read

Aya 27 – 37: Watakabilana Wao Kwa Wao

Maana

Watakabiliana wao kwa wao kuulizana. Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kuume.

Neno yamin, tulilolifasiri kwa maana ya kuume, huwa lina maana nyingi; miongoni mwazo ni: mkono, upande usiokuwa wa kushoto na baraka na nguvu. Makusudo hapa ni kupoteza.

Wahalifu wataulizana na kulaumiana wakati watakapoiona adhabu. Wanyonge watawatupia lawama viongozi kuwa kama si nyinyi tunge- likuwa waumini. Hadaa hii wameiletea ibara ya kuume. Kwa sababu waarabu wanakiona kitu kinachokuja kwa upande wa kuume kuwa ni kizuri. Kwa hiyo kusema kwao mkitujia kwa upande wa kuume ni sawa na anayesema umenilenga hasa au umeniwahi kweli. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:38).

Watasema: Bali nyinyi wenyewe hamkuwa waumini. Na hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi mlikuwa waasi. Basi kauli ya Mola wetu imekwishatuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja. Tuliwapoteza kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.

Hii ni kauli ya viongozi wakiwajibu wale wanyonge, kwamba sisi kazi yetu ilikuwa ni kutoa mwito na kuupamba, nanyi mkauitikia. Nasi tuliwaita kwenye kufuru mkaitikia na mtume akawaita kwenye imani mkamkimbia, kwa sababu ya uhabithi na upotevu wenu. Vinginevyo sisi tuna uwezo gani juu yenu lau mngeliamua kumwamini Mwenyezi Mungu; kama walivyoamini wengine?

Kwa hiyo basi natija ya ukafiri wetu na upotevu wenu na kutuitikia ni kustahiki kauli ya adhabu kwetu na kwenu; kama muonavyo.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 20 (29:25) na Juz. 22 (33:67).

Basi hakika wao siku hiyo watashirikiana katika adhabu.

Haya ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Maana yake ni kuwa adhabu itawaangukia wote siku hiyo watakayolaumiana.

Hivyo ndivyo tutakavyowafanyia wakosefu.

Adhabu ya daima bila ya kutofautisha mfuasi na mwenye kufuatwa.

Wao walipokuwa wakiambiwa:Hapana Mola ila Mwenyezi Mungu (La ilaha illa Llahu) tu, wakijivuna.

Walijivuna na wajifanya wakubwa kuliko haki, ndio yakawapata yaliyowapata wajivuni waliokuwa kabla yao.

Na wakisema: Hivi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mshairi mwendawazimu?

Wafasiri wamesema kuwa washirikina walijichanganya kwenye maneno yao; pale walipomsifu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kuwa ni mshairi na mwenda wazimu, ambapo mshairi huwa anatumia akili kupangilia maneno yake kwa usanifu wa hali ya juu. Sasa mwendawazimu anaweza kweli kazi hii.

Bali ameleta haki, na amewasadikisha Mitume.

Hapana! Huyo si mshairi wala mwendawazimu isipokuwa ni Mtume mtukufu, ameleta haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na amewasadikisha Mitume waliomtangulia na vitabu vyao.

Baada ya hayo. Kwa hakika mwendawazimu ni bora kuliko yule aliyemsifu Muhammad, (s.a.w.) aliyeteulia na Mwenyezi Mungu na kumchagua kwa ujumbe wake na kumjaalia ni bwana na mwisho wa Mitume, kuwa ni mwendawazimu. Tazama tafsri ya (36:69) katika Juzuu hii tuliyo nayo.

إِنَّكُمْ لَذَائِقُو الْعَذَابِ الْأَلِيمِ {38}

Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.

وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ {39}

Wala hamtalipwa ila mliyokuwa mkiyafanya.

إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ {40}

Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliotakaswa.

أُولَٰئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَعْلُومٌ {41}

Hao ndio watakaopata riziki maalum.

فَوَاكِهُ ۖ وَهُمْ مُكْرَمُونَ {42}

Matunda, nao watahishimiwa.

فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ {43}

Katika Bustani za neema.

عَلَىٰ سُرُرٍ مُتَقَابِلِينَ {44}

Wako juu ya viti wameelekeana.

يُطَافُ عَلَيْهِمْ بِكَأْسٍ مِنْ مَعِينٍ {45}

Wakizungushiwa kikombe cha chemchem.

بَيْضَاءَ لَذَّةٍ لِلشَّارِبِينَ {46}

Cheupe kitamu kwa wanywao.

لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنْزَفُونَ {47}

Hakina madhara, wala hakimaliziki.

وَعِنْدَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ عِينٌ {48}

Na watakuwa nao wanawake wenye macho makunjufu.

كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَكْنُونٌ {49}

Kama kwamba wao ni mayai yaliyohifadhika.