read

Sura Ya Thelathini: As-Saffat

Imeshuka Makka ina Aya 182

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

وَالصَّافَّاتِ صَفًّا {1}

Naapa kwa wanaojipanga safu-safu.

فَالزَّاجِرَاتِ زَجْرًا {2}

Na kwa wenye kuzuia sana.

فَالتَّالِيَاتِ ذِكْرًا {3}

Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.

إِنَّ إِلَٰهَكُمْ لَوَاحِدٌ {4}

Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.

رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ {5}

Mola wa mbingu na ardhi, na vilivyomo kati yake, na ni Mola wa mashariki zote.

إِنَّا زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِزِينَةٍ الْكَوَاكِبِ {6}

Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya dunia (karibu) kwa pambo la nyota.

وَحِفْظًا مِنْ كُلِّ شَيْطَانٍ مَارِدٍ {7}

Na kuilinda na kila shetani muasi.

لَا يَسَّمَّعُونَ إِلَى الْمَلَإِ الْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِنْ كُلِّ جَانِبٍ {8}

Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.

دُحُورًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ {9}

Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.

إِلَّا مَنْ خَطِفَ الْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ ثَاقِبٌ {10}

Isipokuwa anayenyakua kitu kidogo, na mara humfuatia kimondo kinachong’ara.