 8 (6:142) na Juz. 14 (16:5- 8). Lengo ni kuhimiza Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kushukuriwa na kutiiwa. Hilo ameliashiria kwa kauli yake: “Basi je, hawashukuru?” Katika Nahjul-Balagha imeelezwa: “Hata kama Mwenyezi Mungu asingelitoa kiaga kwa kuasiwa kwake, bado ingelikuwa ni wajibu kutoasiwa kwa kushukuru neema zake.”
Makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Kutokana na iliy- ofanya mikono yetu,” ni sababu za kimaumbile. Kwa vile Mwenyezi Mungu sio mwili, mpaka isemwe kuwa ana mikono hasa.
Ibn Al- Arabi anasema katika Futuhat: “Watu wa Mwenyezi Mungu wanawagawanya viumbe kwenye namna mbili: Kuna namna inayopatikana kwa ulimwengu wa amri kwa sababu neno “kun” (kuwa) ni amri. Na aina nyingine inapatikana kwa mikono ya sababu, wanaita ulimwengu wa maumbile. Haya yamefafanuliwa katika Juz. 3 (2:255) kifungu cha ‘Mwenyezi Mungu na desturi ya maumbile.’
Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu wapate kusaidiwa! Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio jeshi lao watakaohudhurishwa.
Yaani hao washirikina ndio jeshi la hayo masanamu. Maana ni kuwa masanamu hayawezi kuwanufaisha washirikina, lakini pamoja na hayo wao wanayalinda. Ni jambo la kushangaza sana kuwa mwenye akili anaabudu mawe yasiyodhuru wala kunufaisha.
La kushangaza sana ni kuwa wao wanayalinda yasiibwe au kuharibiwa na wakati huo huo wanayatarajia yawasaidie katika shida na kuwakurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Hayo yenyewe hayawezi kujisaidia yatawasaidiaje wengine.
Zaidi ya hayo yote, waabudu masanamu walimwambia Mtume (s.a.w.) kuwa yeye ni mwendawazimu. Kwa nini? Kwa sababu yeye haabudu mawe. Wao ndio wenye akili kwa sababu wanaaabudu yale wanayoya- chonga. Jambo la kushangaza kabisa.
Basi isikuhuzunishe kauli yao kuwa wewe Muhammad ni mwendawazimu, au mshairi au ni kuhani. Hakika Sisi tunayajua wanayoyaweka siri na wanayoyatangaza.
Walidhamiria chuki na kinyongo kwa Mtume (s.a.w.) na wakatangaza shutuma kwake na kwa mwito wake. Hakuna shaka kwamba Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa hilo na muweza wa kuwahisabu na kuwaadhibu. Basi hakuna haja ya huzuni na uchungu.
أَوَلَمْ يَرَ الْإِنْسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِنْ نُطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُبِينٌ {77}
وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَنْ يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ {78}
قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنْشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ {79}
الَّذِي جَعَلَ لَكُمْ مِنَ الشَّجَرِ الْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَا أَنْتُمْ مِنْهُ تُوقِدُونَ {80}
أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَنْ يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ ۚ بَلَىٰ وَهُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ {81}
إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَنْ يَقُولَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ {82}
فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ {83}